Barabara za Mtaa Kibaha Maili Moja hali ni mbaya, Mbunge kaingia mitini, DC na RC wameuchuna tu

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257

Haya ndio Maisha yetu watu wa Kibaha Maili Moja, hii ni sehemu tu ya mfano mdogo jinsi changamoto ya Barabara ilivyo hasa mvua zinaponyesha.

Watu wameshapiga kelele sana kuhusu hii Barabara inayoanzia Kituo cha Sheli kuelekea Muheza hadi Mpiji, sasa hivi magari hayapiti kwa urahisi, yakipita ni kwa tabu na mengine yanakwama.

Bodaboda ndio kila siku watu waanguka kutokana na ubovu wa Barabara.

Tunateseka hivi Mbunge wetu Koka yupo, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa na watendaji wengine wapo.

Wakiwa na jambo lao la kukimbiza Mwenge na kuzindua miradi yao mingine ya mchongo wanavizia wakati ambao sio msimu wa mvua, wakijua wataleta katapira litachonga Barabara kisha wao wapite, baada ya hapo ni vumbi.

Ndio maana mimi huwa sina shobo za kwenye kwenye mishe zao kama hizo kwa kuwa najua hakuna cha maana kitakachozungumzwa, ukiwambia kuhusu Barabara wanarukaruka tu, ahadi nyingi hakuna utekelezaji.


 
Yote tisa kumi, aina ya udongo wa hapo Kibaha ni mbaya sana, kipindi cha masika(mvua ikinyesha) matope yakuwa ya hovyo sana kutembea kwa miguu inakuwa shida.

Udongo unaonyonya maji bila kutengeneza matope ndio mzuri sana, hata mvua ikinyesha hauwezi kuona adha kama hiyo.

Suluhu ya hapo Kibaha, barabara za mitaani zijengwe kwa angalau kiwango cha Moramu.

Vumilieni uchaguzi season is around the corner watawatengenezeeni za mchongo za kuwahadaa ili wapite wakajinyakulie vitita kwa mwezi kwenye jumba lao huko Idodomya
 
Hiyo barabara upana ni mitaa ngapi mkuu
Mnataka lami hapo au mumwagiwe kifusi

Ova
 
Kama unamsubiri Koka basi.
Huyo atakuwa anaishi zake Masaki, hana habari na jimbo lake.

Hivi kuna Mbunge hata mmoja ambaye hana makazi Dar na badala yake ana makazi jimboni kwake/mkoani lilipo jimbo?
 
Pesa zimeelekezwa kununua V8 za wapambe wa uchaguzi mwakani
 
Hii ndio Tanzania, hapo watatizama kisha watapuuzia kama kawaida yao
 
Poleni sana watu wa Kibaha, Ila kuna balaa nimeliona jana katika barabara za jimbo la ukonga jijini Dsm, mfano kutoka kituo cha pale Mombasa kwenda bomba mbili mpaka kwa mhaya ile zaidi ya Adhabu.
 
We unaongelea habari za 'Swekeni' wakati hapa mjini 'Daslam' hali ni mbaya kuliko huko.
Ninyi ni baadhi ya wale mnaomini makazi mwisho Ubungo kuelekea mjini (Dar). Tembea uone; maisha ya sasa si yale ya mwaka 1990/2000
 
Shida ya hii barabara kipande cha kuanzia Shell kupitia kwa Mchicha hadi hapo juu njia panda ni nyembamba sana; magari hayapishani vzr. Kwa wembamba huo mvua zikinyesha ni kero kama hiyo. Hao wa pembeni wangekubali fidia wapishe upanuzi wa barabara. Angalau kuanzia njia panda hadi kuelekea Mailimoja Shule hadi Stone pitch ni pana kiasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…