SI KWELI Baraza la Maaskofu limetoa wito wa amani kuelekea uchaguzi mkuu

SI KWELI Baraza la Maaskofu limetoa wito wa amani kuelekea uchaguzi mkuu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
TEC01.jpg
TEC02.jpg
TEC03.jpg
TEC..GX.jpg
TEC.GX.jpg
TECGX.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kuwa waraka wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania ukiwa na kichwa cha habari kinachosomeka "Tamko la baraza la maaskofu katoliki tanzania (TEC) kuhusu amani kwa taifa kuelekea siku ya uchaguzi mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 oктова 2025." Rejea hapa na hapa.


Je, ni upi uhalisia kuhusu waraka huo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha waraka unaodaiwa kutolewa na baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ni wa kughushi kwani haujatolewa na baraza hilo.

Aidha waraka huo umebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo matumizi ya fonti isiyotumiwa na baraza hilo, makosa ya kiuandishi, jambo linalodhihirisha kuwa ni wa kutengenezwa na wapotoshaji.

Katibu wa baraza la maskofu katoliki Tanzania Padri Charles Kitima Akizungumza na waandishi wa Leo Oktoba 13,2025 amesema waraka huo si wa baraza hilo huku akisisiza kuwa wanaofanya hivyo wakome mara moja.

Aidha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram baraza hilo limetoa taarifa kwa umma inayokanusha waraka huo wa kughushi.

"Tunapenda kuwatangazia Waamini na Watanzania wote kwa ujumla, kuwa waraka huo haukutolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Baraza halihusiki na hayo maudhui yaliyomo kwenye andiko hilo.​

Tabia hii mbaya yakutumia Taasisi ya Maaskofu kupitishia jumbe zisizotokana na Baraza ikomeshwe. Tunawataka wenye tabia hiyo waache tabia hiyo."

Kumbuka TEC huchapisha taarifa zake rasmi katika ukurasa wake rasmi kwenye mtandao wa Instagram, hivyo unapokutana na taarifa inayokupa mashaka kuhusu baraza hilo jiridhishe kupitia ukurasa huo au iwasilishe taarifa hiyo katika jukwaa la JamiiCheck.com kupata uhalisia.​
Waroma 8:2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru mimi RAZIEL-13 mbali na sheria ya dhambi na mauti.

RAZIEL-13 IN 13th October 2025; Monday My Thirteen-13.
 
Ninawapongeza sana TEC kwa kuamua kutiki tarehe 29 October. Ila TEC nao wajiandae kwa mvua ya matusi toka kwa wafuasi wa CHADEMA wanaoongozwa na Mange KImambi kwa wakati huu.
 
Ninawapongeza sana TEC kwa kuamua kutiki tarehe 29 October. Ila TEC nao wajiandae kwa mvua ya matusi toka kwa wafuasi wa CHADEMA wanaoongozwa na Mange KImambi kwa wakati huu.
Hiyo ni barua feki mbona
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
Wazi afande
 
Moderators tuondolee taarifa hii ya baraza la maaskofu kwani inazua taharuki wakati ukweli umejulikana. Tunaomba taarifa ya jamiicheck iwe pale kwenye carousel ili ionekane kwa uharaka.
 
Back
Top Bottom