Halafu barabara za Tandika zimekuwa za muhimu sana kukwepa foleni za Kilwa rd ila zinachofanywa ni Mungu pekee anajua!!
Malori yanayotoka mikoa ya Kusini kwenda Kaskazini ndiyo yanayoharibu hizi barabara! Ni barabara nyepesi, si za kupitisha mizigo mizito! Sijui nchi haina sheria hii!!?
Pili, ukweli uwekwe wazi! Gondwe ana kazi nzito sana, hakuna wilaya zembe kama wilaya ya Temeke si kwenye kuzoa uchafu, mitandao ya maji safi na taka na hadi kuziba mashimo ya barabarani! Wilaya ya Temeke ni zembe, zembe, zembe sijapata kuona