Mkuu
Matola , kwenye uteuzi wa wabunge WA viti maalum, kila chama kina utaratibu wake wa ndani, kwa Chadema ni CC ya Chadema kwanza kwa kila mjumbe kuleta watu wake, ndio maana ulikuta mtu anamleta mwanae wa kike, na mke wa mtoto wake wa kiume hivyo bungeni wako Baba, mtoto na mkwe!. Lisu na Zitto wakaleta dada zao!. Wajumbe wengine wake zao na kwa baadhi ya viongozi wakaleta hadi vidumu vyao!, ambavyo havichangii hoja yoyote mule Bungeni zaidi ya kutoa tuu zile huduma za kibinaadamu!.
Majina hayo huwasilishwa NEC 30 days kabla ya uchaguzi in order of preference.
Baada ya uchaguzi, NEC hufanya calibration ya kura za urais na kukokotoa idadi ya viti maalum kutoka kila chama na kuwaandikia barua vyama vi confirm uteuzi. Chadema responded kwa barua halali, yenye headed paper ya Chadema na signature ya office bearers.
NEC ikafanya uteuzi na kumpa Spika majina. Katibu Mkuu, JJ.Mnyika, huyu ni Nyerere type, hakuleta jina la ndugu yake yoyote, mke au kidumu, akashangaa barua hiyo ya uteuzi imeandikwa na nani na kusainiwa na nani wakati yeye ndiye KM na hakuandika!. Akaliamsha!. Ukweli barua ya uteuzi ipo ni bonafide genuine, ina bonafide genuine headed paper ya Chadema, ina bonafide genuine signature ya office bearers, hivyo hakuna forgery yoyote ndio maana hawakuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike!. Na kikao cha Baraza Kuu, hakikufanya and due diligence yoyote kujiridhisha CC did the right thing zaidi ya kuyabariki maamuzi ya CC ya Chadema.
Chadema ina katiba yake yenye miongozo yote ya nidhamu, kwanini haikufutwa?. Ule ni Ukangaroo!.
Kama ilivyo kwa Zitto as NKM na Halima Mdee as Mwenyekiti wa Bawacha, hawa wanachaguliwa na Baraza Kuu, ndilo mamlaka yake ya nidhamu, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtiimua Zitto na sasa Halima?!. Huu ni Ukangaroo!.
Kiukweli karma imekuwa iki washughulikia Chadema collectively as chama na kuwashughulikia viongozi wake individually!. Why now add an insult to an injury?.
Karma is real!.
P