KERO Barabara ya Temeke ni mbovu, wahusika hamuioni?

KERO Barabara ya Temeke ni mbovu, wahusika hamuioni?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ZINDAGI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
1,118
Reaction score
1,430
Kuna hali ya kutozijali barabara za Wilaya ya Temeke kwa kiasi kikubwa, wahusika ni kama hawajihusishi kabisa.

1. Barabara ya Temeke ina mashimo makubwa ambayo yanachangia kuharibu magari, kusababisha foleni, na kufika sehemu muhimu kwa wakati. Mashimo haya yapo tangu mvua za vuli za mwaka jana mpaka naandika uzi huu hayajawahi kufukiwa, hali ni mbaya sana.

2. Watu waliopewa zabunibya kisafisha mitaro na kufagia barabara, wanaacha uchafu na mchanga juu ya barabara bila kutolewa kwa kipindi chose, hii inasababisha kupungua kwa upana wa barabara na wakati mwingine uchafu na mchanga kurudi ktk mitaro na kuziba tena.

3. Load limit haifuatwi, barabara za mtaani zinapitwa na malori yenye uzito zaidi ya kiwango kilichoweka, hali ambayo inasabibisha barabara kutodumu kabisa.

Tuwaombe wahusika watimize wajibu wao.
 
Kipande cha Temeke Mwisho mpaka Pile kuna mashimo makubwa karibu na zile tuta hata gari ya juu inapata tabu
 
Kuna hali ya kutozijali barabara za Wilaya ya Temeke kwa kiasi kikubwa, wahusika nin
kama hawajihusishi kabisa.
1.Arabara ya Temeke ina mashimo makubwa ambayo yanachangia kuharibu magari, kusababisha foleni, na kufika sehemu muhimu kwa wakati.
Mashimo haya yapo tangu mvua za vuli za mwaka jana mpaka naandika uzi huu hayajawahi kufukiwa, hali ni mbaya sana.
2.Watu waliopewa zabunibya kisafisha mitaro na kufagia barabara, wanaacha uchafu na mchanga juu ya barabara bila kutolewa kwa kipindi chose, hii inasababisha kupungua kwa upana wa barabara na wakati mwingine uchafu na mchanga kurudi ktk mitaro na kuziba tena.
3.Load limit haifuatwi, barabara za mtaani zinapitwa na malori yenye uzito zaidi ya kiwango kilichoweka, hali ambayo inasabibisha barabara kutodumu kabisa.
Tuwaombe wahusika watimize wajibu wao
Mkuu hii hali iko Wilaya zote.
Umefika Kimara Makurunge, Umefika Kifuru, Umefika Mbezi Msakuzi, Je Kigamboni.
Njoo Mawezi to Kimanga kwenda hadi Kisukuru utaacha gari pembeni uchukue boda boda. Funga kazi fika Kisukuru useme unaenda Segerea kupitia njia ya Masilingi.
Kwa kifupi Barabara za Jiji la Daaslam zimechakaa ile mbaya.

Bandari kavu kila mahala na hivyo kufanya Malori HGV kuingia hadi Vichochoroni ni miongoni mwa uharibifu, chanzo kikuu ni Ubora hafifu wa barabara hizo kwa pamoja na Usanifu wa kiwango cha chini. Injiniaz wetu ni Zero Brain
 
Nachelea kusema bado Temeke hakujawa na barabara mbovu japo sikupingi.

Njoo Mbezi mzee utaziona mimi nipo huku Makabe barabara hata mtembea kwa miguu lazima awe na timing la sivyo atateguka au kuvunjika kabisa.zaidi kuna huyu mdau hapa alijaribu kufafanua baadhi ya sehemu.

 
Moja kati ya wilaya ambayo ilisahaulika ila kwa barabara wapo vizuri ni temeke na viunga vyake, kasoro labda temeke mwisho (sudani, na pile). ila sehemu zingine kama sijui huko buza kwa azizi ally kiwalani kijichi daah wanabarabara nzuri. 😆😆 nenda sehem zingine mfano kimara, kifuru, bonyokwa kimanga utalia
 
Back
Top Bottom