Barabara za Tandika ni changamoto, mashimo makubwa mno

Barabara za Tandika ni changamoto, mashimo makubwa mno

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Kuna hii changamoto ya barabara za Tandika aisee ni mtihani mkubwa Serikali za mitaa usiku wajaribu kuangalia namna ya kufukia mashimo makubwa sana ambapo kuna zingine gari ndogo upiti Mimi Jana nimepasua sampo oil yote imemwagika wananchi hata kuweka kifusi wakati mamlaka zinajipanga kukarabati
 
Kama pale. Buguruni sokoni mbele ya ofisini za serikali ya mtaa sijui, kuna shimo pale kama mgodi wa dhahabu halafu ofisi zao wamepaka na rangi nyeupe kabisa
 
Halafu barabara za Tandika zimekuwa za muhimu sana kukwepa foleni za Kilwa rd ila zinachofanywa ni Mungu pekee anajua!!

Malori yanayotoka mikoa ya Kusini kwenda Kaskazini ndiyo yanayoharibu hizi barabara! Ni barabara nyepesi, si za kupitisha mizigo mizito! Sijui nchi haina sheria hii!!?

Pili, ukweli uwekwe wazi! Gondwe ana kazi nzito sana, hakuna wilaya zembe kama wilaya ya Temeke si kwenye kuzoa uchafu, mitandao ya maji safi na taka na hadi kuziba mashimo ya barabarani! Wilaya ya Temeke ni zembe, zembe, zembe sijapata kuona
 
Back
Top Bottom