Natumaini mheshimiwa Raisi alikuwa na sababu na muda wa kutosha kutafakari na kuamua nani na nani awatumie katika kuleta maisha bora kwa kila mtanzania na nani amuondoe katika baraza.
Siamini na sipendi sana msemo unaozidi kuwa maarufu kuwa ILIKUWA NI KAZI NGUMU SANA KUAMUA NANI AWE KWENYE BARAZA! Msemo huu kwangu una implication mbaya...! Raisi hatakiwi kuchagua baraza la mawaziri ili kumfurahisha mtu au kumzawadia mtu. Huwezi kumwacha mtu mbovu kwa kuogopa lawama eti kwa sababu kuna fisadi mmoja atakosa "ulaji". Mbona CVs za watu zinajuliakana, achievements zao zinaeleweka, na ufisadi wao haujajificha? Rais anajua ni mikakati gani ipo kuleta hali nzuri kwa wananchi na anajua ni mawaziri wenye sifa gani anawahitaji kutekeleza hiyo mikakati. Kwa nini kazi ya kuchagua baraza ni ngumu? Au CCM imejaa vilaza!!??? (I am sorry)
Baraza la mawaziri ni chombo muhimu sana kwa Rais mwenyewe, serikali, na taifa kwa ujumla. Hili ni kama mkusanyiko wa mikono, miguu, akili, na zana zote ambazo Rais anaweza kuzitumia kutatua matatizo na kufikia matarajio ya wapiga kura wake. Nionavyo mimi ni kuwa hii ni 2nd chance kwa JK baada ya kufeli kwenye 1st chance. Natumaini alitumia uwezo wake wote kuchagua Baraza la mwanzo lakini "say bahati mbaya" uchaguzi wake ulikuwa ZERO. Matarajio yetu ni kuwa Baraza jipya ni moja ya mkakati wake wa kujirekebisha na kurudi kwenye muelekeo uliokuwa umepotezwa. Kuna uwezekano mkubwa Mheshimiwa Rais ametumia busara zake zote na akili zake zote na za akiba kuchagua na kupanga Baraza jipya. Sisi wananchi tunalipokea baraza jipya kwa MATUMAINI; inawezekana tusiwe na imani sawa na ya kutosha kwa baraza jipya lakini tuna imani na uchaguzi na upangaji wa JK. Lakini wakati huohuo mheshimiwa raisi lazima ajue assessment inayofanywa na wananchi juu ya utendaji wa baraza la mawaziri at the same time ni assessment ya utendaji wa Rais. Baraza lililopita liliboronga; wananchi tunajua lile baraza halikushuka kutoka mbinguni... alilichagua Rais mwenyewe!
Ni ngumu sana kujua kama mabadiliko haya katika baraza Mheshimiwa rais ameyafurahia au amelazimika tu kwa sababu ya kelele za wananchi na JF katika kumkoma nyani giladi! Kwa mtazamo wangu ni kuwa mabadiliko ya Waziri mkuu na baadhi ya mawaziri kumetokea very late ukizingatia muda ambao wananchi wamepiga kelele. Ni ngumu sana kujua sababu za kuchelewa kuchukua hatua kwa kiasi hicho lakini ni matumaini yetu wananchi kuwa Mheshimiwa Rais this time atakuwa SEREOUS KWA NIABA YETU kwa kuchukua hatua haraka pale inapojulikana kuna tatizo katika mawaziri wake.
Siku zote inahitaji moyo na ujasiri katika kuleta mabadiliko na mageuzi katika nchi. Woga, aibu, ushikaji, na mazagazaga mengine ni maadui wakubwa sana katika kujenga jamii iliyo bora na iliyostaarabika.
Sisi kama wananchi tungependa kuona KAZI inafanyika na Taifa linasonga mbele katika maendeleo kiuchumi n.k. Majina ya watu hayatuvutiii wala hayana faida yoyote kwetu. Sina sababu ya kumpongeza wala kumlaumu Jk kwa baraza jipya. Ni uwezo na matunda ya kazi zao ndio tunayoangalia. Ni TIME tu ndio itasema whether I should CONGRATULATE the new cabinet au KOMANYANI-GLADI kama kawa. Najua kuna watanzania wengi sana wanaishi katika dhiki kubwa ndani ya nchi yetu yenye utajiri mwingi. Najua kuna wilaya na vijiji ambavyo watu wanaishi kama ni wakimbizi au watu wasio na kwao. Hii inauma na inakera sana. Hii sio karne ya kuwa na mawaziri wanaoishia kufanya ziara kwa wananchi masikini kila siku kwa kutumia magari ya kifahari utadhani wanaenda kutembelea wadudu mbugani bila kufanya chochote kubadili hali ya maisha ya hawa ndugu zetu.
Tunataka mawaziri wenye vitendo na sio midomo iliyojaa kelele na hekaya za kale. Tunataka viongozi wenye VISON na wanaofanya kazi kwa malengo. Tunataka viongozi wennye busara, akili, na uchungu wa nchi na wananchi waliowapa hizo dhamana za uongozi. Lazima wawe ni viongozi wanaojua wanatutoa wapi wanatupeleka wapi. Tumechoka kuendelea kuwa watumwa na mzigo kwa mataifa mengine duniani.
Mungu ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania