Kwanini Baraka Da Prince licha ya kuweza kuimba hatoweza kuja kurithi kijiti cha Diamond
1.Mziki wa sasa hivi ili uweze kua kwenye peak unahitaji promo..promo inakuaje? promo ni pale unapokua umetoa video yako ukaipeleka T.V station itapigwa mara 2 tu baada ya hapo ni nguvu zako kuomba mashabiki wawe wanairequest nyimbo kwenye vipindi tofauti tofauti..cha pili ni kutoa hela ili nyimbo yako ipigwe Diamond kutoa 10mil kwa ajili ya promo kwake sio issue...
2. Scandal hizi zinasaidia sana mtu kuwa current Diamond alikua na scandal nyingi sana magazetini hata zingine jamaa alikua analipa hela ili aweze kuandikwa rejea akina dudubaya na mr nice enzi wanatamba walikua wanatokea sana kwenye magazeti sasa msanii gani mwenye uwezo wa kutoa hela au mwenye akili za kuweza kufanya hivyo? ndo mana harmonize alishazushiwa anamla rose ndauka wasioelewa industry inakwendaje lazima watakua na majina kimziki lakini pesa hakuna
3. Diamond ameweza kujibrand ndo mana deals za matangazo yumo rejea coca cola, azam(unga wa sembe) Tiffa na NMB baraka da prince ni brand?nani Tanzania anaweza fanya shoo yake mwenyewe kukodi ukumbi Diamonds are forever? hivi wewe huna brand huna scandal hausisimui watu nani atakuja? diamond ana fan base kubwa..walalahoi,uwezo wa kati na wenye uwezo mkubwa...
Hitimisho: Hakutawahi kuja kua na msanii aliewahi wekeza pesa nyingi kwenye mziki kama Diamond(promo), Diamond yupo tayari kutumia pesa nyingi kulipia promo nani anaweza kufanya hivyo? kusurvive mziki wa bongo ni zaidi ya kujua kuimba...na kuandika mistari mizuri
via in the industry...