Wasomi wa kiswahili wanazingua sana na ni nyanja zote takribani... Kuna Kiswahili kama hivyo halafu kuna watu wa dini na hapa nitaongelea dini yangu (waislamu)
Yaani ukitaka kugoogle jambo la kiislamu basi ili ufanikiwe ni lazima ngeli iwe inapanda au uwe na "ujanja" wa kugoogle translate ili usachi kingereza ndipo utapata maudhui ya kitu unachohitaji! Vinginevyo huambulii kitu au utapata bora elimu na si elimu bora!
Angalia kwa namna ya hali halisi ya sasa watu wana uhitajio mkubwa sana wa tafsiri na ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya kijamii na wanahamasika sana kufuatilia dini lakini ajabu ni kwamba vitabu vingi vya kutegemewa vya fiqih vipo katika lugha za kiarabu na kiingereza pekee
Sasa huwa nabaki kujiuliza tu hivi kweli fiqih za maswala mbalimbali ya kijamii kweli nikihitaji kujifunza mpaka nikakunje goti nijifunze kwanza kiarabu?
Wasomi wa Tanzania hebu badilikeni bwana! Mnavyosomea fani zenu hizo kubwakubwa ni ili mtukomboe jamii kwenye ujinga tulionao na si vinginevyo! Google inakosa vitu vingi sana vya maudhui ya Kiswahili matokeo yake ndio mtu unasachi kitu fulani cha kielimu hasa unapelekwa moja kwa moja Jamii forums ukapate ufafanuzi wa watu ambao wengine hata ID zao tu zinaonesha kwamba utapotezwa
Halafu nilichogundua kuna JamiiForums kwa maudhui ya Kiswahili kisha kuna Quora kwa maudhui ya kiingereza yaani humo kuna karibu kila nyanja imegusiwa japo changamoto ni kwamba unakuta kila mtu kaandika kwa anavyojua yeye kwahiyo usipokuwa makini unaweza kuingizwa chaka!