SI KWELI Baraza la Maaskofu limetoa wito wa amani kuelekea uchaguzi mkuu

SI KWELI Baraza la Maaskofu limetoa wito wa amani kuelekea uchaguzi mkuu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
TEC01.jpg
TEC02.jpg
TEC03.jpg
TEC..GX.jpg
TEC.GX.jpg
TECGX.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kuwa waraka wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania ukiwa na kichwa cha habari kinachosomeka "Tamko la baraza la maaskofu katoliki tanzania (TEC) kuhusu amani kwa taifa kuelekea siku ya uchaguzi mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 oктова 2025." Rejea hapa na hapa.

Je, ni upi uhalisia kuhusu waraka huo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha waraka unaodaiwa kutolewa na baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ni wa kughushi kwani haujatolewa na baraza hilo.

Aidha waraka huo umebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo matumizi ya fonti isiyotumiwa na baraza hilo, makosa ya kiuandishi, jambo linalodhihirisha kuwa ni wa kutengenezwa na wapotoshaji.

Katibu wa baraza la maskofu katoliki Tanzania Padri Charles Kitima Akizungumza na waandishi wa Leo Oktoba 13,2025 amesema waraka huo si wa baraza hilo huku akisisiza kuwa wanaofanya hivyo wakome mara moja.

Aidha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram baraza hilo limetoa taarifa kwa umma inayokanusha waraka huo wa kughushi.

"Tunapenda kuwatangazia Waamini na Watanzania wote kwa ujumla, kuwa waraka huo haukutolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Baraza halihusiki na hayo maudhui yaliyomo kwenye andiko hilo.​

Tabia hii mbaya yakutumia Taasisi ya Maaskofu kupitishia jumbe zisizotokana na Baraza ikomeshwe. Tunawataka wenye tabia hiyo waache tabia hiyo."

Kumbuka TEC huchapisha taarifa zake rasmi katika ukurasa wake rasmi kwenye mtandao wa Instagram, hivyo unapokutana na taarifa inayokupa mashaka kuhusu baraza hilo jiridhishe kupitia ukurasa huo au iwasilishe taarifa hiyo katika jukwaa la JamiiCheck.com kupata uhalisia.​
Wahuni hawajui kuandika wala kusoma.
KATORIKI ndiyo nini?
Hilo tatizo la kuokota vilaza na kuwapa kazi ya upotoshaji (disinformation).
Hatari kubwa ni kwamba hawa siyo wahuni wa kawaida. Hawa ni watu waovu, wauaji.

Hii haikutungwa tu na "wahuni" kama akina LukasMshamba. Hawa ni watu maalum walioshikilia nyadhifa za heshima serikalini; ndani ya chama au hata ndani ya dini nyingine inayopishana maoni na hawa wenzao.. HII NI VITA.

Hii siyo mara ya kwanza kutoa nyaraka yenye upotoshaji kwa madai kuwa imetolewa na kanisa wakati wa mkasa wa padre Kitima..
Hawa ni watu waovu
 
Inajulikana wengi wao hawa wahuni ni wavaa kobazi waliovuka maji.
Tunakwepa kuwataja kobazi kwa makusudi ili wasijitenge kwenye harakati za kupigania uhuru kwa mara ya pili.
 
Inajulikana wengi wao hawa wahuni ni wavaa kobazi waliovuka maji.
Tunakwepa kuwataja kobazi kwa makusudi ili wasijitenge kwenye harakati za kupigania uhuru kwa mara ya pili.
Hawa hawapiganii uhuru; kwa mara ya pili; hawa hata uwape nchi nzima watawale wenyewe, matatizo yatakuwa ni yale yale kama ya Sudan au Somalia.
Hawa siyo watu wa kuogopa kuwataja moja kwa moja; hawa ni watu wa kuanikwa wazi wazi kuwa ndio maadui wakubwa wa usalama wa waTanzania wote.
 
Back
Top Bottom