Uchaguzi 2020 Baraza la Maaskofu Katoliki wamesisitiza amani na uadilifu vizingatiwe kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho

Uchaguzi 2020 Baraza la Maaskofu Katoliki wamesisitiza amani na uadilifu vizingatiwe kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limewataka Watanzania waiheshimu na kuisikiliza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa ndiyo mratibu wa kisheria wa uchaguzi wa Tanzania.

Aidha, maaskofu hao wamesisitiza amani na uadilifu vizingatiwe kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani TEC, Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa'Ichi na Katibu Mkuu wa TEC, Padri Charles Kitima walitoa wito huo jana kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam.

Waliwataka Watanzania waongozwe na dhamiri nyoofu kwa kufanya uamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa badala ya maslahi binafsi.

Walisisitiza Watanzania kupitia imani zao wauombee Uchaguzi Mkuu uwe wa amani na salama na uzae matunda tarajiwa kwa nchi kupata viongozi bora.

Askofu Mkuu Ruwa'Ichi aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kesho na kupiga kura kwa uelewa mpana, ukomavu na uzalendo na kuzingatia amani na maendeleo ya jamii.

Kiongozi huyo ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam alivihimiza vyombo vyote vinavyohusika kuratibu na kusimamia Uchaguzi Mkuu vizingatie sheria, taratibu na maadili ya kazi ili wapigakura wawe na imani na uchaguzi huo.

"Tuwe makini kufuata sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na mamlaka husika katika kipindi hiki cha uchaguzi hususan Tume ya Taifa ya Uchaguzi."

"Uchaguzi ni zoezi la kiraia linalohusisha haki za kirai hivyo Watanzania wote waheshimu zoezi hilo na kushiriki kwa unyofu mkubwa wa moyo, nidhamu, ukomavu, uzalendo na uwajibikaji wa hali ya juu," alisema Askofu Mkuu Ruwa'Ichi.

Padri Kitima alisema wapiga kura wanapaswa kuongozwa na dhamiri nyoofu wakati wa kupiga kura kwa manufaa mapana ya Watanzania na taifa kwa jumla.

Akiwa na Padri Chesco Msaga, Padri Kitima alisema miongoni mwa mambo muhimu yanayoweza kulivusha salama taifa katika Uchaguzi Mkuu ni vyama vyote kuwa na haki sawa.

Aidha, aliwataka wadau wa uchaguzi waheshimu matokeo yatakayotangazwa.

"Tume ndiyo refa mkuu baada mchezo anayeshinda kubali hivyo, tunaomba mratibu mkuu wa kazi hii ya uchaguzi ambaye ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi aheshimiwe na kusikilizwa, sisi tuna imani na tume hii hivyo wadau wake wote wazingatie uadilifu wa kisheria na kiutu kwa kuwa Mungu anataka watu wote waheshimu dhamira za watu ili tupate matokeo mazuri," alisema Padri Kitima.
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku).

Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
TEC wamekuwa genge la wahuni na wachumia matumbo.
Kanisa katoliki Tanzania ni hovyo kabisa tofauti na nchi nyingine ambapo ndio hutoa mwaka na tumaini la haki na usawa na ukweli bila kuangalia cheo cha mtu.
Pumbafu kabisa, hivi hawaoni hujuma na dhuluma inayofanywa na tume ya uchaguzi?
 
Ukiona kiongozi wa dini anafunga ndoa na utawala batili Utawala dhalimu upaswi kuumiza kichwa kumjua anaemtumikia
 
Kwa hiyo huyo refa mkuu hamna cha kumwambia hata kidogo? Kumkumbusha kiapo na kutenda haki, kuanzia kupiga kura, kuhesabu na kutangaza hamna onyo lolote la kumwambia? Kwamba ni wapiga kura tu ndio wa kuonywa kweli?
 
Wanaogopa kutekwa Hawa na kubambikizwa kesi za uraia tuwapuuze tu

@pigakuralindakura
 
Labda CCM itakapotoka madarakani ndio uadilifu utakuwepo, leo Gwajima na uasikofu wake kamugeuza Mungu wake kuwa koti kamtundika kwenye msumari atamkumbuka baada ya uchaguzi.
 
Sisi watanzania tunafuata maelekezo ya viongozi wetu wa dini wanaopenda amani ya nchi yetu nzuri ya Tanzania.
 
Sijui hii nchi ina mashetani gani, kila mtu ni mchumia tumbo.
Hata ambaye ungedhani habanwi kwa njia yoyote kupata UBWABWA wake. Viongozi wa Dini TZ wanaogopa nini kusimamia haki?
 
Hao maaskofu ni PhD tupu lakini kichwani wana funza badala ya akili.Amani itatoka wapi kama hakuna haki?Yaani usiku unapita nyumba kwa nyumba kupiga risasi watu waliolala kama huko Zanzibar halafu unahubiri amani?!
 
Viongozi wangu wa TEC mnaniangusha Sana, Haki Kama haipo hayo yote mliyoshauri ni kazi bure!

Haki Haki Haki Haki!!
#Justicematter
 
Hii dini nayo inafundisha uzezeta sana. Badala msisitizo uwe kwenye 'HAKI' wao walima mulemule kwenye shamba la 'mbogamboga'! Swine. Ona wanavyo sema :

”Aidha, maaskofu hao wamesisitiza amani na uadilifu vizingatiwe kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho"

Besides, I respect Rev. Niwemugizi.
 
Back
Top Bottom