PostGE2025 Baraza la maaskofu Tanzania (TEC) mnatukosea sana wakatoliki

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Je Mapadri waliochinja watu maelfu ndani ya kanisa huko Rwanda waliagizwa na kanisa?
Nyinyi wapuuzi we're talking about current issues and current situations in our country, nawaambia kila siku tunazungumzia yanayoendelea nchini kwa wakati huu sio kufanya comparison kwa ya nchi nyingine wakati uliopita tuzungumzie yetu kwa wakati huu hatupo 1980 sasa ni 2025.. zungumza padri gani kachinja mtu mwaka huu wa 2025 nchini kwetu humu mtaje.. huna pita hivi usiongee ujinga kupandikiza chuki za kijingajinga na kidini bila kuangalia consequences zake ni zipi, pumbave wahed
 
Upumbavu mtupu, yani TEC wasiseme kisa Nchimbi Mkatoliki! Kisa kuna wafanyakazi wakatoliki ikulu!
Kwani maelfu ya hao waliouwawa hakuna waumini Wakatoliki? Yani kazi ya Nchimbi na hao wenzake Ikulu waliopo kwa kupora madaraka ina thamani zaidi kuliko uhai wa maelfu ya waumini wengine wakatoliki!
 
Tunazungumzia TEC ya tanzania. Usihishe goli
Katoliki ni kanisa moja mkuu na kiongozi wenu ni mmoja tu Papa (Mungu duniani aka Mungu anayechaguliwa).
Nieleze kuhusu Katoliki kuhusishwa na mauaji ya kimbali huko Rwanda. Sababu ilikiuwa ni nini?
 
Unamaliza tu miti. CCM mmeshikwa pabaya na hapa tulipofika hamtoki.
 
Katoliki ni kanisa moja mkuu na kiongozi wenu ni mmoja tu Papa (Mungu duniani aka Mungu anayechaguliwa).
Nieleze kuhusu Katoliki kuhusishwa na mauaji ya kimbali huko Rwanda. Sababu ilikiuwa ni nini?
tunazungumzia TEC. Oct 29 yaliyotokea hayakutokea rwanda.
Tunajadili ya hapa kwanza
 
Mimi nipatie maelezo kuhusu hili kaka.

This is Bishop Athanase Seromba of the Catholic Church who was involved in the massacres of over 800,000 people in the Rwandan genocide of 1994.

Worse still, after those horrific massacres the Catholic Church helped these people escape, for example, Seromba was smuggled into Italy and there he continued to serve as a priest under a new name.

When you come with matters of wanting to whitewash these people, know that they have no good in them, they have nothing to tell us because history judges them.
1763271038892.png

View: https://x.com/Getrude_mollel/status/1989623966030340176?s=20
 
Huwa mnatambua ID zenu zina comments na post zenu zote za nyuma?

Kujitia ukatoliki leo hii hakuondoi ulichowahi kuandika kabla.

Ninyi sio sisi, sisi tunatambuana kwa lugha moja ya haki.

Hakuna lugha mtakayoitumia kumpinga anayehubiri haki tukawaelewa.

Sio sawa kushambulia mtu wala ID yake, lakini ni sahihi kudiscredit andiko la mtu kutokana na historia yake kimaadili ambayo yawezekana amesahau kuwa imetunzwa .
 
Mimi nipatie maelezo kuhusu hili kaka.

This is Bishop Athanase Seromba of the Catholic Church who was involved in the massacres of over 800,000 people in the Rwandan genocide of 1994.

Worse still, after those horrific massacres the Catholic Church helped these people escape, for example, Seromba was smuggled into Italy and there he continued to serve as a priest under a new name.

When you come with matters of wanting to whitewash these people, know that they have no good in them, they have nothing to tell us because history judges them.
View attachment 3502541

View: https://x.com/Getrude_mollel/status/1989623966030340176?s=20

Haha kwa hiyo umehama kutoka tz unataka tujadili ya rwanda.?
What about yalitokea tanzania?
 
𝗕𝗔𝗥𝗔𝗭𝗔 𝗟𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗦𝗞𝗢𝗙𝗨 (𝗧𝗘𝗖) 𝗠𝗡𝗔𝗧𝗨𝗞𝗢𝗦𝗘𝗔 𝗦𝗔𝗡𝗔 𝗪𝗔𝗞𝗔𝗧𝗢𝗟𝗜𝗞𝗜.

Tumsifu Yesu Kristo.

Jina langu ni Joseph Simon Mapunda, Muumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga Mkoani Ruvuma ambaye kwa mapenzi ya Mungu mwaka jana 2024 nilikuja Dar es Salaam kikazi na naishi Tegeta.

Leo tarehe 15 Novemba, 2025 nimesoma andiko la Baraza la Maaskofu lililoitwa “Tafakari ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Juu ya Yaliyotokea Siku na Baada ya Uchaguzi-2025”

Awali ya yote kabisa naomba kuchukua nafasi hii kutoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza ndugu zao katika vurugu zilizotokea tarehe 25 Oktoba, 2025 na siku zilizofuata wakati ambapo nchi yetu Tanzania ilijikuta katika matukio ambayo hayajawahi kutokea na hayafanani kabisa na utamaduni wa Watanzania. Matukio mageni haswa.

Naungana na Watanzania wote kuwaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka.

Napenda pia kuwapa pole wote waliopoteza mali zao, walipoteza biashara zao, walipoteza ajira zao na ambao wanapitia kipindi kigumu cha giza nene kutokana na kupoteza kipato ambacho kiliendesha maisha yao na familia zao ama wapendwa wao.

Kwa wale ambao wamehusika na uhuni huu ama kwa kuchochea ama kwa kutekeleza matukio ya uharibifu wa miundombinu ya umma, wizi wa mali za watu binafsi na umma, uchomaji moto wa majengo, magari na biashara za watu mbalimbali, Mwenyezi Mungu mwenye kutoa haki awape wanachostahili.

Naomba nirudi kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), bila kupepesa macho naomba kusema wazi nasikitishwa sana na mwenendo wa TEC kutoa matamko na maandiko ambayo badala ya kuponya Taifa yanachochea mgawanyiko, uhasama na kuligombanisha Kanisa na Serikali. Ni kweli Maaskofu ndio viongozi wakuu wa majimbo ya Kanisa Katoliki lakini ni muhimu Mababa Askofu mkaheshimu demokrasia na haki ya waumini wa Kanisa Katoliki kwa kutofanya mambo ambayo yanatokana na matakwa yenu, hayana baraka za waumini na yanawaharibia waumini wa Kanisa hili lenye heshima kubwa hapa Tanzania na ambalo limejengwa kwa jasho jingi la Watanzania vizazi na vizazi.

Nimeona mara kadhaa mnavyotoa matamko yenye vinasaba vya Kisiasa ambayo hakuna asiyejua kuwa yana mwelekeo wa siasa za upinzani na yanalenga kuishambulia Serikali. Sina tatizo na hoja mnazojenga lakini muhimu hapa kwa nini mnatumia Kanisa kufanya minyukano ya Kisiasa? Sisi Wakatoliki tumejenga Kanisa hili ili litupe huduma za kiroho, lihubiri Injili, lituweke pamoja na lidumishe amani na upendo kwa mwanadamu. Mnayoyafanya mnakiuka misingi hii.

Matukio yaliyotokea tarehe 29 Oktoba, 2025 na siku kadhaa za mbele hakuna yaliyemfurahisha, kwa nini nyie TEC mnaibuka na andiko la namna hii tena siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutoa hotuba ya kuwaunganisha Watanzania, ya kuhimiza amani na utulivu, ya kujibu hoja za vijana na ya kuendeleza mkono wa maridhiano? Kwa nini Kanisa langu mnafanya mambo haya?

Tuseme Waumini wa Kanisa Katoliki na wanaopendezwa na mambo yanayoendelea nchini watawashangilia na kwa kuwa kuna kampeni ya mitandaoni ya kuitisha maandamano tarehe 9 Desemba, 2025 ili wajitokeze tena kupambana na vyombo vya dola kama ilivyokuwa tarehe 29 Oktoba, 2025, mnataka watu wengine wauawe? hata wale ambao hawahusiki na uchochezi huu? Mnataka watu wengine waingie kwenye umasikini kwa biashara zao kuvamiwa, kuibiwa, kuharibiwa na kuchomewa moto? Au tuseme mnataka nchi iingie katika mapinduzi? Hamzijui gharama za mapinduzi?

Nimesoma andiko lenu mstari kwa mstari. Nataka niwaulize hoja chache kabisa na nyie mtafakari huku mkiongozwa na Roho Mtakatifu na roho wa haki;

1. Hivi Mababa Askofu kwenye andiko lenu mnasema tarehe 29 Oktoba, 2025 waandamaji walishambuliwa na kuuawa. Naomba kuuliza wale walikuwa waandamanaji au waleta vurugu, wezi na waharibifu wa mali za umma? Nyie mmetembea nchini nyingi Duniani, watu wanaoandamana huwa wanafanya vitendo ambavyo vilifanyika siku ile? Waandamaji wanakwenda kuwatia umasikini binadamu wenzao na kutishia maisha yao au wanakwenda kudai haki zao kwa watawala? Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mnaowaita waandamanaji walikuwa na silaha za moto na wameua askari polisi ambao walikuwa wanakabiliana nao walipokuwa wanakwenda kuvamia mali za watu kuvunja na kuiba? Mnafahamu hao watu wameua watu wasio na hatia wakijiita ni Askari?

2. ⁠Mababa Askofu mnajua kuwa hao mnaowaita waandamanaji walivamia vituo vya polisi ili kuchukua silaha na walipozikosa walivichoma moto vituo vya polisi vingi? mababa Askofu ina maana hamjuia madhara ya makundi ya wahuni kuchukua silaha na kuvamia watu na biashara zao? Mlitaka Askari wafanyeje? Nyie wenyewe nyumba zenu mmeweka Askari wenye silaha, leo watu waje kuvamia nyumba ya Askofu wachome moto na kisha waanze kutaka kuingia ndani hao Askari wenu watawaacha?

3. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mnaowaita Waandamanaji walikwenda kuchoma moto jengo la Mawasiliano ambalo sio tu lingesababisha kuzimwa kwa mawasiliano yote bali nchi ingekosa mawasiliano kwa asilimia 100 kwa muda usiojulikana. Mnajua kuwa watu hao walishachoma eneo la mapokezi na jengo hilo liliokolewa na Askari Zimamoto waliowahi kabla ya moto kusambaa. Mnajua madhara ambayo yangetokea kwa nchi kukosa mawasiliano kabisa? Madhara kwa huduma za kifedha, mapato ya Serikali, huduma za matibabu hospitali, elimu na biashara zao watu.

4. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa hao mliowaita waandamanaji wamechoma moto vituo vya mafuta. Hamjui madhara ya kituo cha mafuta kikiungua hadi kufika hatua ya kulipuka?

5. ⁠Mababa Askofu mnahamu kuwa uharibifu wa miundombinu ya mwendokasi umesababisha huduma hiyo kusitishwa? Mnajua madhara yake? Kwa sababu nyie hamsafirii usafiri wa umma, mnatumia magari binafsi ambayo sisi waumini tumewanunulia.

6. ⁠Mababa Askofu mnafahamu kuwa vijana waliokuwa wanapambana kutafuta kipato wamefirisika na hivi sasa wanakosa mpaka pesa ya kununua chakula cha watoto wao majumbani kwa sababu hao mnaowaita waandamanaji wamewaibia na kuharibu kabisa biashara zao?

7. ⁠Mababa Askofu mnafahamu madhara mengine mengi ambayo kama Nchi tunayapitia kutokana na vurugu zile?

Mababa Askofu hamuoni kuwa sio sawa kwa chombo hiki cha Dini, cha Kanisa Katoliki kubeba ajenda za chama cha upinzani ambacho kimeamua kutoshiriki uchaguzi ambao ni takwa la kikatiba ili kihamasishe watu kuleta vurugu ndani ya nchi? Kwani mkitoa tamko la kujenga imani za watu, watu kumrudia Mungu, kutubu na kujisahihisha pamoja kuhamasisha amani, upendo na utulivu mtapungukiwa nini?

Sawa, sasa mnatwambiaje Wakatoliki tujiandae kwa majambia, visu shoka, mawe na manati ili tukapambane na Polisi wenye silaha na JWTZ tarehe 9 Desemba, 2025 ili mje muandike tafakari nyingine ya TEC au mtatuletea bunduki, mabomu na mizinga ya kukabiliana na dola inayosimamia utawala wa Sheria?

Rais kaunda tume ya kuchunguza chanzo cha vurugu na kutoa mapendekezo ya namna ya kushughulikia mambo yaliyojitokeza tarehe 29 Oktoba, 2025 na nyie mmetoa tamko siku inayofuata, kwa hiyo mnataka sisi Wakatoliki tumsikilize Rais au tuwasikilize nyinyi TEC? Kwa nini mnataka kushindana na Rais? Hii nchi inaongozwa na TEC au inaongozwa na Serikali ambayo imewekwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi?

Kama na nyie TEC mnataka kuwa viongozi wa kisiasa kwa nini msiwe mnagombea nafasi za kisiasa kama wanavyofanya viongozi wa madhehebu mengine ya Kikristo? Ili nanyi muwe na haki na mamlaka ya kiuwakilishi. Maana hivi mnavyofanya mnapaswa kuulizwa ni wananchi wanawatuma au mnajituma wenyewe?

Hamkuanza tabia hizi leo, mlifanya sana wakati wa tawala zilizopita. Hivi mmewahi kuwaza viongozi wa Serikali ambao ni Wakatoliki tena wengine ni wasaidizi wa karibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnawaweka katika mazingira gani? Hebu vaeni viatu vya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ni Mkatoliki, Wasaidizi katika Ofisi Binafsi ya Rais ambao ni Wakatoliki na wanakuja kusali kwenye Ibada ambazo nyie mnaacha kuhubiri Injili na mnaanza kuhubiri hoja za Vyama vya Siasa, wanajisikiaje hawa?

Naomba kuwauliza TEC, kwa nini hamkusubiri Tume ya Uchunguzi ifanye kazi kisha ilete majibu? Mnajua tume itakuja na majibu gani? Hivi ikija na majibu ya sababu za msingi za namna vyombo vilivyokabiliana na matukio yale, mtabadilisha andiko na tamko lenu?

Mababa Askofu ina maana hamjui kuwa kinachoendelea ni ushawishi mkubwa wa watu wasioitakia mema Tanzania?

Mababa Askofu hamsikii hoja za kwamba mnaipiga vita Serikali hii kwa sababu Rais sio Mkatoliki? Kwamba mmeshaona Kanisa Katoliki ndio pekee lenye haki ya kuweka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Labda niulize Rais Samia amefanya mangapi ambayo huko nyuma Kanisa Katoliki lilinyimwa? Hivi mnadhani Serikali ikikunjua makucha Kanisa litabaki salama? Mmesahau jinsi Hayati Rais Magufuli alivyowashughulikia? Mmesahau jinsi Rais Samia alivyowasaidia? Kwa nini mnafanya mipango ya kumkwamisha huyu Mama Rais Samia. Amekosa nini?

Hayo madai ya wanasiasa ambayo na nyinyi mmefanya ajenda yenu hamjui majibu yake?

Hamjui kama Rais Samia ameahidi katika kipindi cha miaka mitano tutapata Katiba mpya? Hamjasikia ahadi ya maridhiano? Hamjasikia mipango ya mageuzi ya kiuchumi? Hamna ufahamu na falsafa ya R nne na namna ambavyo Rais Samia ameanza kuzitekeleza?

Mababa Askofu hamjui namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita imechukua hatua madhubuti za kujenga uchumi na kukuza kipato cha Watanzania? Hamjui namna ambavyo Rais Samia ameongeza fursa za ukuaji wa demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kisiasa na uhuru wa masuala mengine mengi? Mmesahau jinsi mambo haya yalivyobanwa wakati wa utawala wa Mkatoliki mwenzetu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli?

Naomba kuwasihi, msitukwaze Wakatoliki, msiwagombanishe Watanzania na Serikali yao, msiwe chanzo cha machafuko ya nchi. Nawasihi kwa unyenyekevu, fanyeni jitihada za kuliunganisha Taifa, na kama haiwezekani basi kaeni kimya muache Wadau wengine waunganishe Taifa.

Mwacheni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aongoze Tanzania, acheni Tanzania idumishe amani na waacheni Watanzania waamue wanataka nchi iendaje.

Naiomba Serikali isisite kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi wa Kanisa Katoliki ambao wanatupeleka katika mwelekeo huu. Mimi ni Mkatoliki, najua sio viongozi wote wa Kanisa hili wanafurahishwa na mwenendo huu, najua najua ubabe na utamaduni usio wa kidiplomasia ndani ya Kanisa unaficha sauti za Wakatoliki ambao wanatofautiana na msimamo wa NEC. Acheni kufanya hivyo viongozi wangu, mnatukwaza waumini.

Kaeni mbali na siasa na pambaneni na kueneza Injili na kuunganisha watu wa Mungu. Sambazeni upendo na usuluhishi, tangazeni amani na upendo na muwe na furaha pale nchi inapokuwa na amani.

Tumsifu Yesu Kristo.
Mkuu na mimi ni Mkatoliki pia na nilikwisha jipambanua muda mrefu. Sijawahi kujubaliana na namna TEC chini ya Askofu Pisa na Katibu Mkuu Fr Kitima namna walivyojiingiza kisiasa. Moja kwa moja unaliona Kanisa letu hakina neutrality, unaliona likisafiri na hoja za CHADEMA.

Influence kubwa ilijengwa na Fr Kitima ambaye ni cousin brother wa Tundu Lissu.

Hata wakibisha hoja zako na kukutukana lakini hoja zako zitaishi kwa vile zimejikita katika kuleta umoja wa kitaifa
 
Akili za matopeni hizi. Kutaka uwajibikaji ndio kuleta mpasuko?

Hivi kwa serikali inayojali uhai wa raia wake IGP angekuwa bado yuko madarakani kweli kwa vifo na aina ya vifo vilivyotokea? Watu wamepigwa risasi majumbani mwao tena kwa kulengwa sio kwa bahati mbaya, hao nao walikuwa wanachoma vituo gani vya polisi?

Ametangazwa amepata kura milioni 31, wewe kwa akili zako siku hiyo kuna kura zilipigwa kufikia hiyo idadi?

Halafu usivyo na akili, mtu anayejali uhai wa raia wake angeweza kujigamba na kuwabananga waangalizi wa kimataifa eti "ongezeko la vituo vya kupigia kura ndilo lilifanya wapiga kura wasionekane". Huyu anayesema hivi ana akili kichwani mwake kweli? Ana nia njema na Taifa letu kweli?

Kwa hadhi ya kiti anachokalia, ana haja gani ya kukubali kudanganya uongo wa kitoto namna hii? Anajaribu kumdanganya nani? Kwa faida gani? Kwa faida ya nani?

Vurugu zilianza mapema sana, wasimamizi walikimbia kuokoa maisha yao na kutelekeza masunduku ya kupigia kura, hizo walizohesabu zilitoka wapi? Nani hakuona kura zilivyochomwa moto, kusambazwa na kuharibiwa? Walizotangaza walizitoa wapi?

Kwa mtu mwenye busara na hekima, walishindwa nini kusitisha kutangaza matokeo ya mikoa yote ambayo vurugu zilitokea? Nadhani hapa ndipo palikuwa pazuri pa kuanzia kwasababu ni ukweli usiopingika kuwa maeneo yote yaliyokumbwa na vurugu kura hazikupigwa na zilizopigwa hazikuhesabiwa. Sehemu kama Tunduma, Dsm, Mbeya, Mwanza na Arusha, kwa mtu mwenye kulipenda Taifa hili na asiye na dharau anawezaje kutangaza matokeo yake?

Siku nyingine unapotaka kutoa hoja, tuliza kichwa kwanza. Watu kama nyie ndio mliobeba damu za vijana waliopotea. Acheni upuuzi
 
Je Mapadri waliochinja watu maelfu ndani ya kanisa huko Rwanda waliagizwa na kanisa?
Hakuna padre alichinja mtu Rwanda, hizi stori sijui huwa mnasimuliwa vipi.Uzuri babu yangu katokea Rwanda upande wa mama na hizo simulizi za kanisa kuhusika ni tofauti na masimulizi yenu
 
Umeandika andiko linalojieleza. Tatizo la TEC kwa sasa ni Padri Kitima. Msipomtimua Kitima hapo, atalichafua Kanisa Katoliki. Kabla ya Padri Kitima kuwa Katibu wa TEC hatujawahi kuona matamko ya namna hii.
Kweli tupu Mkuu Venus Star , Fr Kitima ameiweka TEC mkononi mwake. Ni bora tu angevua kanzu na collar aungane na Dr Slaa kwenye magwanda ya khaki
 
Kwa hiyo hayo yote yaliyofanywa adhabu yake ni risasi za kifua na kichwa? Waliofuatwa kuuwawa majumbani na bar walikuwa wanachoma mwendokasi?

Ukipita Dar yote unaweza kuonesha uharibifu mkubwa uliofanyika wa kuhalalisha mauaji ya maelfu ya watu?

Pia acheni uongo, hakuna kituo cha mafuta kilichochomwa. Lake oil wamechomewa magari yaliokuwa kituoni ambayo hayazidi mawili kwa kila kituo na zaidi ni baadhi ya pump za mafuta zimefunjwa.
Kwa hiyo hicho kilichofanywa dhidi ya Lake Oil unaona ni sahihi?
 
Back
Top Bottom