Barabara ya Mwenge-Tegeta itaisha lini?

Barabara ya Mwenge-Tegeta itaisha lini?

Status
Not open for further replies.
Barabara kweli inaelekea kuisha lakini mapungufu mengi sana na sehemu nyingi imeshaanza kubomoka huwa naona wanaweka viraka.

Njia za kuchapuka pembeni wameziweka haziendani na entrace za upande wa pili wa barabara kubwa. Yaani very risky mfano pale chini ukipita njia Africana kabla hujafika njia panda kunduchi ukitoka kituo cha Total kama unarudi Mwenge ni majanga hadi urudi tena kule njia panda kunduchi au uchukue risk arudi against magari yanayotoka Mwenge.

Hii ipo sehemu nyingi hivohivyo na kingo za madaraja wamejenga nusu nusu pale Tegeta naona juzi juzi wameengozea. Pia ajali nyingti zimetokea especially pale Tegeta darajani kwa uzembe wa hawa wajenzi wanaweka yale matofali magumu kati kati ya barabara bila tahadhari yoyote mida ya usiku ukitungua gari unaingia unaimalizia pale.

Angalau tunashukuru inaisha ila sijui itadumu muda gani maana traffic imeongezeka sana kwa wanaotumia njia ya Bagamoyo Msata kwenda mikoani. Tunategemea itaongezeka zaidi Bandari ya Bagamoyo ikianza.
 
Mbaya zaidi vivuko vya Zebra zimewekwa lakini mlemavu hawezi kupita na baskeli yake maana Zebra lakini inabidi uruke kikuta cha kati kati ya barabara.
 
Mimi sio mhandisi ila kwa kungalia jinsi ile mitaro ilivyojengwa ukilinganisha na barabara hata ahaviendeani. Kawaida mtaro huanzia lami inapoishia.
Mkuu pale makutano ya Africana /Bagamoyo rd ndo kichekesho,mtaro wa maji toka Sala sala unaishia barabarani.
TANROADS mbuzi huyo kwenye gunia!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom