PostGE2025 Baraza la maaskofu Tanzania (TEC) mnatukosea sana wakatoliki

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kweli tupu Mkuu Venus Star , Fr Kitima ameiweka TEC mkononi mwake. Ni bora tu angevua kanzu na collar aungane na Dr Slaa kwenye magwanda ya khaki
Kwetu mtu ambaye hajaoa hata kama ni mzee tunamwita mvulana.
Unajua huyu Mvulana Kitima ataliharibu kanisa katoliki liliojijengea umaarufu mkubwa Tanzania.
 
"If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. If an elephant has its foot on the tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality."
Archbishop Desmond Tutu, 1931-2021
 
Mimi si mkatili, lkn sadaka yangu ya leo jumapili nimeitoa RC.
 
Kama ww ni mkatoliki kweli na umeweka majina yako matatu, ni kama hujadanganya chochote. Sasa weka namba yako ya simu, na NIDA na vyote visome jina lako. Tunafahamu uchafu wenu usalama wa taifa uliotuikisha hapa.

Nimesoma ujumbe wako mrefu, huna popote unapoongelea haki, bali unaongelea amani ambayo imegeuzwa kutuona sisi watanzania wote ni wajinga. Huna popote unapodhibitisha rais kapata kura 31m kihalali. Ila unataka tumuoene ni rais kweli, na tumtii bila kumuonyesha kuwa hana uhalali wa umma. Rais ameunda tume ya uchaguzi, anaundaje tume ya uchunguzi wake yeye mwenyewe ni sehemu ya uhalifu? Unataka maaskofu waendelee kukaa kimya hadi lini?

Unatutajia mali zilizoharibiwa ni kweli, lakini ni machafuko gani hakuna uharibifu wa mali? Sababu zilizopolekea machafuko haya ziko wazi, nazo ni ccm na serekali kuendelea kuchezea box la kura. Uliona voters turnout ya juzi, iliendana na matokeo ya uchaguzi wa juzi? Basi maelezo yako yote na utetezi wako wote ujikite kwenye uchafu ule uliotoa matokeo yale ya urais, wabunge na madiwani.

Sasa ni hivi tarehe 9 december tunarudi tena barabarani, safari hii hakuna kuharibu mali za watu, lakini hatutakuwa tayari kuongozwa na watu wasio na uhalali wa umma. Kama mlitegemea mtaendelea kutuuzia hofu na amani ya hadaa ili muendelee kututawala kwa shuruti, safari hii haitawezekana. Kitendo cha kutushambulia kwa silaha za moto, kitapelekea mauji ya familia zenu pia, tutazika wote. Hatutaki maridhiano ya hadaa, tunataka rais aliyepora uchaguzi na kumwaga damu apishe, iundwe serekali ya mpito tupate katiba mpya, na mengine yaendelee.
 
Umeandika uharo mtupu. Bora ungeumalizia huko huko chooni, badala ya kutuletea huku. 🚮
Msome na huyu hapa:-
TUNAWASIKILIZA MAASKOFU KISHA TUNAWAPUUZA

Anaandika Mwl/ Tambulu Dodoma-Tanzania

Nianze kwa maneno ya Rais wa Marekani Jimmy Carter, amewahi kusema kuwa "Kanisa Katoliki linapopata nafasi ya Uongozi wa Kisiasa katika Nchi, nchi hiyo haiwezi kupata maendeleo....." Iwe maendeleo ya kiuchumi, Kisiasa, kielimu nk.

Hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu la Viongozi wa Makanisa (Maaskofu, Mapadri na Wachungaji) kushambulia uongozi wa Rais Samia kwa kigezo cha kutaka utawala wake utende haki kwa watanzania. Nimesikiliza hotuba iliyotolewa na Askofu Mkuu Ruwaichi jana akisema Taifa limegawika, watu wamepoteza wapendwa wao na mengine mengi. Kubwa zaidi Askofu Ruwaichi nae ameendelea kuunyoshea kidole utawala huu wa Rais Samia kwa kusisitiza swala la Haki na kwamba hakuna Amani bila Haki. Nae Askofu Musomba ameonyesha masikitiko yake kwa vifo vilivyo tokea na watu kupoteza wapendwa wao, wimbo ukabaki ule ule wa Haki kisha amani itakuja yenyewe.

Watanzania na dunia inazidi kuona Kasi ya wachungaji na maaskofu nchini kushambulia uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kudai haki za watu zinakandamizwa, na hivyo kuitaka Serikali ya Rais Samia na Rais Samia mwenyewe kulinda haki na uhuru wa watu.

Hilo ni jambo jema sana, hakuna asie jua umuhimu wa haki. Kama Viongozi wa dini wanafanya kazi nzuri kumkumbusha Rais Samia kuongoza nchi kwa misingi ya Haki ili kujenga umoja wa kitaifa na kulinda amani ya nchi yetu.

Tatizo langu mpaka nashawishika kuandika makala hii sio maneno ya Maaskofu wapendwa, bali dhamira na lengo la maneno yao. Kama ni mfatiliaji mzuri wa matukio na matendo ya Viongozi wa Kikristo unaweza kubaki na maswali mengi.

Ni kweli maaskofu wetu wanamaanisha Haki? Au ni aina nyingine ya vita dhidi ya Rais Samia na Serikali yake?

Machungu wanayo onyesha Maaskofu wetu kwa vifo kadhaa vilivyo tokea October, 29 katika Maandamano haramu ni machungu ya kweli au yameficha jambo jingine nyuma yake.

Haki zinazo zungumzwa na Viongozi wa Kanisa leo ni haki zipi? Haki hizo ni haki za nani? Ni haki za watanzania au haki za Wakristo.

Ni vigumu kushawishika na madai ya haki yanayo semwa na Viongozi wa Kikristo nchini hasa kwa kurejea kumbukumbu za namna Taasisi za Kikristo zinavyo kandamiza haki za Watanzania. Tujikumbushe matukio machache ili tuone kama madai ya haki yanayo semwa na Viongozi wa dini ya Kikristo yanaukweli au yanaficha dhamira zao dhidi ya Utawala wa Rais Samia

1. Mwaka 1992, CCT na TEC wameingia mkataba(Memorandum of Understanding) na Serikali ya Tanzania kuchota ma billion ya Shilling ambayo ni Kodi za watanzania kila mwezi kwa ajili ya kujinufaisha wao na Makanisa yao. Tukumbuke kuwa nchi yetu si nchi ya Kidini, kitendo cha Makanisa kutumia Kodi za Watanzania kulipa mishahara wachungaji na Maaskofu kinawanyima Haki watu wa dini nyingine. Kwa nini Maaskofu hawasemi Haki hii wanayodhulumu watu wa dini nyingine kwa kushirikiana na Serikali.

2. Mwaka 1998, Askofu Lwambano wa Parokia ya Mburahati alitoa maagizo ya kuvamiwa na kuawa Waislaam Msikiti wa Mwembechai Manzese Jijini Dar es salaam kwa madai kuwa wanafanya mihadhara inayo umiza hisia za Wakristo. Kwa maelekezo yake Jeshi la Polisi lilivamia Msikiti wa Mwembechai na Waislaam kadhaa wakapigwa risase na kuuawa huku wengine wakibaki vilema hadi leo. Damu za Watanzania hawa zilimwagika bila hatia yoyote huku Maaskofu wakishangilia. Kwa nini leo wanaumia sana kwa watu waliopoteza maisha kwa kufanya Maandamano haramu, kuharibu na kuchoma Mali za watu, kuharibu miundombinu ya umma kama kuchoma moto vituo vya mabasi ya mwendoiasi nk. Watanzania hawa na wale waliouawa Mwembechai kwa agizo la Kanisa wanatofauti gani. Kwa nini hatukusikia matamko ya Haki kwa damu za Waislaam wale waliouawa Mwembechai.

3. Waislaam kama sehemu ya raia wa nchi hii wamekuwa wakipiga kelele na kuomba Serikali ya Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kiislaam (OIC). Kwa kutoa mifano ya nchi wanachama wanavyo nufaika na Jumuiya hiyo ya OIC na kuwaletea maendeleo wananchi wake ikiwemo Benin, Msumbiji, Nigeria, Sierra Leon, Uganda, Urusi, Gabon, Guinea Bissau na hata baadhi ya nchi za Ulaya. Bila kujali kuwa Waislaam wana Haki na nchi yetu itanufaika na miradi mikubwa ya Maendeleo. Viongozi wa Makanisa wamekuwa mstari wa mbele kupinga jambo hilo na kusababisha Waislaam kupoteza haki yao. OIC walikuwa tayari kuanza ujenzi wa Chuo Kikuu hapa Tanzania, baada ya Viongozi wa Makanisa kupinga swala hilo mradi huo mkubwa wa Maendeleo ulijengwa Mbale Nchini Uganda. Maaskofu na Wachungaji wameanza lini kusemea haki za Watanzania. Hata Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya nje wakati huo Mh. Bernard Membe ilipotoa taarifa Bungeni kuwa Tanzania kujiunga na OIC hakuna madhara yoyote na badala yake Serikali yetu itanufaika, Kardinal Policap Pengo alimwita Mh. Membe na kumtaka asitishe mara moja mpango huo. Kwa maslahi yao Walidhulumu haki ya Mamilioni ya Waislaam na Watanzania wengine kujipatia miradi ya maendeleo. Makanisa yakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Serikali kuingiza swala la OIC na mahakama ya Kadhi katika Katiba yetu ni sawa na kuinajisi Katiba. Gazeti la Utatu Juma pili September 28- October 4, 2008.

4. Swala la mauaji na watu kutekwa, tatizo hili halikuanza wakati wa utawala wa Rais Samia. Kama kuna wakati watanzania wametekwa, kupotezwa na kuuawa ni wakati wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli. Wakati wa utawala wa Rais Magufuli ndipo kwa mara ya kwanza miili ya watu ilianza kuokotwa ufukweni mwa Bahati ya Hindi ikiwa kwenye viroba. Mauaji ya MKIRU(Mkuranga, Kibiti, Rufiji) ni wakati wa Rais Magufuli. Hali ilikuwa mbaya sana, Watanzania waliishi kwa hofu kubwa. Hakuna aliejua hatma ya kesho yake. Wanasiasa waliishi kama wako Gerezani, vyombo vya Habari vilifungwa midomo. Hata Bunge lilikuwa siri. Waliojaribu kusema walikula risase bila Idadi, hakuna Mtanzania aliekuwa na Haki. Maaskofu wetu mlikuwa likizo wakati huo. Wengi wenu mlikuwa sio tu Viongozi wa Rais Magufuli bali kipenzi chenu. Hotuba za haki hazikusikika, zaidi mliendelea kumuimbia nyimbo za kumsifu. Kwa nini Leo kwa Rais Samia

5. January 11,2019 Wafanya kazi 11 Waislaam wakiwemo MaProfesa, Madaktari, na watumishi waandamizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma-Tanzania walipewa uhamisho wa ghafla bila kuzingatia Sheria na haki zao kama watumishi. Wakati huo huo Serikali ya Rais Magufuli akapeleka watumishe wengine 11 wote Wakristo. Jambo ambalo lilipigiwa kelele na kukosolewa na watu mbalimbali kwa namna swala hilo lilivyo kiuka haki na taratibu za kiutumishi. Maaskofu wetu mlikuwa kimya bila kuunyoshea kidole utawala uliokuwepo.

6. November 3, 2025 wakati wa sherehe za kuapishwa Rais mteule Dr. Samia Suluhu Hassan, Watanzania tulionao Viongozi wa dini ya Kiislaam na Kikristo mkipata nafasi ya kufungua Sherehe hizo kwa dua na sala. Watanzania tuliona Kiongozi wa dini ya Kiislaam mmoja tu Mufti. Dr. Abuubakar Zuberi akipewa nafasi, na baada yake Viongozi wa Taasisi kadhaa za Kikristo walipewa nafasi ya kusimamia na kuomba. Haki ipi mnazungumzia japo katika hili dogo tu mmeshindwa kuona haki ya Viongozi wengine wa Kiislaam kutoka Taasisi zingine. Kwani hamuwezi kusema hapa Waislaam hawakutendewa Haki. Au haki kweni ni kwa nani

Ndio maana TUNAWASIKILIZA, KISHA TUNAWAPUUZA!

Kwa sababu hatuoni dhamira ya dhati bali chuki za wazi kwa Rais Samia. Pia hatushangai Maaskofu wetu kumshambulia Rais Samia, tumezoea kuona mkitumia madhabahu kuwashambulia watawala Waislaam licha ya kuwa wanauwezo wa kufanya vizuri katika utawala wao.

Mlifanya hivyo kwa Rais Kikwete, mkaenda mbali zaidi na kusema nchi haitatawalika. Makanisa yote nchini yakaja na madai yaKatiba mpya kwa Rais Kikwete, nae akakubali. Mchakato ukaanza

Tukaingia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kabla mchakato haujakamilika. Mchakato wa Katiba ulikuwa hatua za mwisho. Akaingia Rais Magufuli, tukaona mkiwa kimya, hakuna madai ya Katiba mpya tena. Tukagundua tatizo halikuwa Katiba mpya, tatizo alikuwa Rais Kikwete.

Alipo ondoka Rais Magufuli na kuingia Rais Samia, madai ya Katiba mpya yakaanza tena. Na Sasa sio tu Katiba mpya, ni haki za watanzania. Sisi TUNAWASIKILIZA KISHA TUNAWAPUUZA kwa sababu tatizo kwenu sio Katiba, sio Haki, sio maridhiano. Tatizo kwenu ni Rais Samia.

Aluta continua
 
Dunia yote inajua hivyo, wewe pekee ndiye unayepinga. Basi leta ushahidi ni nani aliwachinja wanyarwanda?


View: https://x.com/Getrude_mollel/status/1989623966030340176?s=20
Hizi narration huwa mnadanganywa sana.Hiko hivi kanisa lilikuwa linatoa hifadhi kwa watu.Kumbuka uhasama ulikuwa kati ya wahutu na watusi(haukuwa baina ya kanisa na watusi,sasa sijui logic ya kanisa kuua watu umetoa wapi au huwa mnasimuliwa na nani?)

Ukienda Rwanda au ukiuliza wakimbizi wengi kutoka Rwanda ambao wamekuja 1954 na wengine wa 1994 na kuendelea watakueleza hili vizuri.Babu yangu mzaa mama ni miongoni.Kama kuna padre alihusika kwenye hili,tambua alikuwa mhutu na ugomvi huu lazima ujue ulikuwa wahutu vs watusi(wanatajwa hadi Wafaransa kuhusika lakini hakukuwa na uhasama kati ya Ufaransa na raia wa Rwanda)
 
Duh!
 
Umeandika andiko linalojieleza. Tatizo la TEC kwa sasa ni Padri Kitima. Msipomtimua Kitima hapo, atalichafua Kanisa Katoliki. Kabla ya Padri Kitima kuwa Katibu wa TEC hatujawahi kuona matamko ya namna hii.
Ndio maana mlitaka kumuua kwa mtazamo huu?
 
Wewe ni mpotoshaji. Oktoba 29 hakuna mtu alitoka ili akapambane na vyombo vya dola kama ulivyosema.
 
Wewe sio Mkatoriki... nimekushtukia njoo kivingine unavyoandika tu nimekugundua wewe sio mkatoriki
Huyu ni tiss uchwara, hawa ndio waliokuwa wanasimamia wizi wa kura, sasa umma umekataa wanakuja na story za kutisha taasisi zinazotaka uwajibikaji.
 
Ona punga hili Samia hatumtambui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…