Barabara ya lami iliyokuwa inajengwa Kigamboni mnadani imekamilika lakini bado imefungwa kusubiri uzinduzi; Wakati wananchi wakiendelea kutaabika

Barabara ya lami iliyokuwa inajengwa Kigamboni mnadani imekamilika lakini bado imefungwa kusubiri uzinduzi; Wakati wananchi wakiendelea kutaabika

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Eneo la kipande Cha barabara lililopo Kigamboni baada ya kuvuka daraja la mwl Nyerere linaonekana kukamilika lakini bado barabara hiyo imefungwa kusubiri uzinduzi wa kisiasa ilihali wanainchi wanaendelea kupata tabu!

Barabara hiyo ndiyo inayounganisha viunga vya kigamboni na maeneo Mhimu ikiwemo Hospital kubwa ya Vijibweni!

Ambulance zenye wagonjwa mahututi zinalazimika kuzunguka umbali mrefu kupitia barabara korofi Wakati kipande Cha lami hiyo kimekamilika!

Ombi langu kwa Serikali; Hiki kipande mkiendelea kukifunga kitawapotezea kura nyingi badala ya kuwaongezea kura! Wanainchi wakirugusiwa kupita haitazuia Uzinduzi kufanyika!

Wahusika fungueni barabara hiyo Ndungulile mtampa Wakati mgumu!

Update
Siku moja baada ya malalamiko hatimaye wamefungua

Mrejesho: Barabara ya lami iliyokuwa imefungwa Kigamboni leo imefunguliwa, tunashukuru Serikali kwa kusikia kilio cha wananchi
 
Unajenga kwa ajili ya Nani Kama watu wanataaabika ingali barabara ipo!
Wakati mwingine Bora kula dagaa kuliko pilau la masimango
Kwani mliambiwa Serikali ndio imeleta tetemeko, kwani sisi tuliahidi kuleta tetemeko ?
 
Mbona fly over ubungo imeanza kutumika bila kuzinduliwa... hao viongozi wa kigamboni wapuuzi
 
Mbona fly over ubungo imeanza kutumika bila kuzinduliwa... hao viongozi wa kigamboni wapuuzi
kamati ya roho mbaya inafurahia wanainchi wanavyotaabika utazan wakimbiz
 
Mkuu ile ya mpaka buyuni inajengwa lini?Kama hautojali niulizie kwa Ndungulile Wakati wa Kampeni za uchaguzi.
 
Mkuu ile ya mpaka buyuni inajengwa lini?Kama hautojali niulizie kwa Ndungulile Wakati wa Kampeni za uchaguzi.
Wajumbe wa huko pembamnazi na Buyuni ndiyo Mliomkata Makonda angewajengea
 
Wajumbe wa huko pembamnazi na Buyuni ndiyo Mliomkata Makonda angewajengea
🤣🤣Mkuu nina site Yale Yale Ila Sina mzuka wa kujenga maana barabara siielewi.Ngoja nivute pumzi huku huku Pugu.
 
Serikali ya kipuuzi sijawai kuona,kutaabisha wananchi ndio kauli mbiu yao
 
Barabara imenitesa sana leo, ikanibidi nipitr barabara za ndani ambazo sizijui, nimetumia zaidi ya dakika 30, nikajikuta ni.etokea pale pale nilipoingilia, imemikera sana.
 
Tuliza mshono hio barabara bado kidogo wanataka kuchora ile michiriz ya kati msigongane nlimskia huyo injinia wa apo akihojiwa majuz kwene tv
 
Tuliza mshono hio barabara bado kidogo wanataka kuchora ile michiriz ya kati msigongane nlimskia huyo injinia wa apo akihojiwa majuz kwene tv
Kuchora hiyo mistari na hadi kukauka inachukua muda gani!?
 
Back
Top Bottom