Barabara ya Mbagala hadi Kongowe inatesa wananchi Serikali itupie jicho

Barabara ya Mbagala hadi Kongowe inatesa wananchi Serikali itupie jicho

selukeng'e

Member
Joined
May 11, 2015
Posts
10
Reaction score
24
Kwa wakazi wa Toangoma Kongowe Mkuranga Vikindu na hata abiria wanaotokea Dar kwenda Lindi, Mtwara, Songea na masasi watakuwa wameshakutana na kero ya kipande cha barabara kutoka Mbagala hadi Kongowe ambapo Barabara ni nyembamba sana.

Kero ya barabara hii hutokea pale mlima wa Kokoto ambapo ikitokea gari ikaharibikaa magari mengine huziba njia na kusababisha foleni kubwa mno aidha huwa haipiti wiki bila adha hii kutokea.

Jana kwa mfano abiria tulitembea kwa mguu kwa umbali mrefu sana.

Nashauri wahusikaa watafute ufumbuzi wa kipande hiki kwa masirahi ya nchi ukizingatia kwamba kwa sasa viwanda vingi vipo mkuranga na pia ndiyo njia kuu ya mikoa ya kusini nawasilisha.
photo_2024-10-17_13-57-15.jpg

Pia soma:
~ Meneja TANROADS aelezea ulipofikia mchakato wa Ujenzi wa Barabara ya Mbagala Mzinga - Kongowe - Kisemvule
~ Waziri Bashungwa: Tutapanua barabara ya Mbagala Rangitatu-Kongowe (km 3.8) na daraja la Mzinga na upanuzi wa barabara ya Mwai – Kibaki (km 11.6)
 
duh! kuna sehemu kuna bonde nadhani ni mtongani pale
wanaiba simu balaaa yaani kama upo kwenye gari na vioo viko wazi hatar sana... wadada wapanda boda boda ndio
wananyang'nywa pochi kila siku

Issue ni barabara hao vibaka kila sehemu wapo. Hiyo barabara kweli ni kero hasa sisi wandengereko tukiwa tunakuja mjini
 
Back
Top Bottom