jambo hili la kukosekana kwa "Uwiano" ktk nafasi za uteuzi halina afya kwa umoja na mshikamano wa nchi yetu.
tunaweza kujifanya hatuoni na tukapuuzia lkn ukweli ni kwamba kuna manung'uniko ambayo tukiyapuuza ynaweza yakaleta athari.
hili ni taifa la watanzania wote hivyo hukuna budi kila mmoja ashiriki kulijenga taifa, sio baadhi ya watu ndio wawe na umuhimu wa kulijenga kuliko wengine.
ni muhimu sana uteuzi/teuzi zozote zile ktk kila nafasi kuzingatia uwiano bila upendeleo lkn kwa kuzingatia weledi, uadilifu n.k
Uwiano ktk nafasi mbali mbali unajenga umoja wa Taifa na pia huchochea uzalendo kwani kila pande zinajihisi kuhusika ktk ujenzi wa taifa lao.