KERO Barabara ya Tabora Mjini hadi Igalula ni mbovu, inatutesa watumiaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Huu ndio muonekano wa Barabara ya kutoka Tabora Mjini kwenda kwenye Kata za Igalula, Goweko, Nsololo na Nyahua iliyo Wilaya jirani ya Sikonge.

Barabara hii ndio kama kiungo kikubwa cha Huduma za Jamii kwa maeneo hayo lakini kwa sasa Wananchi wanapata adha ya usafiri kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

Ikizingatiwa Kituo cha Afya kikubwa ambacho kipo Igalula ndio kikubwa ngazi ya Wilaya, hivyo Wananchi ambao wanapata changamoto kubwa kutoka ngazi ya Zahanati wanapewa rufaa kuelekea kituoni hapo, nao wanapata wakati mgumu kutokana na Barabara.
WhatsApp Image 2024-05-20 at 11.37.23_10bf9804.jpg

WhatsApp Image 2024-05-20 at 11.37.28_c37eb108.jpg

WhatsApp Image 2024-05-20 at 11.38.50_97f254f8.jpg

WhatsApp Image 2024-05-20 at 11.40.03_02820aa0.jpg

Mambo yakiwa magumu kutoka Kituo cha Afya Igagula wanapewa rufaa kwenda HospitalI ya Mkoa wa Tabora (Kitete), wote wanatumia Barabara hiyohiyo ambayo ni changamoto kutumiwa hasa na Vyombo vya Usafiri.

Upande wa nauli kwa sasa inakadiriwa kuwa Shilingi 8,000 hadi 10,000 wakati awali ilikuwa Shilingi 3,500, hiyo ni kwa usafiri wa gari ndogo kutoka Goweko hadi Tabora, hiyo ni kwa kuwa magari makubwa hayawezi kupita hapo.

Upande mwingine nauli ya pikipiki ni shilingi 25,000 mpaka Mjini kupitia Igalula ndevelwa

Gharama hiyo imeongezeka kwa kuwa ubovu wa Barabara unachangia magari mengi kuharibika na hivyo gharama kupanda.

Hivi karibuni, niliona Mbunge wa Jimbo la Igalula, Venant Daud Protas alizungumzia changamoto ya Barabara hii ninayoizungumzia, inaonekana naye ni kama amechoshwa na mazingira hayo na hajaona majibu.

Matengenezo ya Barabara hii - Barabara ya Tabora Mjini hadi Igalula yaanza kufanyiwa maboresho
 
Nilipita hapo 2020 kwenda Goweko.Nimemiss mbuzi choma hapo relini Goweko
 
Huu ndio muonekano wa Barabara ya kutoka Tabora Mjini kwenda kwenye Kata za Igalula, Goweko, Nsololo na Nyahua iliyo Wilaya jirani ya Sikonge.

Barabara hii ndio kama kiungo kikubwa cha Huduma za Jamii kwa maeneo hayo lakini kwa sasa Wananchi wanapata adha ya usafiri kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

Ikizingatiwa Kituo cha Afya kikubwa ambacho kipo Igalula ndio kikubwa ngazi ya Wilaya, hivyo Wananchi ambao wanapata changamoto kubwa kutoka ngazi ya Zahanati wanapewa rufaa kuelekea kituoni hapo, nao wanapata wakati mgumu kutokana na Barabara.

Mambo yakiwa magumu kutoka Kituo cha Afya Igagula wanapewa rufaa kwenda HospitalI ya Mkoa wa Tabora (Kitete), wote wanatumia Barabara hiyohiyo ambayo ni changamoto kutumiwa hasa na Vyombo vya Usafiri.

Upande wa nauli kwa sasa inakadiriwa kuwa Shilingi 8,000 hadi 10,000 wakati awali ilikuwa Shilingi 3,500, hiyo ni kwa usafiri wa gari ndogo kutoka Goweko hadi Tabora, hiyo ni kwa kuwa magari makubwa hayawezi kupita hapo.

Upande mwingine nauli ya pikipiki ni shilingi 25,000 mpaka Mjini kupitia Igalula ndevelwa

Gharama hiyo imeongezeka kwa kuwa ubovu wa Barabara unachangia magari mengi kuharibika na hivyo gharama kupanda.

Hivi karibuni, niliona Mbunge wa Jimbo la Igalula, Venant Daud Protas alizungumzia changamoto ya Barabara hii ninayoizungumzia, inaonekana naye ni kama amechoshwa na mazingira hayo na hajaona majibu.
karibu makibo
 
Acha wapambane na ujinga wao ni miongoni mwa mikoa ambayo CCM wana uhakika wa kushinda tena kwa kupikiwa wali na nyama tu inawatosha
 
Back
Top Bottom