PostGE2025 Baraza la maaskofu Tanzania (TEC) mnatukosea sana wakatoliki

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hawa TEC huu ni utaratibu wao wa mambo ya kitaifa makubwa kuyatolea Maelezo . Sasa wakitoa huwa hawana upendeleo kwa sababu wanaamini wanahubiria na kuwatumza kiroho watu wa kaliba zote . Itanichukua muda Sana kufikiri haya unayosema.
 
Umeandika andiko linalojieleza. Tatizo la TEC kwa sasa ni Padri Kitima. Msipomtimua Kitima hapo, atalichafua Kanisa Katoliki. Kabla ya Padri Kitima kuwa Katibu wa TEC hatujawahi kuona matamko ya namna hii.
Dada choice variables punguza kuwashwa washwa!
 
Kwa hapa tulikofiks HAKUNA MAELEZO YANAYOTOSHA KUHALALISHA MAUAJI YALIYOTOKEA,
Unaongelea waandamanaji ni wezi na wahalifu vipi waliopigwa Risasi majumbani kwao????
Kanisa lina nafasi kubwa katika kushape watu.
Yesu Kristo aliye kiini cha ukristo alikemea waziwazi maovu na alidiriki kufanya reforms hekaluni alipoona inatumika ndivyo sivyo. Sasa huo ujumbe ni wa kwako sio mkatoliki
Roma Lucuta causa Finita
 
Kumtetea mtu mwenye akili kama yako inahitaji nguvu sana.
 
ww huna taarifa watu bado wanaendelea kutekwa

haki ya mungu watu kama ww mnatia hasira mpk mnafanya watu tufikirie kutafuta silaha kbs
 
Sisi tunataka kuwalipa mali zenu zote na kutengeneza miundombinu yote vipi nyie tunaomba mrudisheni ndugu zetu waliokufa.
miundo mbinu ni yetu sio yao , kikubwa wao walipe uhai wa watanganyika wenzetu
 
Umeandika sana alafu hamna point wew ni lile kundi linalo sema amani bila haki .

Wew kama unaona kazi ya kanisa ni kutoa huduma za kiroho hapana . Kanisa lina kemea maovu yote yanayo tendeka.
 
Mleta mada umeandika upuuzi mwingi. Bila shaka, wewe ni chawa wa watawala dhalimu au ni sehemu ya wauaji.

Kama ungekuwa na dhamira njema, na kama ungekuwa impartial, usingepoteza muda wako kuandika andiko hili la kipuuzi kiasi hiki, kwanza kabisa ungejikita kwenye chanzo cha tatizo. Ndiyo maana ukienda kwenye misingi ya haki, watu wawili mnaweza kufanya tendo moja lakini hukumu zake zikawa tofauti kabisa. Kwa mfano, jirani yako, akaiba mali yako, baadaye ukafanya uchunguzi ukagundua ni jirani yako ndiye aliyeiba, wewe ukatoka nyumbani kwako ukaenda kwa jirani yako umebeba upanga, ukavunja mlango wa nyumba ya huyo jirani yako, ulipomkuta ukampiga upanga, ukamwua; ni dhahiri hiyo ni murder case kwa sababu umepanga, ukanuwia, kisha ukatekeleza.
Tukio la pili, ulikuwa unaelekea shambani, umebeba panga lako, ukapita sehemu kwa wakala wa pesa ukachukua hela kwaajili ya mahitaji yako, kumbe kuna vibaka wanakufuatilia, mbele huko wakakuzunguka, mmoja akaja akakukaba shingo, nawe kwa vile una upanga mkononi, ukamkata na panga, akafa, wenzake wakakimbia, wewe hata ukifikishwa mahakamani, huna hatia, kwa sababu hukupanga kumwua mtu, hukuchukua panga kwaajili ya kwenda kumdhuru yeyote, umeua bila kukusudia wakati ukijitetea.

Vitendo vya watawala kuteka na kuua kila wasiyemtaka vimeanza lini? Vitendo vya kishetani vya watawala kudhulumu haki za wananchi kuanzia zile za kuishi, uhuru wa maoni mpaka demokrasia, vimeanza lini?

Wewe yumkini siyo muumini wa dini yoyote, labda ya mizimu. kwa sababu umeandika uwongo mwingi sana. Hakuna mahali popote ambapo serikali imeonesha vijana waandamanaji walikuwa na silaha. Kwa maelfu ya waandamanaji waliuawa na polisi na wale wahuni walioletwa toka Zanzibar, kama waandamanji walikuwa na silaha si wangetuonesha marundo ya silaha zilizotumiwa na marehemu? Wewe juha, ebu tuambie ni kituo gani cha polisi waandamanji walikivamia kisha wakachukua silaha? Hawa waandamanaji waliokuwa wanauawa hovyo na polisi, ulitaka wakikiona kituo cha wauaji, wakipakae rangi? Unaongelea waandamanaji kuua polisi, yawezekana ni kweli kuna polisi wachache sana wameuawa, lakini wakati polisi wakiua maelfu ya waandamaji, hao waandamanaji kama walipata uwezo wa kumkamata yeyote miongoni mwa hao polisi wauaji, ulitaka wamvishe taji la maua?

Umeonekana mpuuzi zaidi pale ulipoandika kuwa eti tamko la maaskofu linazungumzia siasa! Very stupid! Hivi unaelewa maana ya siasa?

Dini zote, iwe ni Ukristo au Uislam, zinasisitiza juu ya haki, kwa sababu, MUNGU WETU, NI MUNGU WA HAKI. Hii ina maana kila aliyemuumini wa kweli ni lazima atende haki, apiganie haki, na awe sauti ya kutetea haki kwa wale wasio na sauti. TEC na SHURA YA MAIMAMU, wametekeleza kikamilifu agizo hili la Mungu, na wameuishi utume wao kwa kukemea dhuluma.

Wewe endelea kuwa chawa wa wadhulumu haki, endelea kumtumikia shetani unayemwabudu, lakini wakatoliki wa kweli, waislam wa kweli, wanaofuata agizo la Mungu kuwa wanatakiwa kuuvaa ukweli wakati wote, hawataacha kuyasema yaliyo ya kweli.

Ukweli ulio dhahiri, chanzo cha yote mabaya yaliyotokea, ni watawala dhulumati. Watu wamevumilia, wamefikia ukomo, watawala wamefunga milango yote ya haki.

Waliouawa kwaajili ya kuitafuta haki, Mungu wa huruma awajalie heri mbinguni kwani wameshiriki utume wake wa kuitafuta haki kwaajili ya wengi.

Tunamwomba Mungu azidi kuwabariki watumishi wa Mungu wote, wa dini zote, wanaotembea katika kweli ya Mungu, wanaokemea dhuluma zinazofanywa na watawala kwa wananchi, sawa na walivyofanya manabii wa Mungu hapo kale. Wala msikatishwe na tamaa na mawakala wa shetani wanaohangaika kuidhoofisha sauti yenu inayotetea haki na kukemea dhuluma. Hawa watumishi wa shetani, watetea dhuluma, kama huyu mleta mada, lazima wataendelea kuwepo, wasiwavunje moyo, na hawa watetezi wa wauaji ni sehemu ya wauaji, tumwombe Mungu awape malipo sawasawa na dhamira zao zilizojaa uovu.
 
We jinga chawa mkubwa Mkatoliki fake
 
Listen bitch,,I support what I believe is working it doesn't mean we have to agree on everything...
 
Katoliki ni kanisa moja mkuu na kiongozi wenu ni mmoja tu Papa (Mungu duniani aka Mungu anayechaguliwa).
Nieleze kuhusu Katoliki kuhusishwa na mauaji ya kimbali huko Rwanda. Sababu ilikiuwa ni nini?
tupe ushahidi wa katoliki kuua watu Rwanda
 
kwamba wanaoua wapo sahihi ila wakosoaj ndo wana makosa , ila ccm ina watu wajinga sn
Kwetu mtu ambaye hajaoa hata kama ni mzee tunamwita mvulana.
Unajua huyu Mvulana Kitima ataliharibu kanisa katoliki liliojijengea umaarufu mkubwa Tanzania.
 
Upumbavu mtupu, hebu kale urojo kwenu huko..!!
 
Kuna tume ya kuchunguza kifo cha ally Kibao hivi ilikuja na ushauri au mapendekezo yoyote ambayo umma pamoja na.familia ya marehemu Ally Mohamed Kibao wanayajua au waliyasikia.

Tume zinapoundwa huwa ni.lugha ya kisiasa lakini hakuna jipya.

Tume ya jaji Othman Chande ilioangazia mfumo wa Haki jinai imewahi kusikika mapendekezo yake hadharani. Kuna umuhimu gani wa kutangaza kuunda tume ilihali haitaleta mabadiliko chanya ya kiutendaji si ni.ufujaji wa pesa za walipakodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…