Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Barabara kipande cha vumbi Michese Dodoma ni kero kubwa na baada ya njia rasmi ya magari kufungwa na inayokusudiwa na wasafiri kutopewa umuhimu sisi wakazi wa Michese tunateseka saana usafiri umekuwa mgumu saaana ni kama hatuna diwani wala serikali.
Njia rasmi ilifungwa kupisha SGR inayokwenda Wilaya ya Bahi sijui lini ujenzi utakamilika maana diversion ni ndefu inayoongeza gharama ya nauli
Picha mbili za mwanzo ni kipande cha vumbi, picha ya mwisho ni kipande cha lami