Baraka kubwa zaidi maishani huwa hazina bei ,lakini ni za thamani isiyoelezeka

Baraka kubwa zaidi maishani huwa hazina bei ,lakini ni za thamani isiyoelezeka

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,043
Tunalipa kodi, tunalipa bili za maji, umeme, nauli na mengine mengi ya maisha , lakini hatujawahi kulipia pumzi.

Tunapata aleji ya vyakula, mafuta, dawa, na hata vumbi , lakini hakuna binadamu mwenye aleji ya oksijeni.
Tumshukuru Mungu kwa hilo.

Je, si hilo peke yake linatosha kumshukuru Muumba?

🕊️ Lakini kuna sauti nyingine ya dhamira inatuonya, Tochi ya maisha huwashwa na aliye juu, na hakuna binadamu aliyepewa funguo ya kuzima mwanga huo.

Sisi si waamuzi wa uhai ,hatukupewa mizani ya uamuzi huo. Uhai si mzigo wa kuondolea mwingine, bali ni zawadi ya kuilinda.
Tusijipe mamlaka ya Mungu katika miili ya wanadamu.

Kwa mwezi huu wa Juni 2025.
  1. Pumzika kwenye neema isiyo na gharama
  2. Tembea kwa shukrani, sio kwa kiburi
  3. Sema kwa upole, tafakari kwa kina, na tenda kwa huruma
  4. Na ujue,Wapo wanaotamani hata sekunde moja ya pumzi unayoipata bure
🙏🏽 Karibu Juni , mwezi wa kutambua kuwa si kila kitu tunachopata kimya kimya ni cha kawaida.
Pengine kile hatulipii, ndicho kilicho cha thamani zaidi.



-Chavalikungu PhD
East Africa Catholic University
Nairobi-Kenya
 
Back
Top Bottom