Barabara ya kutokea Rusumo haipitiki kwa siku mbili sasa

Barabara ya kutokea Rusumo haipitiki kwa siku mbili sasa

Kusanyeni Road Toll kwa kilometa ili Barabara ziweze kujengwa. Haya mambo ya 152 badala ya 500 sio mazuri kbisa. Barabra zinakufa, mfuko nao unakufa..

Mkuu hizo road tolls zinahitajika ili kujenga huku tu? Vipi madaraja ya salenda? Haya ni kasma ipi?

Barabara za kwingine nazo je hizo kasma ipi? Na hii miradi mingine yote kasma ipi ambayo huku kasma hiyo is not applicable hadi hali ikafikie hivi?
 
Si hapo sasa mimi mwezi 12 tumekaa kuanzia asubuhi mpaka saa sita usiku panakera sana hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni balaa mkuu kipindi cha nyuma nyakanazi wakat strabag wanarekebisha hyo njia ya saiv walitengeneza diversion huku kama unaenda kigoma basi ile njia ilikua ni balaa yan kama gari ikipata breakdown hapo hakuna service road wala nin mnakua mnasubiriana.
Ila saiv kutoka nyakanazi hadi lusahunga afadhali wameziba ziba mashimo balaa lipo nyabugombe huko
 
Niandikapo uzi huu ni kuwa hatimaye miraculously nimebahatika kutoka Nyabugombe katika barabara Rusumo kuelekea Rusahunga njia kuu iendayo Dar baada ya kuwepo hapo kwa siku karibia 2.

Kwa hakika hii haina tofauti na escape from Sobibo. Wengine wengi watoto na kina mama bado wapo pale.

Si chini ya magari 1000 kwa hesabu za haraka haraka yamekwama pale kutokana tu na ubovu tu wa barabara uliopo pale unaosababishwa na uzembe wa wenye mamlaka.

Ni usumbufu kiasi gani? Ni upotevu kiasi gani wa biashara? Ni uharibifu kiasi gani wa magari? Hakuna anaye jali?

Eneo lenyewe hili hakuna mitandao yoyote ya simu na hivyo hali kwa ujumla ni tete.

Hakuna askari polisi wala hakuna msaada wowote.

Hivi kweli barabara hii haina ukipa umbele wowote? Kweli hawa TANROADS wanaridhika kabisa na hali hii?View attachment 1340398View attachment 1340398View attachment 1340399View attachment 1340400View attachment 1340401
Hiyo barabara sasa ilivyo na lenzi mbinuo na mbinuko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa misifa Sasa wee hawajambo, watu wa kagera ni shida utakuta wanakwambia wao mkoa mzima wamesoma, kuna mmoja alisema kijiji chao kina ma professor saba.
Sasa sijui hao ma professor wana msaada gani.
Hali ya maisha kule inatisha jamani,kuanzia Lusahunga na vitongoji vyake hali ni tete hadi Rusumo.
Sasa balaa zaidi pita pale Mizani njia ya kati ile kuenda Ngara, kutoka Mizani penyewe, Nyakahura, Mulusagamba hadi ufike Ngara dooh!! Kuna umasikini wa hali ya juu sana.
Kwa kweli hii tz hii bado tuna Safari ndefu sana sisi.
Hapo chacha,Mimi huwa nawaita wasomi uchwara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumepita tarehe 12/02/2020 ukweli hii njia ni majanga inatia watu umasikini
IMG_20200212_163103.jpeg
IMG_20200212_165639.jpeg
IMG_20200212_163107.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumepita tarehe 12/02/2020 ukweli hii njia ni majanga inatia watu umasikiniView attachment 1356293View attachment 1356294View attachment 1356296

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kwa ambaye hajapita njia hii anaweza kubeza taarifa za hali ya dharura sana katika njia hii.

Inaonekana viongozi wakuu wataja kujali kutembelea huku baada ya yale ya mv Nyerere kutokea.

Kwa ufupi barabara hii imetelekezwa na haiakisi ukweli kuwa tuko busy kununua madege tena kwa cash money.

Jana 12/2 njia ilikuwa imefunga kabisa kwa malori yenye mzigo kuelekea boda.
 
Back
Top Bottom