KERO Barabara za Mitaa ya Mbeya Mjini zimeharibika mno, hazipitiki. TARURA fanyieni kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Mbeya Mjini tunapata shida kubwa kipindi hiki cha mvua, barabara za mitaa zimeharibika sana, miundombinu imekua ni changamoto kubwa, barabara hazipitiki.

Maji yanapita barabarani, yaani unakuta barabara imekua kama mto, maji yanapita mengi. Serikali za mitaa hazina msaada, wala madiwani hawana habari yoyote.

Ni aibu kubwa sana kwa TARURA Mbeya Mjini, na viongozi wote wa Mbeya Mjini.

Your browser is not able to display this video.
 
Mbunge wenu Yuko busy na matamasha ya Ngoma za jadi , subirini. Nashangaa kwenye andiko lako hujamtaja. Huyo ndo mbunge anahangaika na vitu vidogo vidogo visivyo na tija kwa wananchi na kuacha mambo ya mhimu
 
Kuna kipande cha mafyati kupita old airport kwenda samora sec, yani madimbwi kama majaruba ya mpunga
Kweli Mbeya mmetulia na Tulia
πŸ˜‚πŸ˜€πŸš€
 
Ametajwa kwenye video iliyoambatanishwa na habari mkuu
 
Kuna kipande cha mafyati kupita old airport kwenda samora sec, yani madimbwi kama majaruba ya mpunga
Kweli Mbeya mmetulia na Tulia
πŸ˜‚πŸ˜€πŸš€
Kweli, ni kama majaruba ya mpunga kabisa, yaani Mbeya haina hadhi ya jiji kabisa.
 
Yaani Mbeya ni kijiji kikubwa, haina hadhi ya kuwa jiji kabisa. Barabara za mitaa Mbeya mjini ni majanga matupu, hazipitiki kabisa..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…