KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Mimi ni mkazi wa Mtaa wa Kisoko, Kata ya Luchelele, Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza ninachojiuliza ni kuwa lini utatuzi wa barabara inayounganisha Mtaa wa Kisoko na Mtaa wa Silivini itatekelezwa?
Hii barabara haipitiki kwa usafiri wa gari kutokana na uwepo wa Korongo kubwa ambalo limetokana na mvua za msimu uliopita.
Kuna kipindi Mbunge wetu wa Jimbo la Nyamagana alituahidi Wananchi kuikamilisha lakini suala hilo bado halijatimizwa.
Ubovu wa Barabara hiyo unaleta changamoto kubwa na kusababisha kukwama kwa huduma za kijamii mtaani kwetu na maeneo ya jirani pamoja na masuala ya usafirishaji wa watu na mizigo.
Bidhaa mbalimbali zimekwama kutolewa upande mmoja kwenda mwingine, hata wale ambao wanakuwa na nia ya kwenda kuabudu pamoja na Wanafunzi wanaopita njia hiyo nao wanakuwa katika hatari.
Wakati wa mvua makorongo yanajaa maji na hali inakuwa ya hatari zaidi, tunaomba marekebisho yafanyike kwa wakati kabla ya msimu wa mvua kuanza inaweza kuleta athari zaidi kwa Wananchi wa mitaa hiyo.