Barabara ya Tabata (segerea road) inazidi kuwa mbaya- TARURA mna mpango gani?

Insidious

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2020
Posts
749
Reaction score
1,023
Kile kilichoanza kama nyufa ndogo kwenye lami, sasa kimegeuka kuwa kero ya kila siku kwa watumiaji wa barabara hii. Kila kukicha, mashimo mapya yanaongezeka, lami inazidi kumomonyoka, na kuziacha gari, bajaji, bodaboda, na watembea kwa miguu wakiingia kwenye mtihani mkubwa wa usalama na uvumilivu.

Picha zinajieleza zenyewe na ni mfano tu ukiwa unaingia tabata: mbele tu ya kituo cha mafuta cha Puma, barabara imechakaa vibaya na kujaa madimbwi makubwa ya maji machafu yanayoficha kina halisi cha mashimo hayo. Hali ni mbaya zaidi karibu na mtaro wa maji ulio wazi hatari ya wazi kwa waendesha pikipiki na magari yanayojaribu kukwepa mashimo katikati ya barabara. Matokeo yake ni uharibifu wa vyombo vya usafiri, foleni zisizo na lazima, na hatari ya ajali kila saa.

Je, TARURA pamoja na serikali kwa ujumla mna mpango wowote wa kufanya matengenezo ya kiwango cha juu kwenye barabara hii kabla haijawa janga kabisa na kukata mawasiliano? Wananchi na watumiaji wa barabara hii tunahitaji suluhu ya kudumu ikiwemo mfumo mzuri wa mifereji na uwekaji wa lami imara na sio kuweka viraka vya muda vinavyosombwa na mvua.

IMG_4245.jpeg
IMG_4246.jpeg
IMG_4244.jpeg
 
Ni barabara gan???
Namaanisha inayotoka relini-segerea- kinyerezi???
 
View attachment 3645564View attachment 3645566View attachment 3645567
CCM washenzi wa tabia
 
Wakifanya matengenezo ya kudumu sasa hivi, mradi mwingine wa kupiga pesa mwakani utatoka wapi?
 
Hiyo ipo vizuri.uliza barabara za wilaya ya ubungo.Ukiondoa barabara ya morogoro ambayo imewashinda kuimmaliza toka magufuli afariki zingine zote ni za hovyo kama anavyofanya mahovyohovyo dereva wa awamu ya sita
 
Tanganyika inapitia kipindi kigumu sana
Utajiri wake unaliwa na watoto wa kambo. Kwao huduma zote za afya ni bure, mfadhili ni Tanganyika.

Juzi tumeambiwa kwamba ubavu wa Tanganyika unadaiwa matrilioni ya shilingi. Halafu, Kiranja wa fedha wa ubavuni kwa dharau anawaambia watoto wa kambo, msijali, hili deni litalipwa na Tanganyika
 
Mshana Jr
 
Mshana Jr
Hata ccm wenyewe wanajuta
 
Back
Top Bottom