Barabara ya Mandela kilio hakiishi

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Unapokuwa na safari yako ambayo inahusisha Barabara ya Mandela Mkoa wa Dar es Salaam, kubali kubadili ratiba zako kwani lazima utakwazika tu.

Barabara imekuwa bize kupita maelezo ikipitisha malori, gari binafsi na gari za abiria.

Kero zaidi ambayo pia inachangia uwepo wa foleni ni asubuhi na jioni ingawa mchana pia kuna wakati tatizo hilo linakuwepo.

Tunaomba mamlaka husika iliangalie hili kwa ukaribu zaidi ikiwezekana utanuzi wa barabara ufanyike kama ilivyo Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kibaha.
 
Utanuzi wa barabara sio suluhisho
Suluhisho la kudumu limeshapatikana , ujenzi wa bandari kavu kwala vigwaza upo 99.9% kukamilika plan iliyopo ni kuwa mizigo toka bandarini itakua inapelekwa kule vigwaza , then malori ya kubeba mizigo ya mikoani na nchi jirani yatachukulia mizigo vigwaza instead ya kuja dsm
 
Barabara hovyo Kweli, huwa sipendi kabisa kukaa karibu na Malori yenye container na tanks, Hiyo bandari ya kwala kwani imefikia wapi maana ndio tiba ya hii kitu.
 
Dada zenu hapo dar waliozoea kugawiwa hela za mileage na madereva wataishi vipi ?
 
waondoe zile service roads ili barabara ziwe njia tatu kila upande.

Service roads ndiyo zinaleta foleni za kijinga maana wajanja ndiyo wanatumia zile halafu wanakata foleni na kuchomokea kwa mbele. Nyinyi mulioko kwenye foleni halali ndiyo munaokula hasara.
 
Mandela Road.

Aisee lazima uwe na shati mbili. Moja kwenye begi ya akiba.

Foleni +jasho lazima ukifika ofisini ubadali nguo
 
Hii barabara wameweka taa siku hizi?
 
Kwann Yale malori wasiyatafutie boda kupitia pugu huko yasisumbue barabara hii. Mana kinacholeta shida ni Ile milori kupita na gari za kawaida. Nipewe barabara yao tu
 
Inapelekwa kwa kutumia njia gani?
 
swali la msingi.
Labda reli ila kama ni barabara tunarudi palepale kwenye foleni.
Hapo hakuna swali la msingi kwa ambaye anafikiria sawa sawa
Yan wajenge bandari kavu lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa mizigo na magari. Afu watumie tena magari hayo hayo kubeba mizigo?

Mbona iko wazi kabisa ..treni ndo itakayotumika?
 
Kuna reli toka bandari hadi Vigwaza?
 
Foleni,harufu mbaya kuanzia Tabata mpaka Buguruni,ndio barabara inayoongoza bodaboda kuchomekea,daladala zinajaza kero tupu
 
Good solution, hilo liende sambamba na upanuzi wa barabara Vigwaza - Morogoro even boyond
 
Ata kama bandari kavu itaanza, Mandela road itaendelea kuwa na foleni, tatizo lipo buguruni, kulitakiwa kuwe na angalau fly over pale. Suluhisho ni fly over buguruni, Kuanzisha route ya daladala za tabata zingine zipite Tabata dampo, Kigogo Njia panda mpaka Karume, au kujenga BRT(Mwendokasi) ili kuyaachia malori Njia. Au kujenga barabara mbadala ya juu kutoka Tabata Matumbi hadi Rozana. Au kutengeneza Barabara bora ya mchepuko, kutoka Matumbi - SUKITA- Rosana itasaidia asubuhi gari zote za Kariakoo na posta kutofika buguruni sheli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…