CCM washenzi wa tabiaKile kilichoanza kama nyufa ndogo kwenye lami, sasa kimegeuka kuwa kero ya kila siku kwa watumiaji wa barabara hii. Kila kukicha, mashimo mapya yanaongezeka, lami inazidi kumomonyoka, na kuziacha gari, bajaji, bodaboda, na watembea kwa miguu wakiingia kwenye mtihani mkubwa wa usalama na uvumilivu.
Picha zinajieleza zenyewe na ni mfano tu ukiwa unaingia tabata: mbele tu ya kituo cha mafuta cha Puma, barabara imechakaa vibaya na kujaa madimbwi makubwa ya maji machafu yanayoficha kina halisi cha mashimo hayo. Hali ni mbaya zaidi karibu na mtaro wa maji ulio wazi hatari ya wazi kwa waendesha pikipiki na magari yanayojaribu kukwepa mashimo katikati ya barabara. Matokeo yake ni uharibifu wa vyombo vya usafiri, foleni zisizo na lazima, na hatari ya ajali kila saa.
Je, TARURA pamoja na serikali kwa ujumla mna mpango wowote wa kufanya matengenezo ya kiwango cha juu kwenye barabara hii kabla haijawa janga kabisa na kukata mawasiliano? Wananchi na watumiaji wa barabara hii tunahitaji suluhu ya kudumu ikiwemo mfumo mzuri wa mifereji na uwekaji wa lami imara na sio kuweka viraka vya muda vinavyosombwa na mvua.
View attachment 3645564View attachment 3645566View attachment 3645567
Utajiri wake unaliwa na watoto wa kambo. Kwao huduma zote za afya ni bure, mfadhili ni Tanganyika.Tanganyika inapitia kipindi kigumu sana
Mshana JrUtajiri wake unaliwa na watoto wa kambo. Kwao huduma zote za afya ni bure, mfadhili ni Tanganyika.
Juzi tumeambiwa kwamba ubavu wa Tanganyika unadaiwa matrilioni ya shilingi. Halafu, Kiranja wa fedha wa ubavuni kwa dharau anawaambia watoto wa kambo, msijali, hili deni litalipwa na Tanganyika
Brother nadhani hata ccm wamejiapiza hawatarudia tena hili kosaUtajiri wake unaliwa na watoto wa kambo. Kwao huduma zote za afya ni bure, mfadhili ni Tanganyika.
Juzi tumeambiwa kwamba ubavu wa Tanganyika unadaiwa matrilioni ya shilingi. Halafu, Kiranja wa fedha wa ubavuni kwa dharau anawaambia watoto wa kambo, msijali, hili deni litalipwa na Tanganyika
Hata ccm wenyewe wanajutaMshana Jr
Waziri wa Fedha na Mipango, Juma Malik Akil, amebainisha kuwa Zanzibar inaendelea kupata manufaa makubwa na hadhi ya kipekee ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa katika uimarishaji wa uchumi wake. Akizungumza wakati akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Juni 18, 2026, kufuatia uwasilishaji wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri Akil alifafanua jinsi ushirikiano huo unavyosaidia kurahisisha upatikanaji wa mitaji na mikopo.
Katika ufafanuzi wake, Waziri Akil aliweka wazi siri ambayo wengi hawakuijua kuhusu...
- Waufukweni
- deni la taifa zanzibar juma malik akil serikali ya mapinduzi zanzibar serikali ya muungano
- Replies: 10
- Forum: Jukwaa la Siasa