Kwani wana tatizo lipi? Muulize mkenya yeyote kuhusu raia wa S.Sudan ambao wanaishi nchini Kenya. Hutasikia jambo lolote negative kuwahusu. Infact kwa maoni yangu wao ndio 'model immigrants/refugees' nchini Kenya.
Huwa wapo busy na shughuli zao, wanafata sheria na huwa hawana fujo wala bifu na mtu yeyote yule. Tena wamekuwepo Kenya kwa muda mrefu sana na sio tu kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma, wapo wengi, sanasana kule mtaa wa Ngumo, Lang'ata jijini Nairobi.
Nina rafiki zangu wengi kutoka S.Sudan na nimefika Juba nikielekea mji wa Malakal, asikuhadae mtu na 'stereotypes' kuhusu S.Sudan. Licha ya vita vya muda mrefu jamaa wanajitahidi sana. Kule Juba wakenya wanachapa biashara sio mchezo. Kuna shule, maduka makubwa, hospitali hadi na benki za wakenya kule S.Sudan.
Nilishangaa kuona kwamba mashuleni wanatumia syllabus ya Kenya, mitihani na vitabu vya wanafunzi pia. Usidhani bendera yao ipo hivi kibahati bahati
View attachment 1689682