Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Rhz4567

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2018
Posts
4,893
Reaction score
6,599
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWA RASMI CHADEMA

Baraza Kuu la #CHADEMA limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 wakipinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa Viti Maalumu bila baraka za chama
======
UPDATE:

199EB08E-50AF-48D1-9554-D3959A4CE965.jpeg

Halima Mdee: Kilichofanyika ni Uhuni, hata Mbowe (Freeman) mwenyewe anajua

John Mrema: Baada ya uamuzi wa Baraza Kuu, Katibu Mkuu ataandika barua kumuarifu Spika kuwa suala lao limehitimishwa; tutamwachia spika afanye uamuzi kama alivyosema anasubiri Rufaa zao
=======

Matokeo ni kama ifuatavyo;

Kanda ya Victoria (Wajumbe 44)
-Wanaokubalia wavuliwe uwanachama 42
-Wasiokubali 1
-Wasiofungamana na Upande wowote 1
Jumla kura 44

Kanda ya Nyasa (Wajumbe 57)

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 57
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 57

Kanda ya Unguja (Wajumbe 22)

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 19
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 1
Jumla ya Kura 22

Kanda ya Pemba 15
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 12
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 15

Kanda ya Kusini 32

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 32
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 32

Kanda ya Pwani 47

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 45
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 47

Kanda ya Kati 44

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 44
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 44

Kanda ya Serengeti Wajumbe 41

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 41
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 41

Kanda ya Magharib Wajumbe 37

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 37
Wasiokubali 0
Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 37

Kanda ya Kaskazini Wajumbe 61

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 61
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 61

MATOKEO YA JUMLA

Idadi ya wajumbe 423

Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%

Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%

Wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%


Pia, soma;

1). BAVICHA: Tumesikitishwa sana na walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika. Wataka hatua kali zichukuliwe

2. Uchaguzi 2020 - CHADEMA yaitaka Tume ya Uchaguzi NEC kutoa Ufafanuzi kuhusu Majina ya Wabunge wa Viti Maalum Wanaodaiwa wamepelekwa Bungeni

3). Mnyika: Ni miezi 5 sasa NEC hawajajibu barua yangu kuhusu walikopata majina ya Wabunge 19 na nani amesaini fomu zao

4). Uchaguzi 2020 - Hatimaye Wabunge wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

5. Uchaguzi 2020 - Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

6. Spika Ndugai: Wabunge waliofukuzwa CHADEMA wapo kwenye mikono salama

7. Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni UHUNI!
 
Yani kwa Ile statement ya Mbowe kwamba yeyote atakayesaliti chama hatavumiliwa nilijua kabisa Covid imekula kwao.

Anyway wameshatengeneza hela ya kutosha na Kama wamechukua mikopo dhamana ni mshahara wa ubunge hivyo serikali italipa huo mkopo.

Magufuli na Ndugai walituharibia sana bunge. Anyway wapumzike waende CCM Sasa waone Kama watapewa nafasi kule.
 
Back
Top Bottom