Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwenu maharusi watarajiwa watia nia na hasa wale wa urais. Kuna maeneo nyeti ya nchi hii kwa hakika yatawabeba sana watia nia. Katika picha hii ni hali ya leo katika barabara hii kuu pande za wilaya ya Biharamulo na Ngara.

Kwa hakika pana mtaji wa kura za kutosha huko. Si kwa wenyeji tu bali hata kwa waitumiao njia hiyo na pia jamaa zao:

Fursa hiyo, kazi kwenu watia nia!
 
Environmental impact assessment report ya hii barabara imeshatoka nadhani soon wataanza michakato ya kutangaza tender...Yajayo yanafurahisha
 
Environmental impact assessment report ya hii barabara imeshatoka nadhani soon wataanza michakato ya kutangaza tender...Yajayo yanafurahisha

Huu ni uzi wa 2017:

Hali ya mbaya mno ya barabara Nyakanazi Rusumo vipaumbele vyetu ni nini?

Zingine hizi ni nyingi tu hiyo assessment ilikuwa ije toka nchi gani?

Madhila ya Barabara Rusahunga -Rusumo

Hata kurekebisha sehemu hizi 3 (nyamalagala, ngazi 7 na nyabugombe) mbaya zaidi zenye takribani 200m each nayo ilikuwa inasubiria assessment?

Au ni vile sasa wajumbe tunataka kuingia kazini?

Ama kweli yajayo yanafurahisha!
 
Sada hivi ni kukataa tuu, hakuna kuremba
 
Huyu mungu anaye jisifia vipi, hajaona hii barabara.?
 
Kuna kampuni ya kiitaliano ndo ilipewa hio kazi...kazi haijaanza leo wala jana. Bt now ishakamilika wataenda next stage...hio barabara ni 97km huwezi amka tu ukasema unaijenga.
 
Anyway mleta mada target yako ya hiyo barabara haina wapiga kura wengi pia watumiaji wakuu Ni madereva wa malori ambao Sio wapiga kura wa eneo Hilo na kura zao chache tu is not a big issue as far as votes are concerned
 
Rusahunga rusumo si inalami toka zamani kutokea kahama nyantakara? hiyo siilikuwa barabara ya bmlo rusahunga kweli?.
 
Kwa akili zenu hizi CCM mnazidi kutudhihilishia kuwa tumefanya makosa sana kuwaachia muiongoze hii nchi kwa miaka yote hii.

Kumbe mnafanya miradi kwa kuangalia kura sio kwa mahitaji ya kiuchumi ya nchi???

Asanteni sana. Tuna kila sababu ya Kumuweka ikulu Tundu Antipas Lissu mwaka huu, 2020
 
Kuna kampuni ya kiitaliano ndo ilipewa hio kazi...kazi haijaanza leo wala jana. Bt now ishakamilika wataenda next stage...hio barabara ni 97km huwezi amka tu ukasema unaijenga.

Hata kurekebisha sehemu mbaya zaidi hamna inasubiri beberu mtaliano?

Nani atawajibika na hasara ya mali na maisha inayotokea huku kila uchao kwa sababu tu ya ubovu wa barabara?

Rusahunga rusumo si inalami toka zamani kutokea kahama nyantakara? hiyo siilikuwa barabara ya bmlo rusahunga kweli?.

Umeona TANROADS au mamlaka yoyote inakanusha hilo?

Unadhani tunapowastahi na laghai zao za vishindo vya awamu ya tano huwa si kuwafichia aibu zao tu?

Ukiona hivi ujue ni zaidi ya too much. Ukweli mchungu nyingi za hadithi za vishindo vya awamu ya tano ni magumashi!

Gari hiyo ipo sasa hivi barabarani. Miti ile ikilega ni mweleka kisa barabara. Mitaa ya huku hiyo ni kawaida.

Hizo ni takribani 90km tu miaka nenda rudi hakuna hata ukarabati mdogo?
 
Soon hii road itakua historia...subira yavuta heri
 
Anyway mleta mada target yako ya hiyo barabara haina wapiga kura wengi pia watumiaji wakuu Ni madereva wa malori ambao Sio wapiga kura wa eneo Hilo na kura zao chache tu is not a big issue as far as votes are concerned

Haba na haba hujaza kibaba. Wanaoathirika na ikiwamo barabara hii jidanganyeni kuwa ni wachache:

Kwani wanaokufa na wanaoathirika hawana ndugu wala jamaa?

Watia moyo wa dhati kwa kuongezea na huku njia ya ikulu ni nyeupe pee!
 
Magufuli sio kiongozi anwawekwa pale na Polisi
 
Soon hii road itakua historia...subira yavuta heriView attachment 1530605

Kuwa historia ni jambo la kheri lakini uwajibikaji wa TANROADS kwenye sehemu mbaya zaidi 3 zilizopo huko kwa miaka zaidi ya 5 sasa uko wapi?

Au inasubiri hiyo history?

Watu wanakufa, uharibifu ndiyo hivyo. Kama hawawezi kufanya marekebisho hata minimal si waifunge tu ijulikane haipo?

Kuwa fair hii barabara haifai kwa matumizi ya binadamu.

Ni aibu kubwa kwa awamu ya tano kujitanabaisha kwa ubora wa miundo mbinu hasa kwa yeyote mwenye taarifa ya hali ilivyo katika barabara hii na kwa zaidi ya miaka 5 sasa.

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu. Mtoa nia yeyote atakaye wahi huko, atapokelewa kwa nderemo.

Kimya kingi kina mshindo mkuu!
 
Anyway mleta mada target yako ya hiyo barabara haina wapiga kura wengi pia watumiaji wakuu Ni madereva wa malori ambao Sio wapiga kura wa eneo Hilo na kura zao chache tu is not a big issue as far as votes are concerned
Kwahiyo sehemu zisizo na wapiga kura wengi maendeleo hampeleki lakini kodi mnachukua.
 
Kwahiyo sehemu zisizo na wapiga kura wengi maendeleo hampeleki lakini kodi mnachukua.

Haupo muda bora wa kuwatia adabu hawa jamaa kuliko huu. Yote wanayofanya ni siasa tu.

Wajumbe ambao ndiyo mahakimu wa haki safari hii watatukuta.

Hatudanganyiki!
 
Kupanga ni kuchagua mkuu...hakuna mtu anaweza kufanya kila kitu kila mahali kwa wakati mmoja,hatuna resources hizo...lazima zipo zitakazo anza na zitakazo chelewa...kila kitu kina muda wake...ww unadhani ktk ya hilo barabara na daraja la wami kipi kingeanza?au io na kigoma nyakanazi kipi kingeanza..now that ipo kwenye mchakato tuwe positive tuache kulalamika.
 
Kuna kampuni ya kiitaliano ndo ilipewa hio kazi...kazi haijaanza leo wala jana. Bt now ishakamilika wataenda next stage...hio barabara ni 97km huwezi amka tu ukasema unaijenga.
Acha kujitoa ufahamu,kwani daraja la busisi ilikuaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…