KERO Barabara ya Ndegesera–Mwime–Machimboni, Manispaa ya Kahama ni mbovu sana

KERO Barabara ya Ndegesera–Mwime–Machimboni, Manispaa ya Kahama ni mbovu sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
May 30, 2025
Posts
47
Reaction score
71
Barabara ya Ndegesera–Mwime–Machimboni katika Manispaa ya Kahama imekuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na hali yake kuwa mbaya kwa muda mrefu.

Ubovu wa barabara hiyo unasababisha usumbufu na changamoto mbalimbali kwa watumiaji, hususan kina mama wajawazito, wagonjwa na waendesha vyombo vya moto, huku pia ukiongeza hatari ya kutokea kwa ajali.

Barabara hiyo haijawahi kufanyiwa matengenezo ya maana kwa muda mrefu, licha ya eneo hilo kuchangia mapato kwa Serikali kupitia shughuli za uchimbaji madini katika Mgodi wa Mwime.

Aidha, viongozi wa eneo hili hawajafanya mikutano ya kutosha na wananchi ili kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo.

Diwani wa eneo hili, Machibya Jidula Mabambasi, licha ya shughuli zake kuwepo katika eneo hilo, bado hatujaona hatua madhubuti za kushughulikia tatizo la barabara.

Tunaomba JamiiForums na mamlaka husika kusaidia kufikisha kilio chetu kwa Serikali ili hatua zichukuliwe kurekebisha barabara hiyo na kuhakikisha inakuwa salama na inapitika kwa urahisi.

Tunasisitiza kuwa ni muhimu viongozi kutekeleza wajibu wao kwa wananchi, hasa kwa maeneo yanayochangia mapato kwa Serikali, ili wananchi nao wanufaike na huduma bora za msingi.
 
Back
Top Bottom