DOKEZO Barabara ya Kongwa - Mpwapwa ni tatizo

DOKEZO Barabara ya Kongwa - Mpwapwa ni tatizo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Swahili AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
10,174
Reaction score
89,364
Hakika katika wilaya nchini zinazosababisha Tanzania kuendelea kuwepo kwenye kumi bora ya nchi zenye wanachi wasio na furaha basi hii wilaya ina mchango mkubwa.

Barabara ni ya vumbi na mbaya zaidi ina matuta madogomadogo a.k.a rasta ambapo kwa basi au gari mtikisiko unaotoka kwa kupita kwenye hii barabara unaweza ukaacha baadhi ya parts za gari njiani. Yani una vibrate mpaka mwili unakufa ganzi.

Huwezi kuongea na simu au hata kupiga stori na mtu sababu ya kelele zinazosababishwa na mtikisiko wa gari.
Serikali hebu fanyeni jambo hii wilaya ni kongwe hizo 45kms zilizobaki toka round about ya Kongwa mzutandike mkeka.
 
Attachments

Huku si ndiyo kwa yule Spika aliyekuwa mbunge kwa miaka 15? Hv ccm ya ilipokuwa inasema haipeleki maendeleo kwenye majimbo ya upinzani na badala yake watapeleke walikochagua ccm tu huwa waamanisha wapi?

Mbona hata huko kwa waliochagua ccm hali ni mbaya sana?
 
Changamoto ya rasta kwenye barabara nyingi za vumbi kwa sasa ni kutokana na kipindi kirefu cha kiangazi,maana nimegundua kuwa hata kama wakipitisha greda huwa haichukui muda inakufa tena, kilio hiki kiwafikie wahusika huko juu, wapitishe hata lami ya kiwango cha chini kwenye hizo barabara korofi,kwani kiukweli mateso yake ni mabaya sana hasa ukisafiri kwa basi...
 
Hakika katika wilaya nchini zinazosababisha Tanzania kuendelea kuwepo kwenye kumi bora ya nchi zenye wanachi wasio na furaha basi hii wilaya ina mchango mkubwa...
Njoo Kondoa-Kiteto/Kibaya
 
Kuna ile round about yao, da!! [emoji2957] [emoji2957] Nahisi Ndugai alikula zaidi ya 20%. Ukipita usiku unaweza kuhisi ni njia ya nyoka.

Back
Top Bottom