Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Nikiangalia hili baraza la mawaziri, by all standards haliakisi sura ya Taifa na kwa hiyo halisaidii kwa namna yoyote kuimarisha umoja wa Kitaifa.

1. Hivi inawezekana vipi uje na baraza la Mawaziri la watu 23 lakini lenye Mawaziri Waislamu 3 tu?
Takwimu hizi ni 87% Wakiristo, na 13% Waislamu. Je, hii maana yake ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanaoweza kufanya kazi ya kuendesha serikali yetu katika nchi yetu more than 80% ni watu wa dini moja? Hili linaacha maswali mengi. Lakini haya sishangai, inaonyesha tu kuhusu ujeuri wa mamlaka za uteuzi, Waislamu hili suala wamelilamikia sana, Mwaka 2016 Sheikh Khalifa alilisemea, Kisha mwaka huu kwenye Waraka wa shura ya maimamu Sheikh Ponda alilisema.

Binafsi sioni kama ni weledi wa kiungozi kutoheshimu demography za nchi yako katika kuunda timu ya kufanya nayo kazi. Naiona kama ni udini wa dhahiri tu ambao unashuhudiwa na aina ya teuzi zilizofanyika toka muhula wa kwanza wa serikali hii!. Je, Waislamu wanapenda haya? - La hasha, lakini pamoja na hayo Wa kulaumiwa pia ni viongozi wao, hawajitambui, hawajielewi, wanapigana mishale wao kwa wao badala ya kusimama kwa sauti moja ya kuangalia maslahi ya watu wao. Angalau Sheikh Ponda anajitambua, aliliona hili.

2. Baraza la Mawaziri halina Waziri hata mmoja kutoka Zanzibar
Zipo wizara za muungano, hakuna waziri hata mmoja wa wizara hizo ambaye ni Mzanzibar. Ni yaleyale niliyoyasema kwenye nukta ya juu. Huwezi kuunda timu ya mambo ya nchi isiyozingatia demography za kitaifa. Kwa mfano Huwezi mathalani ukachukua watu kutoka Kanda moja ukaunda baraza la mawaziri halafu ukasema eti hawa vigezo vyao vinatosha, Well hata kama vinatosha je wao peke yao ndo wenye vigezo? . Lakini katika hili Wazanzibar wa CCM nao wajilaumu wenyewe, Wameamua kuitoa nchi yao kwa Tanganyika "iwasimamie" basi wacha nchi yao igeuzwe mkoa, yaani hata mawaziri kutoka kwao ni hiyari tena kama ilivyo mawaziri kutoka Mtwara, Mwanza au Tanga

3. Idadi ya Wanawake ni ndogo katika baraza zima la Mawaziri

Sijajua kama ilikuwa ni vision ya kitaifa au ni maono ya kiuongozi tu wa serikali za awamu ya tatu na nne. Lakini kuna kipindi tumewahi kuwaza 50/50. Japo kwa maoni yangu hiyo siyo hoja, lakini kwangu hoja ya msingi ilikuwa ni kuwa lazima katika vyombo vya mamlaka na maamuzi jinsia zote zionekane vizuri siyo kuwa na mfumo uliolalia upande mmoja kupita kiasi (mfumo dume), Sasa wanawake wa kutosha wapo, kwa nini baraza la mawaziri liwe na wanawake kiduchu sana kwenye hili baraza?

Kwa hiyo ukiniuliza kuhusu hili baraza nitakwambia kuwa:
a)
Hili baraza linanuka udini, ni as if Magufuli katuletea parokia ya Mtakatifu Joseph, haliakisi demography ya kitaifa ya kwamba nchi hii ina watu wengi wa imani zote hizi mbili. Nilitegemea kuona baraza lenye sura ya kitaifa, lakini naona baraza lenye sura ya Tanzania ya Kikristo zaidi

b) Hili ni baraza la Tanganyika, yawezekana vipi usiwe na baraza lenye waziri kamili hata mmoja Mzanzibar?

4) Ni baraza la Mfumo dume - Ratio ya akina mama katika baraza hilo siyo wakilishi, sioni ni kwa namna gani baraza hilo linasaidia kuondoa mfumo dume

Namshauri Magufuli atengue hilo baraza kabla ya kuliapisha. La sivyo litampa tabu kwenye kubalance force za kijamii za kitaifa.

Katika kipindi hiki ambapo jumuia ya kimataifa inamnyooshea kidole juu ya aina ya utawala wake, ingekuwa busara kujaribu kubalance force za ndani, ingemsaidia sana.

Ila akizidi kukataliwa ndani ya nchi na nje ya nchi, basi ajiandae kutumia miguvu zaidi kutawala katika kipindi hiki cha miaka mitano, kwa sababu kutakuwa na silent rejection ya utawala wake ndani ya nchi na hii itamsumbua sana!
 
Nimesoma bandiko na kuelewa hoja. Lakini sikubaliani na hoja hiyo. Nitaifupisha na kuihakiki hapa chini, tena kwa ufupi kabisa. Mleta bandika amejenga hoja ifuatayo:

  1. Kwa ajili ya kuimarisha umoja wa kitaifa, Baraza la Mawaziri linapaswa kuakisi uanwai wa kijamii katika Taifa kwa kuwa na wajumbe wanaoakisi uwiano mwafaka wa sekta za kidemografia zilizomo katika Taifa;
  2. Baraza la Mawazi lililotangazwa na Rais Magufuli jana halina uwiano mwafaka wa kidemografia katika Taifa kwa sababu uwiano wa Wakristo kwa Waislamu ni 87:13; uwiano wa Wabara na Wazanzibari ni 1:0; na uwiano wa wanawake kwa wanaume sio 50:50.
  3. Kwa hiyo, Baraza la Mawazi lililotangazwa na Rais Magufuli jana haliwezi kuimarisha umoja wa kitaifa.
Hoja hii inabutulika kwa sababu madokezo mawili ya kwanza ni kauli zisizo na ukweli wowote. Hebu tuone uwongo wake.

Uwongo katika dokezo la kwanza: Majukumu ya Baraza la Mawaziri yaliyotajwa kwenye Katiba hayasemi kuwa jukumu mojawapo la Baraza la hilo ni kuonyesha mfano wa jinsi ya kubalansi uanwai wa nguvu za kijamii katika Taifa, kama anavyosema mleta hoja.

Hilo ni wazo lake na anapaswa kulijengea hoja ili liingizwe kwenye katiba ya nchi kabla ya kulitumia kama kugezo cha kutathmini maamuzi ya Rais.

Lakini pia, hata kama akilileta lijadiliwe ili liingizwe ktk katiba litapata wakati mgumu kwa sababu ya utata wake.

Kuna njia 101 za kubuni na kufundisha, sio tunu za kiparokia, bali tunu za kitaifa, na hivyo kuimarisha umoja wa kitaifa kwa njia hizo.

Mfano, ni programu za JKT, shule za mabweni na vyuo vinazounganisha makabila tofauti, kufundisha lugha ya taifa mashuleni na vyuoni, kuwa na mtaala mmoja wa elimu katika Taifa, kuwa na mitaala ya uraia inayofundisha tunu za kitaifa mashuleni, michezo ya kitaifa, matukio ya sanaa za kitaifa, kupanua vyombo vya upashanaji habari hadi vijijini, kufundisha masomo ya falsafa yenye kusisitiza sifa mtambuka za kibinadamu (universally accepted philosophical anthropology attributes as opposed to particularised attributes) juu ya ubinadamu, kutandawazisha maisha ya jamii za jirani kwa kulifanya taifa kuwa kijiji kimoja kupitia tehama, kuwa na serikali isiyofungamana na dini waka dhehebu lolote, n.k

Hivyo, itambidi mleta bandiko atwambie kwa nini anafikiri kutengeneza mseto wa kidemografia kwenye Baraza la Mawaziri ni jambo muhimu kuliko hizi njia mbadala.

Kwa hiyo, dokezo la kwanza limeletwa hapa kabla ya juhudi za utafiti kufanyika.

Uwongo katika dokezo la pili: Dhana ya uwiano wa kidemografia katika nchi inamaanisha kwamba, Baraza ligawanywe katika sekta kadhaa kwa kutumia vigezo tofauti vya kidemografia. Vigezo hivyo vya kidemografia ni pamoja na jinsi, dini, umri, jiografia, kabila, mbari, hali ya ulemavu, nk. Kuna matatizo mawili hapa.

Mosi, hizi sifa za kidemografia ni vibadilika (variables) vinavyoweza kubeba thamani kati ya mbili na 123 wakati wizara ni 23 pekee.

Kweli, kibadilika cha jinsi kinaweza kuwa ME au KE, na hapo hakuna shida kubwa, kwani, inangia akilini kuanzisha mjadala wa uwiano wa nusu kwa nusu.

Lakini, vibadilika baki vyote vinabeba thamani zaidi ya mbili, kama ifuatavyo: dini (ukatoliki, ulutheri, usabato, usuni, ushia, ubahai, uhindu, ubuda, ATR, n.k); umri (watoto, vijana, wazee, vikongwe,n.k.); hali ya ndoa (wenye ndoa, wajane, wagane, makapera); jiografia (mikoa 25, kanda 10, wilaya 200, mashariki, magharibi, kaskazini, kusini, bara, visiwani, n.k); kabila (yapo 122); mbari (wabantu, waarabu, wahindi, wanilo, n.k); itikadi (ujamaa, ubepari, ukomunisti, ufashisti, utemi, n.k.); n.k. Mpaka hapo uwiano wa kidemografia unaoongelewa ni wazo ambalo ni too vague.

Tatizo la pili ni kwamba, uwaziri ni ofisi yenye majukumu maalum yaliyotajwa kwenye hati ya majukumu. Hakuna hati ya majukumu ya Waziri inayotaka sifa za kidemografia kama kigezo ya uteuzi.

Kwa hiyo, dokezo la pili ni longo longo za vijiweni tu. Halina umuhimu wala uharaka wowote.

Hivyo basi, kwa sababu madokezo mawili ya kwanza yamebutuliwa, inafuata kimantiki kwamba hitimisho pia halikubaliki.

Kwa maoni yangu, vigezo muhimu katika uteuzi wa Mawaziri sio sifa za kidegorafia, bali uraia, weledi, elimu, uzoefu na utayari wa kufanya kazi. Mengine yote ni ziada tu kulingana na busara za mteuaji!

Naona kuea, inawezekana kabisa tukawa na Mawaziri 23 wanatoka mkoa mmoja, dini moja, kabila moja, mbari moja, jinsi moja, na bado Baraza la Mawaziri likatekeleza majukumu yake kwa kasi na ufanisi.

Nashauri tuelekeze nguvu zetu katika haya:


  1. Jinsi Ilani itakavyotafsiriwa katika mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25
  2. JInsi mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25, utakavyotafsiriwa kwenye mipango mikakati ya kisekta (wizara),
  3. Jinsi, mpango mkakati wa Taifa wawa miaka mitano, 2020/25, utakavyounganishwa na mipango mikakati ya LGAs.
  4. Vigezo vya kuwapata watekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25, pamoja na mipango mikakati ya LGAs.
  5. Ukusanyaji wa rasilimali kwa ajili ya kutekeleza mipango hii.

Mama Amon,
Karibuni Sumbawanga!
 
Rais anateua baraza la Mawaziri kwa kushauriana na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Hao wote ni Waislamu kwani wao hawakuliona hilo?

Ishu ya wanaweke wacha wakae nyumbani watulee.

Wazanzibar na wenyewe wana nchi yao. Anyway Mbarawa ameniumiza moyo kukosekana kwenye baraza la mawaziri.

Anyway today is Sunday take your Bible and go to your nearest church.
 
Wanawake si Katibu wake wa CCM na SUPIKA wamedai watapewa nafasi. Sasa kawageuka
 
Rais anateua baraza la Mawaziri kwa kushauriana na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu..hao wote ni waislamu kwani wao hawakuliona hilo?
Ishu ya wanaweke wacha wakae nyumbani watulee
Wazanzibar na wenyewe wana nchi yao..Anyway Mbarawa ameniumiza moyo kukosekana kwenye baraza la mawaziri..
Anyway today is Sunday take your Bible and go to your nearest church...
Alipomteua Kabudi na Mpango alishauriana na waziri mkuu yupi wakati hao watatu wote walikula kiapo siku moja?
 
Kwa hiyo hicho kikao cha Baraza la Mawaziri kitakuwa kama misa ya jumuiya, kigango au Parokia?

Mzee alishasema hapendi kuchanganyiwa watu, anataka cream ya watu wenye background zinazofanana, kama kisiasa, kiimani, kijinsia, kikabila na kikanda.

Mitano tena.
 
Mkuu umetoa boko leo, lol
Huwa mnaungana pamoja na kuteteana kwenye maslahi ya watu wa dini yenu.

Nahisi ningeishia kutaja wanawake na wazanzibar peke yake mgeunga mkono hoja, ila kitendo cha kutaja kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa notable inclusiveness ya waislamu kwenye baraza mmeona hii mada haijakaa sawa hahaha

Kemeeni teuzi za udini, nchi hii ni yetu sote

Lakini tutaendelea kulisema hili maana halijakaa sawa
 
Katika utendaji hakuna udini , Ujinsia na Uzanzibar au Ubara
 
Sijawahi kuona serikali jeuri, insensitive isiyojali hisia za wananchi kama hii serikali ya awamu ya tano...
Moja: Balaza la Mawazili ni pamoja na manaibu, je manaibu wale hujawaona?!?

Mbili: Balaza la Mawazili ni pamoja na Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Raisi wa Zanzibar, hawa nao ni makafiri?!? ewe uliyedini ya 'kweli'

Tatu: Nafasi za uongozi si zawadi, kwa dini, makabila, mikoa; hadi liwe ni swala la kufa na kupona, kwamba ni lazima dini, kabila, mkoa upate
 
Back
Top Bottom