PostGE2025 Baraza la maaskofu Tanzania (TEC) mnatukosea sana wakatoliki

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
𝗕𝗔π—₯𝗔𝗭𝗔 π—Ÿπ—” π— π—”π—”π—¦π—žπ—’π—™π—¨ (π—§π—˜π—–) π— π—‘π—”π—§π—¨π—žπ—’π—¦π—˜π—” 𝗦𝗔𝗑𝗔 π—ͺπ—”π—žπ—”π—§π—’π—Ÿπ—œπ—žπ—œ.

Tumsifu Yesu Kristo.

Jina langu ni Joseph Simon Mapunda, Muumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga Mkoani Ruvuma ambaye kwa mapenzi ya Mungu mwaka jana 2024 nilikuja Dar es Salaam kikazi na naishi Tegeta.

Leo tarehe 15 Novemba, 2025 nimesoma andiko la Baraza la Maaskofu lililoitwa β€œTafakari ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Juu ya Yaliyotokea Siku na Baada ya Uchaguzi-2025”

Awali ya yote kabisa naomba kuchukua nafasi hii kutoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza ndugu zao katika vurugu zilizotokea tarehe 25 Oktoba, 2025 na siku zilizofuata wakati ambapo nchi yetu Tanzania ilijikuta katika matukio ambayo hayajawahi kutokea na hayafanani kabisa na utamaduni wa Watanzania. Matukio mageni haswa.

Naungana na Watanzania wote kuwaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka.

Napenda pia kuwapa pole wote waliopoteza mali zao, walipoteza biashara zao, walipoteza ajira zao na ambao wanapitia kipindi kigumu cha giza nene kutokana na kupoteza kipato ambacho kiliendesha maisha yao na familia zao ama wapendwa wao.

Kwa wale ambao wamehusika na uhuni huu ama kwa kuchochea ama kwa kutekeleza matukio ya uharibifu wa miundombinu ya umma, wizi wa mali za watu binafsi na umma, uchomaji moto wa majengo, magari na biashara za watu mbalimbali, Mwenyezi Mungu mwenye kutoa haki awape wanachostahili.

Naomba nirudi kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), bila kupepesa macho naomba kusema wazi nasikitishwa sana na mwenendo wa TEC kutoa matamko na maandiko ambayo badala ya kuponya Taifa yanachochea mgawanyiko, uhasama na kuligombanisha Kanisa na Serikali. Ni kweli Maaskofu ndio viongozi wakuu wa majimbo ya Kanisa Katoliki lakini ni muhimu Mababa Askofu mkaheshimu demokrasia na haki ya waumini wa Kanisa Katoliki kwa kutofanya mambo ambayo yanatokana na matakwa yenu, hayana baraka za waumini na yanawaharibia waumini wa Kanisa hili lenye heshima kubwa hapa Tanzania na ambalo limejengwa kwa jasho jingi la Watanzania vizazi na vizazi.

Nimeona mara kadhaa mnavyotoa matamko yenye vinasaba vya Kisiasa ambayo hakuna asiyejua kuwa yana mwelekeo wa siasa za upinzani na yanalenga kuishambulia Serikali. Sina tatizo na hoja mnazojenga lakini muhimu hapa kwa nini mnatumia Kanisa kufanya minyukano ya Kisiasa? Sisi Wakatoliki tumejenga Kanisa hili ili litupe huduma za kiroho, lihubiri Injili, lituweke pamoja na lidumishe amani na upendo kwa mwanadamu. Mnayoyafanya mnakiuka misingi hii.

Matukio yaliyotokea tarehe 29 Oktoba, 2025 na siku kadhaa za mbele hakuna yaliyemfurahisha, kwa nini nyie TEC mnaibuka na andiko la namna hii tena siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutoa hotuba ya kuwaunganisha Watanzania, ya kuhimiza amani na utulivu, ya kujibu hoja za vijana na ya kuendeleza mkono wa maridhiano? Kwa nini Kanisa langu mnafanya mambo haya?

Tuseme Waumini wa Kanisa Katoliki na wanaopendezwa na mambo yanayoendelea nchini watawashangilia na kwa kuwa kuna kampeni ya mitandaoni ya kuitisha maandamano tarehe 9 Desemba, 2025 ili wajitokeze tena kupambana na vyombo vya dola kama ilivyokuwa tarehe 29 Oktoba, 2025, mnataka watu wengine wauawe? hata wale ambao hawahusiki na uchochezi huu? Mnataka watu wengine waingie kwenye umasikini kwa biashara zao kuvamiwa, kuibiwa, kuharibiwa na kuchomewa moto? Au tuseme mnataka nchi iingie katika mapinduzi? Hamzijui gharama za mapinduzi?

Nimesoma andiko lenu mstari kwa mstari. Nataka niwaulize hoja chache kabisa na nyie mtafakari huku mkiongozwa na Roho Mtakatifu na roho wa haki;

1. Hivi Mababa Askofu kwenye andiko lenu mnasema tarehe 29 Oktoba, 2025 waandamaji walishambuliwa na kuuawa. Naomba kuuliza wale walikuwa waandamanaji au waleta vurugu, wezi na waharibifu wa mali za umma? Nyie mmetembea nchini nyingi Duniani, watu wanaoandamana huwa wanafanya vitendo ambavyo vilifanyika siku ile? Waandamaji wanakwenda kuwatia umasikini binadamu wenzao na kutishia maisha yao au wanakwenda kudai haki zao kwa watawala? Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mnaowaita waandamanaji walikuwa na silaha za moto na wameua askari polisi ambao walikuwa wanakabiliana nao walipokuwa wanakwenda kuvamia mali za watu kuvunja na kuiba? Mnafahamu hao watu wameua watu wasio na hatia wakijiita ni Askari?

2. ⁠Mababa Askofu mnajua kuwa hao mnaowaita waandamanaji walivamia vituo vya polisi ili kuchukua silaha na walipozikosa walivichoma moto vituo vya polisi vingi? mababa Askofu ina maana hamjuia madhara ya makundi ya wahuni kuchukua silaha na kuvamia watu na biashara zao? Mlitaka Askari wafanyeje? Nyie wenyewe nyumba zenu mmeweka Askari wenye silaha, leo watu waje kuvamia nyumba ya Askofu wachome moto na kisha waanze kutaka kuingia ndani hao Askari wenu watawaacha?

3. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mnaowaita Waandamanaji walikwenda kuchoma moto jengo la Mawasiliano ambalo sio tu lingesababisha kuzimwa kwa mawasiliano yote bali nchi ingekosa mawasiliano kwa asilimia 100 kwa muda usiojulikana. Mnajua kuwa watu hao walishachoma eneo la mapokezi na jengo hilo liliokolewa na Askari Zimamoto waliowahi kabla ya moto kusambaa. Mnajua madhara ambayo yangetokea kwa nchi kukosa mawasiliano kabisa? Madhara kwa huduma za kifedha, mapato ya Serikali, huduma za matibabu hospitali, elimu na biashara zao watu.

4. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mliowaita waandamanaji wamechoma moto vituo vya mafuta. Hamjui madhara ya kituo cha mafuta kikiungua hadi kufika hatua ya kulipuka?

5. ⁠Mababa Askofu mnahamu kuwa uharibifu wa miundombinu ya mwendokasi umesababisha huduma hiyo kusitishwa? Mnajua madhara yake? Kwa sababu nyie hamsafirii usafiri wa umma, mnatumia magari binafsi ambayo sisi waumini tumewanunulia.

6. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa vijana waliokuwa wanapambana kutafuta kipato wamefirisika na hivi sasa wanakosa mpaka pesa ya kununua chakula cha watoto wao majumbani kwa sababu hao mnaowaita waandamanaji wamewaibia na kuharibu kabisa biashara zao?

7. ⁠Mababa Askofu mnafahamu madhara mengine mengi ambayo kama Nchi tunayapitia kutokana na vurugu zile?

Mababa Askofu hamuoni kuwa sio sawa kwa chombo hiki cha Dini, cha Kanisa Katoliki kubeba ajenda za chama cha upinzani ambacho kimeamua kutoshiriki uchaguzi ambao ni takwa la kikatiba ili kihamasishe watu kuleta vurugu ndani ya nchi? Kwani mkitoa tamko la kujenga imani za watu, watu kumrudia Mungu, kutubu na kujisahihisha pamoja kuhamasisha amani, upendo na utulivu mtapungukiwa nini?

Sawa, sasa mnatwambiaje Wakatoliki tujiandae kwa majambia, visu shoka, mawe na manati ili tukapambane na Polisi wenye silaha na JWTZ tarehe 9 Desemba, 2025 ili mje muandike tafakari nyingine ya TEC au mtatuletea bunduki, mabomu na mizinga ya kukabiliana na dola inayosimamia utawala wa Sheria?

Rais kaunda tume ya kuchunguza chanzo cha vurugu na kutoa mapendekezo ya namna ya kushughulikia mambo yaliyojitokeza tarehe 29 Oktoba, 2025 na nyie mmetoa tamko siku inayofuata, kwa hiyo mnataka sisi Wakatoliki tumsikilize Rais au tuwasikilize nyinyi TEC? Kwa nini mnataka kushindana na Rais? Hii nchi inaongozwa na TEC au inaongozwa na Serikali ambayo imewekwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi?

Kama na nyie TEC mnataka kuwa viongozi wa kisiasa kwa nini msiwe mnagombea nafasi za kisiasa kama wanavyofanya viongozi wa madhehebu mengine ya Kikristo? Ili nanyi muwe na haki na mamlaka ya kiuwakilishi. Maana hivi mnavyofanya mnapaswa kuulizwa ni wananchi wanawatuma au mnajituma wenyewe?

Hamkuanza tabia hizi leo, mlifanya sana wakati wa tawala zilizopita. Hivi mmewahi kuwaza viongozi wa Serikali ambao ni Wakatoliki tena wengine ni wasaidizi wa karibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnawaweka katika mazingira gani? Hebu vaeni viatu vya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ni Mkatoliki, Wasaidizi katika Ofisi Binafsi ya Rais ambao ni Wakatoliki na wanakuja kusali kwenye Ibada ambazo nyie mnaacha kuhubiri Injili na mnaanza kuhubiri hoja za Vyama vya Siasa, wanajisikiaje hawa?

Naomba kuwauliza TEC, kwa nini hamkusubiri Tume ya Uchunguzi ifanye kazi kisha ilete majibu? Mnajua tume itakuja na majibu gani? Hivi ikija na majibu ya sababu za msingi za namna vyombo vilivyokabiliana na matukio yale, mtabadilisha andiko na tamko lenu?

Mababa Askofu ina maana hamjui kuwa kinachoendelea ni ushawishi mkubwa wa watu wasioitakia mema Tanzania?

Mababa Askofu hamsikii hoja za kwamba mnaipiga vita Serikali hii kwa sababu Rais sio Mkatoliki? Kwamba mmeshaona Kanisa Katoliki ndio pekee lenye haki ya kuweka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Labda niulize Rais Samia amefanya mangapi ambayo huko nyuma Kanisa Katoliki lilinyimwa? Hivi mnadhani Serikali ikikunjua makucha Kanisa litabaki salama? Mmesahau jinsi Hayati Rais Magufuli alivyowashughulikia? Mmesahau jinsi Rais Samia alivyowasaidia? Kwa nini mnafanya mipango ya kumkwamisha huyu Mama Rais Samia. Amekosa nini?

Hayo madai ya wanasiasa ambayo na nyinyi mmefanya ajenda yenu hamjui majibu yake?

Hamjui kama Rais Samia ameahidi katika kipindi cha miaka mitano tutapata Katiba mpya? Hamjasikia ahadi ya maridhiano? Hamjasikia mipango ya mageuzi ya kiuchumi? Hamna ufahamu na falsafa ya R nne na namna ambavyo Rais Samia ameanza kuzitekeleza?

Mababa Askofu hamjui namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita imechukua hatua madhubuti za kujenga uchumi na kukuza kipato cha Watanzania? Hamjui namna ambavyo Rais Samia ameongeza fursa za ukuaji wa demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kisiasa na uhuru wa masuala mengine mengi? Mmesahau jinsi mambo haya yalivyobanwa wakati wa utawala wa Mkatoliki mwenzetu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli?

Naomba kuwasihi, msitukwaze Wakatoliki, msiwagombanishe Watanzania na Serikali yao, msiwe chanzo cha machafuko ya nchi. Nawasihi kwa unyenyekevu, fanyeni jitihada za kuliunganisha Taifa, na kama haiwezekani basi kaeni kimya muache Wadau wengine waunganishe Taifa.

Mwacheni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aongoze Tanzania, acheni Tanzania idumishe amani na waacheni Watanzania waamue wanataka nchi iendaje.

Naiomba Serikali isisite kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi wa Kanisa Katoliki ambao wanatupeleka katika mwelekeo huu. Mimi ni Mkatoliki, najua sio viongozi wote wa Kanisa hili wanafurahishwa na mwenendo huu, najua najua ubabe na utamaduni usio wa kidiplomasia ndani ya Kanisa unaficha sauti za Wakatoliki ambao wanatofautiana na msimamo wa NEC. Acheni kufanya hivyo viongozi wangu, mnatukwaza waumini.

Kaeni mbali na siasa na pambaneni na kueneza Injili na kuunganisha watu wa Mungu. Sambazeni upendo na usuluhishi, tangazeni amani na upendo na muwe na furaha pale nchi inapokuwa na amani.

Tumsifu Yesu Kristo.
Ukiwa hukubaliani na muongozo wa kanisa basi toka kwenye hilo kanisa jiunge na lingine au anzisha lako.

Maana huendani na misingi ya hilo kanisa.
 
takataka....
 
Msome na huyu hapa:-
TUNAWASIKILIZA MAASKOFU KISHA TUNAWAPUUZA

Anaandika Mwl/ Tambulu Dodoma-Tanzania

Nianze kwa maneno ya Rais wa Marekani Jimmy Carter, amewahi kusema kuwa "Kanisa Katoliki linapopata nafasi ya Uongozi wa Kisiasa katika Nchi, nchi hiyo haiwezi kupata maendeleo....." Iwe maendeleo ya kiuchumi, Kisiasa, kielimu nk.

Hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu la Viongozi wa Makanisa (Maaskofu, Mapadri na Wachungaji) kushambulia uongozi wa Rais Samia kwa kigezo cha kutaka utawala wake utende haki kwa watanzania. Nimesikiliza hotuba iliyotolewa na Askofu Mkuu Ruwaichi jana akisema Taifa limegawika, watu wamepoteza wapendwa wao na mengine mengi. Kubwa zaidi Askofu Ruwaichi nae ameendelea kuunyoshea kidole utawala huu wa Rais Samia kwa kusisitiza swala la Haki na kwamba hakuna Amani bila Haki. Nae Askofu Musomba ameonyesha masikitiko yake kwa vifo vilivyo tokea na watu kupoteza wapendwa wao, wimbo ukabaki ule ule wa Haki kisha amani itakuja yenyewe.

Watanzania na dunia inazidi kuona Kasi ya wachungaji na maaskofu nchini kushambulia uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kudai haki za watu zinakandamizwa, na hivyo kuitaka Serikali ya Rais Samia na Rais Samia mwenyewe kulinda haki na uhuru wa watu.

Hilo ni jambo jema sana, hakuna asie jua umuhimu wa haki. Kama Viongozi wa dini wanafanya kazi nzuri kumkumbusha Rais Samia kuongoza nchi kwa misingi ya Haki ili kujenga umoja wa kitaifa na kulinda amani ya nchi yetu.

Tatizo langu mpaka nashawishika kuandika makala hii sio maneno ya Maaskofu wapendwa, bali dhamira na lengo la maneno yao. Kama ni mfatiliaji mzuri wa matukio na matendo ya Viongozi wa Kikristo unaweza kubaki na maswali mengi.

Ni kweli maaskofu wetu wanamaanisha Haki? Au ni aina nyingine ya vita dhidi ya Rais Samia na Serikali yake?

Machungu wanayo onyesha Maaskofu wetu kwa vifo kadhaa vilivyo tokea October, 29 katika Maandamano haramu ni machungu ya kweli au yameficha jambo jingine nyuma yake.

Haki zinazo zungumzwa na Viongozi wa Kanisa leo ni haki zipi? Haki hizo ni haki za nani? Ni haki za watanzania au haki za Wakristo.

Ni vigumu kushawishika na madai ya haki yanayo semwa na Viongozi wa Kikristo nchini hasa kwa kurejea kumbukumbu za namna Taasisi za Kikristo zinavyo kandamiza haki za Watanzania. Tujikumbushe matukio machache ili tuone kama madai ya haki yanayo semwa na Viongozi wa dini ya Kikristo yanaukweli au yanaficha dhamira zao dhidi ya Utawala wa Rais Samia

1. Mwaka 1992, CCT na TEC wameingia mkataba(Memorandum of Understanding) na Serikali ya Tanzania kuchota ma billion ya Shilling ambayo ni Kodi za watanzania kila mwezi kwa ajili ya kujinufaisha wao na Makanisa yao. Tukumbuke kuwa nchi yetu si nchi ya Kidini, kitendo cha Makanisa kutumia Kodi za Watanzania kulipa mishahara wachungaji na Maaskofu kinawanyima Haki watu wa dini nyingine. Kwa nini Maaskofu hawasemi Haki hii wanayodhulumu watu wa dini nyingine kwa kushirikiana na Serikali.

2. Mwaka 1998, Askofu Lwambano wa Parokia ya Mburahati alitoa maagizo ya kuvamiwa na kuawa Waislaam Msikiti wa Mwembechai Manzese Jijini Dar es salaam kwa madai kuwa wanafanya mihadhara inayo umiza hisia za Wakristo. Kwa maelekezo yake Jeshi la Polisi lilivamia Msikiti wa Mwembechai na Waislaam kadhaa wakapigwa risase na kuuawa huku wengine wakibaki vilema hadi leo. Damu za Watanzania hawa zilimwagika bila hatia yoyote huku Maaskofu wakishangilia. Kwa nini leo wanaumia sana kwa watu waliopoteza maisha kwa kufanya Maandamano haramu, kuharibu na kuchoma Mali za watu, kuharibu miundombinu ya umma kama kuchoma moto vituo vya mabasi ya mwendoiasi nk. Watanzania hawa na wale waliouawa Mwembechai kwa agizo la Kanisa wanatofauti gani. Kwa nini hatukusikia matamko ya Haki kwa damu za Waislaam wale waliouawa Mwembechai.

3. Waislaam kama sehemu ya raia wa nchi hii wamekuwa wakipiga kelele na kuomba Serikali ya Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kiislaam (OIC). Kwa kutoa mifano ya nchi wanachama wanavyo nufaika na Jumuiya hiyo ya OIC na kuwaletea maendeleo wananchi wake ikiwemo Benin, Msumbiji, Nigeria, Sierra Leon, Uganda, Urusi, Gabon, Guinea Bissau na hata baadhi ya nchi za Ulaya. Bila kujali kuwa Waislaam wana Haki na nchi yetu itanufaika na miradi mikubwa ya Maendeleo. Viongozi wa Makanisa wamekuwa mstari wa mbele kupinga jambo hilo na kusababisha Waislaam kupoteza haki yao. OIC walikuwa tayari kuanza ujenzi wa Chuo Kikuu hapa Tanzania, baada ya Viongozi wa Makanisa kupinga swala hilo mradi huo mkubwa wa Maendeleo ulijengwa Mbale Nchini Uganda. Maaskofu na Wachungaji wameanza lini kusemea haki za Watanzania. Hata Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya nje wakati huo Mh. Bernard Membe ilipotoa taarifa Bungeni kuwa Tanzania kujiunga na OIC hakuna madhara yoyote na badala yake Serikali yetu itanufaika, Kardinal Policap Pengo alimwita Mh. Membe na kumtaka asitishe mara moja mpango huo. Kwa maslahi yao Walidhulumu haki ya Mamilioni ya Waislaam na Watanzania wengine kujipatia miradi ya maendeleo. Makanisa yakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Serikali kuingiza swala la OIC na mahakama ya Kadhi katika Katiba yetu ni sawa na kuinajisi Katiba. Gazeti la Utatu Juma pili September 28- October 4, 2008.

4. Swala la mauaji na watu kutekwa, tatizo hili halikuanza wakati wa utawala wa Rais Samia. Kama kuna wakati watanzania wametekwa, kupotezwa na kuuawa ni wakati wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli. Wakati wa utawala wa Rais Magufuli ndipo kwa mara ya kwanza miili ya watu ilianza kuokotwa ufukweni mwa Bahati ya Hindi ikiwa kwenye viroba. Mauaji ya MKIRU(Mkuranga, Kibiti, Rufiji) ni wakati wa Rais Magufuli. Hali ilikuwa mbaya sana, Watanzania waliishi kwa hofu kubwa. Hakuna aliejua hatma ya kesho yake. Wanasiasa waliishi kama wako Gerezani, vyombo vya Habari vilifungwa midomo. Hata Bunge lilikuwa siri. Waliojaribu kusema walikula risase bila Idadi, hakuna Mtanzania aliekuwa na Haki. Maaskofu wetu mlikuwa likizo wakati huo. Wengi wenu mlikuwa sio tu Viongozi wa Rais Magufuli bali kipenzi chenu. Hotuba za haki hazikusikika, zaidi mliendelea kumuimbia nyimbo za kumsifu. Kwa nini Leo kwa Rais Samia

5. January 11,2019 Wafanya kazi 11 Waislaam wakiwemo MaProfesa, Madaktari, na watumishi waandamizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma-Tanzania walipewa uhamisho wa ghafla bila kuzingatia Sheria na haki zao kama watumishi. Wakati huo huo Serikali ya Rais Magufuli akapeleka watumishe wengine 11 wote Wakristo. Jambo ambalo lilipigiwa kelele na kukosolewa na watu mbalimbali kwa namna swala hilo lilivyo kiuka haki na taratibu za kiutumishi. Maaskofu wetu mlikuwa kimya bila kuunyoshea kidole utawala uliokuwepo.

6. November 3, 2025 wakati wa sherehe za kuapishwa Rais mteule Dr. Samia Suluhu Hassan, Watanzania tulionao Viongozi wa dini ya Kiislaam na Kikristo mkipata nafasi ya kufungua Sherehe hizo kwa dua na sala. Watanzania tuliona Kiongozi wa dini ya Kiislaam mmoja tu Mufti. Dr. Abuubakar Zuberi akipewa nafasi, na baada yake Viongozi wa Taasisi kadhaa za Kikristo walipewa nafasi ya kusimamia na kuomba. Haki ipi mnazungumzia japo katika hili dogo tu mmeshindwa kuona haki ya Viongozi wengine wa Kiislaam kutoka Taasisi zingine. Kwani hamuwezi kusema hapa Waislaam hawakutendewa Haki. Au haki kweni ni kwa nani

Ndio maana TUNAWASIKILIZA, KISHA TUNAWAPUUZA!

Kwa sababu hatuoni dhamira ya dhati bali chuki za wazi kwa Rais Samia. Pia hatushangai Maaskofu wetu kumshambulia Rais Samia, tumezoea kuona mkitumia madhabahu kuwashambulia watawala Waislaam licha ya kuwa wanauwezo wa kufanya vizuri katika utawala wao.

Mlifanya hivyo kwa Rais Kikwete, mkaenda mbali zaidi na kusema nchi haitatawalika. Makanisa yote nchini yakaja na madai yaKatiba mpya kwa Rais Kikwete, nae akakubali. Mchakato ukaanza

Tukaingia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kabla mchakato haujakamilika. Mchakato wa Katiba ulikuwa hatua za mwisho. Akaingia Rais Magufuli, tukaona mkiwa kimya, hakuna madai ya Katiba mpya tena. Tukagundua tatizo halikuwa Katiba mpya, tatizo alikuwa Rais Kikwete.

Alipo ondoka Rais Magufuli na kuingia Rais Samia, madai ya Katiba mpya yakaanza tena. Na Sasa sio tu Katiba mpya, ni haki za watanzania. Sisi TUNAWASIKILIZA KISHA TUNAWAPUUZA kwa sababu tatizo kwenu sio Katiba, sio Haki, sio maridhiano. Tatizo kwenu ni Rais Samia.

Aluta continua
Mimi nakazia inaweza ikawa dhehebu lolote lile na hasa nyie mliyeunga mkono Bunge na Serikali ya Dikteka Simba Jike. Mnashindwa pa kutokea, dhamira zinawasuta, mnashindwa muachia hvyo vipato vya damu.

Hii ndiyo laana kubwa, baadala ya kupiga magoti na kusali msamehewe siku hiyo ikifika msamehewe kwa kusaliti roho za watu zaidi ya 10,000 mnaona hata hawa wapenda haki muwabadirishe wawe kama nyie.

Siku hiyo ikifika utaona kiu na utaomba maji upoze kiu lakini utakapopanua mdomo wako ili unywe hayo maji utashangaa hayo maji si maji itakua mafuta yanayowaka damu mdomoni mwako. Na siku hiyo itakuja.

Na hii itachukua hata vizazi na vizazi maana hata vizazi vyenu badaΕ‚a ya kutubu vimeshangilia udhalimu huu.
 
Ndiyo novena mliyofunga ili watu 10,000 wauawe?
 
Umeandika andiko linalojieleza. Tatizo la TEC kwa sasa ni Padri Kitima. Msipomtimua Kitima hapo, atalichafua Kanisa Katoliki. Kabla ya Padri Kitima kuwa Katibu wa TEC hatujawahi kuona matamko ya namna hii.
Padre Raymond Saba karibu wa TEC aliuawa miaka ile ya Magufuli.
 
Ndiyo novena mliyofunga ili watu 10,000 wauawe?
Wewe kazania kuomba laana tu. Mmeteka, mmeua, mmepoteza maisha ya watu kwa sababu ya kung'ang'ania madaraka. Mkabaka katiba ya chama chenu, mkafarakana na kumteka Polepole. Mkaonywa mazidi kukaza shingo, yaiyotokea ndiyo hayo. Mnashindwa pa kutokea. Sasa mmeanza na TEC haaaaaaaaa, mtaliweza hilo jabali? TEC hajali wewe ni nani, neno lake HAKI. Nje waovu mnashindwa kumeza, kwa sababu shetani kawashika.

Cha ajabu sasa mmemuanza Trump, na ujue Rubio ni TEC, sasa utawasha moto, wataacha Nigeria kuja kumsalimu Simba Jike. Hivi njie hata mnaweza kujilinganisha na Ghadafi au Sadam, hata China wenyewe walishindwa kuwasaidia. Kwa Sadam Veto wali-abstain. Hawa wachina wakiona maji marefu huwa wanakimbia kwa sababu wanajua njie ni Useful Idiots- Toliet paper.
 
𝗕𝗔π—₯𝗔𝗭𝗔 π—Ÿπ—” π— π—”π—”π—¦π—žπ—’π—™π—¨ (π—§π—˜π—–) π— π—‘π—”π—§π—¨π—žπ—’π—¦π—˜π—” 𝗦𝗔𝗑𝗔 π—ͺπ—”π—žπ—”π—§π—’π—Ÿπ—œπ—žπ—œ.

Tumsifu Yesu Kristo.

Jina langu ni Joseph Simon Mapunda, Muumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga Mkoani Ruvuma ambaye kwa mapenzi ya Mungu mwaka jana 2024 nilikuja Dar es Salaam kikazi na naishi Tegeta.

Leo tarehe 15 Novemba, 2025 nimesoma andiko la Baraza la Maaskofu lililoitwa β€œTafakari ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Juu ya Yaliyotokea Siku na Baada ya Uchaguzi-2025”

Awali ya yote kabisa naomba kuchukua nafasi hii kutoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza ndugu zao katika vurugu zilizotokea tarehe 25 Oktoba, 2025 na siku zilizofuata wakati ambapo nchi yetu Tanzania ilijikuta katika matukio ambayo hayajawahi kutokea na hayafanani kabisa na utamaduni wa Watanzania. Matukio mageni haswa.

Naungana na Watanzania wote kuwaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka.

Napenda pia kuwapa pole wote waliopoteza mali zao, walipoteza biashara zao, walipoteza ajira zao na ambao wanapitia kipindi kigumu cha giza nene kutokana na kupoteza kipato ambacho kiliendesha maisha yao na familia zao ama wapendwa wao.

Kwa wale ambao wamehusika na uhuni huu ama kwa kuchochea ama kwa kutekeleza matukio ya uharibifu wa miundombinu ya umma, wizi wa mali za watu binafsi na umma, uchomaji moto wa majengo, magari na biashara za watu mbalimbali, Mwenyezi Mungu mwenye kutoa haki awape wanachostahili.

Naomba nirudi kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), bila kupepesa macho naomba kusema wazi nasikitishwa sana na mwenendo wa TEC kutoa matamko na maandiko ambayo badala ya kuponya Taifa yanachochea mgawanyiko, uhasama na kuligombanisha Kanisa na Serikali. Ni kweli Maaskofu ndio viongozi wakuu wa majimbo ya Kanisa Katoliki lakini ni muhimu Mababa Askofu mkaheshimu demokrasia na haki ya waumini wa Kanisa Katoliki kwa kutofanya mambo ambayo yanatokana na matakwa yenu, hayana baraka za waumini na yanawaharibia waumini wa Kanisa hili lenye heshima kubwa hapa Tanzania na ambalo limejengwa kwa jasho jingi la Watanzania vizazi na vizazi.

Nimeona mara kadhaa mnavyotoa matamko yenye vinasaba vya Kisiasa ambayo hakuna asiyejua kuwa yana mwelekeo wa siasa za upinzani na yanalenga kuishambulia Serikali. Sina tatizo na hoja mnazojenga lakini muhimu hapa kwa nini mnatumia Kanisa kufanya minyukano ya Kisiasa? Sisi Wakatoliki tumejenga Kanisa hili ili litupe huduma za kiroho, lihubiri Injili, lituweke pamoja na lidumishe amani na upendo kwa mwanadamu. Mnayoyafanya mnakiuka misingi hii.

Matukio yaliyotokea tarehe 29 Oktoba, 2025 na siku kadhaa za mbele hakuna yaliyemfurahisha, kwa nini nyie TEC mnaibuka na andiko la namna hii tena siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutoa hotuba ya kuwaunganisha Watanzania, ya kuhimiza amani na utulivu, ya kujibu hoja za vijana na ya kuendeleza mkono wa maridhiano? Kwa nini Kanisa langu mnafanya mambo haya?

Tuseme Waumini wa Kanisa Katoliki na wanaopendezwa na mambo yanayoendelea nchini watawashangilia na kwa kuwa kuna kampeni ya mitandaoni ya kuitisha maandamano tarehe 9 Desemba, 2025 ili wajitokeze tena kupambana na vyombo vya dola kama ilivyokuwa tarehe 29 Oktoba, 2025, mnataka watu wengine wauawe? hata wale ambao hawahusiki na uchochezi huu? Mnataka watu wengine waingie kwenye umasikini kwa biashara zao kuvamiwa, kuibiwa, kuharibiwa na kuchomewa moto? Au tuseme mnataka nchi iingie katika mapinduzi? Hamzijui gharama za mapinduzi?

Nimesoma andiko lenu mstari kwa mstari. Nataka niwaulize hoja chache kabisa na nyie mtafakari huku mkiongozwa na Roho Mtakatifu na roho wa haki;

1. Hivi Mababa Askofu kwenye andiko lenu mnasema tarehe 29 Oktoba, 2025 waandamaji walishambuliwa na kuuawa. Naomba kuuliza wale walikuwa waandamanaji au waleta vurugu, wezi na waharibifu wa mali za umma? Nyie mmetembea nchini nyingi Duniani, watu wanaoandamana huwa wanafanya vitendo ambavyo vilifanyika siku ile? Waandamaji wanakwenda kuwatia umasikini binadamu wenzao na kutishia maisha yao au wanakwenda kudai haki zao kwa watawala? Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mnaowaita waandamanaji walikuwa na silaha za moto na wameua askari polisi ambao walikuwa wanakabiliana nao walipokuwa wanakwenda kuvamia mali za watu kuvunja na kuiba? Mnafahamu hao watu wameua watu wasio na hatia wakijiita ni Askari?

2. ⁠Mababa Askofu mnajua kuwa hao mnaowaita waandamanaji walivamia vituo vya polisi ili kuchukua silaha na walipozikosa walivichoma moto vituo vya polisi vingi? mababa Askofu ina maana hamjuia madhara ya makundi ya wahuni kuchukua silaha na kuvamia watu na biashara zao? Mlitaka Askari wafanyeje? Nyie wenyewe nyumba zenu mmeweka Askari wenye silaha, leo watu waje kuvamia nyumba ya Askofu wachome moto na kisha waanze kutaka kuingia ndani hao Askari wenu watawaacha?

3. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mnaowaita Waandamanaji walikwenda kuchoma moto jengo la Mawasiliano ambalo sio tu lingesababisha kuzimwa kwa mawasiliano yote bali nchi ingekosa mawasiliano kwa asilimia 100 kwa muda usiojulikana. Mnajua kuwa watu hao walishachoma eneo la mapokezi na jengo hilo liliokolewa na Askari Zimamoto waliowahi kabla ya moto kusambaa. Mnajua madhara ambayo yangetokea kwa nchi kukosa mawasiliano kabisa? Madhara kwa huduma za kifedha, mapato ya Serikali, huduma za matibabu hospitali, elimu na biashara zao watu.

4. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mliowaita waandamanaji wamechoma moto vituo vya mafuta. Hamjui madhara ya kituo cha mafuta kikiungua hadi kufika hatua ya kulipuka?

5. ⁠Mababa Askofu mnahamu kuwa uharibifu wa miundombinu ya mwendokasi umesababisha huduma hiyo kusitishwa? Mnajua madhara yake? Kwa sababu nyie hamsafirii usafiri wa umma, mnatumia magari binafsi ambayo sisi waumini tumewanunulia.

6. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa vijana waliokuwa wanapambana kutafuta kipato wamefirisika na hivi sasa wanakosa mpaka pesa ya kununua chakula cha watoto wao majumbani kwa sababu hao mnaowaita waandamanaji wamewaibia na kuharibu kabisa biashara zao?

7. ⁠Mababa Askofu mnafahamu madhara mengine mengi ambayo kama Nchi tunayapitia kutokana na vurugu zile?

Mababa Askofu hamuoni kuwa sio sawa kwa chombo hiki cha Dini, cha Kanisa Katoliki kubeba ajenda za chama cha upinzani ambacho kimeamua kutoshiriki uchaguzi ambao ni takwa la kikatiba ili kihamasishe watu kuleta vurugu ndani ya nchi? Kwani mkitoa tamko la kujenga imani za watu, watu kumrudia Mungu, kutubu na kujisahihisha pamoja kuhamasisha amani, upendo na utulivu mtapungukiwa nini?

Sawa, sasa mnatwambiaje Wakatoliki tujiandae kwa majambia, visu shoka, mawe na manati ili tukapambane na Polisi wenye silaha na JWTZ tarehe 9 Desemba, 2025 ili mje muandike tafakari nyingine ya TEC au mtatuletea bunduki, mabomu na mizinga ya kukabiliana na dola inayosimamia utawala wa Sheria?

Rais kaunda tume ya kuchunguza chanzo cha vurugu na kutoa mapendekezo ya namna ya kushughulikia mambo yaliyojitokeza tarehe 29 Oktoba, 2025 na nyie mmetoa tamko siku inayofuata, kwa hiyo mnataka sisi Wakatoliki tumsikilize Rais au tuwasikilize nyinyi TEC? Kwa nini mnataka kushindana na Rais? Hii nchi inaongozwa na TEC au inaongozwa na Serikali ambayo imewekwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi?

Kama na nyie TEC mnataka kuwa viongozi wa kisiasa kwa nini msiwe mnagombea nafasi za kisiasa kama wanavyofanya viongozi wa madhehebu mengine ya Kikristo? Ili nanyi muwe na haki na mamlaka ya kiuwakilishi. Maana hivi mnavyofanya mnapaswa kuulizwa ni wananchi wanawatuma au mnajituma wenyewe?

Hamkuanza tabia hizi leo, mlifanya sana wakati wa tawala zilizopita. Hivi mmewahi kuwaza viongozi wa Serikali ambao ni Wakatoliki tena wengine ni wasaidizi wa karibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnawaweka katika mazingira gani? Hebu vaeni viatu vya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ni Mkatoliki, Wasaidizi katika Ofisi Binafsi ya Rais ambao ni Wakatoliki na wanakuja kusali kwenye Ibada ambazo nyie mnaacha kuhubiri Injili na mnaanza kuhubiri hoja za Vyama vya Siasa, wanajisikiaje hawa?

Naomba kuwauliza TEC, kwa nini hamkusubiri Tume ya Uchunguzi ifanye kazi kisha ilete majibu? Mnajua tume itakuja na majibu gani? Hivi ikija na majibu ya sababu za msingi za namna vyombo vilivyokabiliana na matukio yale, mtabadilisha andiko na tamko lenu?

Mababa Askofu ina maana hamjui kuwa kinachoendelea ni ushawishi mkubwa wa watu wasioitakia mema Tanzania?

Mababa Askofu hamsikii hoja za kwamba mnaipiga vita Serikali hii kwa sababu Rais sio Mkatoliki? Kwamba mmeshaona Kanisa Katoliki ndio pekee lenye haki ya kuweka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Labda niulize Rais Samia amefanya mangapi ambayo huko nyuma Kanisa Katoliki lilinyimwa? Hivi mnadhani Serikali ikikunjua makucha Kanisa litabaki salama? Mmesahau jinsi Hayati Rais Magufuli alivyowashughulikia? Mmesahau jinsi Rais Samia alivyowasaidia? Kwa nini mnafanya mipango ya kumkwamisha huyu Mama Rais Samia. Amekosa nini?

Hayo madai ya wanasiasa ambayo na nyinyi mmefanya ajenda yenu hamjui majibu yake?

Hamjui kama Rais Samia ameahidi katika kipindi cha miaka mitano tutapata Katiba mpya? Hamjasikia ahadi ya maridhiano? Hamjasikia mipango ya mageuzi ya kiuchumi? Hamna ufahamu na falsafa ya R nne na namna ambavyo Rais Samia ameanza kuzitekeleza?

Mababa Askofu hamjui namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita imechukua hatua madhubuti za kujenga uchumi na kukuza kipato cha Watanzania? Hamjui namna ambavyo Rais Samia ameongeza fursa za ukuaji wa demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kisiasa na uhuru wa masuala mengine mengi? Mmesahau jinsi mambo haya yalivyobanwa wakati wa utawala wa Mkatoliki mwenzetu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli?

Naomba kuwasihi, msitukwaze Wakatoliki, msiwagombanishe Watanzania na Serikali yao, msiwe chanzo cha machafuko ya nchi. Nawasihi kwa unyenyekevu, fanyeni jitihada za kuliunganisha Taifa, na kama haiwezekani basi kaeni kimya muache Wadau wengine waunganishe Taifa.

Mwacheni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aongoze Tanzania, acheni Tanzania idumishe amani na waacheni Watanzania waamue wanataka nchi iendaje.

Naiomba Serikali isisite kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi wa Kanisa Katoliki ambao wanatupeleka katika mwelekeo huu. Mimi ni Mkatoliki, najua sio viongozi wote wa Kanisa hili wanafurahishwa na mwenendo huu, najua najua ubabe na utamaduni usio wa kidiplomasia ndani ya Kanisa unaficha sauti za Wakatoliki ambao wanatofautiana na msimamo wa NEC. Acheni kufanya hivyo viongozi wangu, mnatukwaza waumini.

Kaeni mbali na siasa na pambaneni na kueneza Injili na kuunganisha watu wa Mungu. Sambazeni upendo na usuluhishi, tangazeni amani na upendo na muwe na furaha pale nchi inapokuwa na amani.

Tumsifu Yesu Kristo.

Acha Kanisa litutetee. Wakoloni Weusi wamegeuka kuwa Vyura viziwi hawawasikilizi Wananchi wake.

Sisi Wakatoliki tunakubaliana na viongozi wetu. Wewe hama Kanisa. Kuna makanisa mengi tu siyo lazima uwe Katoliki.
 
Ukiwa hukubaliani na muongozo wa kanisa basi toka kwenye hilo kanisa jiunge na lingine au anzisha lako.

Maana huendani na misingi ya hilo kanisa.
Vivyohivyo ukiwa hukubaliani na utaratibu wa nchi ya Tanzania ondoka au anzisha nchi yako.
 
Amani na haki ni pande mbili za shilingi.
"There can be no peace without justice, and no justice without peace.” β€” Pope John Paul II
 
Wanaopiga kelele ni wakatoliki tu. CCT, WASABATO, WALOKOLE n BAKWATA wapo na Samia. Na mpiga kelele mkubwa ni Padri Kitima nduye na Tundu Lisu. Hakuna jipya hapo
We maku kweli, kwa hivyo ni lazima kila taasisi ya kidini imuunge mkono samuya?!
Kwa akili ipi aliyonayo kichwani?? Ile ya kupata zero form 4?!
 
Point niliyoiona ni moja tu TEC iache kujihusisha na siasa wadeal na waumini wao ili kuifikia mbingu bado wanamatatizo mengi kwenye makanisa yao

1. Waumini kufanya ngono makanisani

2. Nguo za kubana na vimini vilivyopitiliza ndani ya makanisa

3. Kufundisha bibilia kuliko kuchangisha sadaka

3. Waumini kutumia midaharati na vilevi vikali

4. Maaskofu kutetea ushoga na usagaji

5. Dini kuwa biashara
 
Kweli wew punda anayetafuta uchawa. Umeandika pumba melee baasha wako
 
Kumbuka hata wewe hauko salama,huu utawala umekuwa kama mbwa mwitu,Kuna kipindi wanakulana wenyewe kwa wenyewe,

Watu wasio na hatia wanauwawa kiholela wewe unaletaje siasa?

Mwisho kabisa ukisikia TEC wanaonya jambo kaa kimya TEC imesheheni watu wenye weledi wa hali ya juu!
 
Acha kujiita mkatoliki shekhe
leo leo unamkana mtume Mudi kwa sababu ya kuitetea serikali
 
Kama hujafurahishwa na tamko la TEC basi fuata lile la Mashehe
 
Njoo Sabato
 
Acha uchochezi, wewe sio mkatoliki.
 
Hawa nao wanatakiwa wapige mawaidha kwa waumini wao

1. Waache zinaa

2. Wamjue Allah ukweli wa kumjua

3. Mabinti wa kiislamu wavae vizuri sio kuvaa kama wadangaji miskitini

4. Wapiganie uislamu kote duniani uwepo utajo wa Allah (S.W)

5. Vijana wa kiislamu wapewe fikra waache kutumia midaharati

Hio siasa wawaachie wanasiasa mambo ya kidini yapo mengi hawajafanya wanakurupukia siasa
 
Back
Top Bottom