Baraza la Famasi latoa elimu kwa umma kuhusu Matumizi sahihi ya Dawa mjini Babati

Baraza la Famasi latoa elimu kwa umma kuhusu Matumizi sahihi ya Dawa mjini Babati

Joined
Mar 27, 2025
Posts
33
Reaction score
45
Wananchi wa Wilaya ya Babati, mkoani Manyara tarehe 08 Mei, 2025 wametembelewa na Baraza la Famasi pamoja na Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma, Wizara ya Afya.

Ufahamu kuhusu Baraza la Famasi na elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa ulitolewa kwa wananchi wa maeneo ya Hospitali ya Mji Babati, Soko kuu la Babati pamoja na Wafanyabiashara wadogo wadogo katika Soko la Machinga Complex, Babati.

Wananchi wa maeneo hayo walipata wasaa wa kuuliza maswali na kujibiwa papo hapo na wataalamu wa dawa kutoka Baraza la Famasi. Wananchi hao wameshukuru kwa kupata elimu hiyo muhimu na wameahidi kuwa mabalozi kwa watanzania wengine.

“Nimeelimika na nitazingatia Matumizi Sahihi ya Dawa”
IMG_2744.jpeg
IMG_2741.jpeg
IMG_2742.jpeg
IMG_2743.jpeg
IMG_2739.jpeg
 
Ni vyuo gani vinavyotoa mafunzo ya utoaji wa dawa(NTA L4)?
 
Ni vyuo gani vinavyotoa mafunzo ya utoaji wa dawa(NTA L4)?
Orodha ya vyuo vilivyosajiliwa inapatikana kwenye tovuti ya NACTVET The National Council for Technical and Vocational Education and Training (NACTVET) | Striving for world-class excellence in Technical and Vocational Education and Training na Baraza La Famasi PC | Home . Ukifungua tovuti ya Baraza, scroll kwa chini utaona Training Institution E register. Bofya hapo na utaona orodha ya vyuo vilivyosajiliwa.

Ahsante
TM
 
Back
Top Bottom