Baraka Shamte aliyemkosoa Rais wa Zanzibar, ajeruhiwa, akufukuzwa uanachama CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio Taarifa mpya iliyotufikia usiku huu, inadaiwa kwamba mtu huyu mzalendo, aliyetekwa na kunusurika kuuawa na Janjawidi pamoja na Mazombie, ambao ni watekaji maalum wa Zanzibar (Tanganyika wanaitwa wasiojulikana), hata baada ya kuokotwa na Majeraha makubwa bado ametimuliwa ndani ya CCM.

Bado haijajulikana ni vikao gani vya ccm vya ngazi ipi vilivyokubaliana kumfuta uanachama.

Pia soma: Shamte: Katiba ya nchi haijasema 'Head of State' atawale miaka 10, miaka mitano ikiisha tutafute Rais mwingine lakini siyo huyu

======
CCM Mkoa wa Mjini Zanzibar imemfukuza Uanachama Mwanasiasa Baraka Shamte ikisema ni sababu amekashifu madaraka ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi hadharani.

Uamuzi huu umekuja baada ya Shamte kuzungumza mambo mbalimbali na video yake kusambaa huku moja ya kauli zake ikisema: “Ukitaka utajiri acha uongozi ukafanye biashara, miiko ya uongozi haifuatwi”.

Imeelezwa kwamba Mzee Baraka Shamte amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja Zanzibar kutokana na kupigwa na Watu wasiojulikana ambapo Polisi Zanzibar, leo wamekiri kupokea taarifa za kujeruhiwa kwa Mzee huyu mwenye umri wa miaka 83 akiwa eneo la Unguja Ukuu.

==================
Your browser is not able to display this video.

Baraka Shamte akizunguma kuhusu utawala wa Zanzibar​

SERIKALI YALAANI SHAMTE KUJERUHIWA



TAMKO LA JESHI LA POLISI ZANZIBAR


 
CCM Mkoa wa Mjini Znz imemfukuza Uanachama Mwanasiasa Baraka Shamte ikisema ni sababu amekashifu madaraka ya Rais Dr. Hussein Mwinyi hadharani.

Uamuzi huu umekuja baada ya Shamte kuzungumza mambo mbalimbali na video yake kusambaa huku moja ya kauli zake ikisema “ukitaka utajiri acha uongozi ukafanye biashara, miiko ya uongozi haifuatwi”

Imeelezwa kwamba Mzee Baraka Shamte amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja Zanzibar kutokana na kupigwa na Watu wasiojulikana ambapo Polisi Znz leo wamekiri kupokea taarifa za kujeruhiwa kwa Mzee huyu mwenye umri wa miaka 83 akiwa eneo la Unguja Ukuu.
 
CCM kuua ni jambo la kawaida sana
 
Alisema Mh Lema, wakitumaliza sisi watawageukia na nyie, sasa ccm uwaneni kabisa ili mtoane kafara,
....hicho kibabu cha 83 years nadhan wangekiua tu, kiliwazodoa sana akina Maalim.
 
Isije ikawa walimpigia miti Mzee wa watu,,

Maana kwenye adhabu zote hiyo ndy inauma Sana.
 
Mzee busara hakuna kabisa alikurupuka hata vijana wadogo kwenye chama hawawezi kuongea utumbo kama ule,amuulize mwenzake huku bara saizi anajuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…