Baraza la Mawaziri 2020 Halina Ukanda, Udini wala Ukabila!

Baraza la Mawaziri 2020 Halina Ukanda, Udini wala Ukabila!

Biteko siyo Shinyanga ni wa Geita
Kwandikwa -shinyanga
Katambi -shinyanga
Biteko- shinyanga
Mashimba- simiyu
Kalemani -Geita
Mabula-Mwanza
Bashungwa- kagera
Waitara-Mara
 
you miss a point dude, " CHADEMA" inataka utawala wa majimbo na si ukanda kama wewe akili zako matope unavyodhani, MAJIMBO nchi za wenzetu imewaletea maendeleo lakini UKABILA umeleta sjhida kwenye CCM.

Usitake kujificha kwenye ukanda na ukabila kuizodoa CHADEMA badala ya CCM iliyoongoza toka uhuru na hakuna kitu imefanya zaifi yakumfanya mtanzania kuwa maskini zaidi
Hakuna CCM imefanya ? Uko serious kweli wewe ? Bila CCM ungekuja hapa kuandika uharo huu ?
 
Mimi naona hao kanda ya ziwa ndio wamesoma sana na CV zao zinawabeba na hata ukiangalia matokeo yao shule za huko zinafaulisha sana, wanastahili.

Hivi unaweza mpa BABU TALE Uwaziri?

Ndio si mbunge wa ccm aliyepita bila kupingwa hivyo anastahili!!! Ccm oyeeee!
 
lengo kuu la hii wizara mpya ni kudhibiti tu habari za wakosoaji mitandaoni...hawana jipya
 
Mh Magufuli kateua baraza la mwaziri, 05-12-2020 mida ya jioni kama alivyotabiri kigogo2014 lakini watu wamelipa kisogo na habari za simba na Plateau zimevuma kuliko Baraza Lenyewe.

Je, watanzania wamechoka na kuona hakuna jipya au?

1. Maji -Juma Aweso
2.Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo- Innocent Bashungwa
3.ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu Jenister Mhagama
4.Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii,jinsia na watoto Doroth Gwajima (Mbunge mpya alikuwa naibu nkatibu mkuu)
5.Wizara anayesimamia Uwekezaji ofisi ya Rais Mkumbo Kitilya
6.Wizara ya Katiba na sheria Mwigulu Nchemba
7.Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako
8.Mifugo na Uvuvi - Mashimba Mashauri Ndaki
9.Maliasili na Utalii DK Ndumbalo Damas
10.Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo
11.Madini Dotto Biteko
12.Nishati Dkt Medard Kalemani
13.Ujenzi na Uchukuzi mbunge mpya Mhandisi Dkt Leonard Chamuliho (alikuwa Katibu Mkuu Uchukuzi)
14.Kilimo Prof.Adolph Mkenda.
15.Viwanda na Biashara Mwambie Geofrey Idelphonce
16.Mambo ya ndani George Simbachawene
17.Muungano na MAZINGIRA Ummy Mwalimu
18.Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari Dkt Faustine Ndugulile
19.Fedha Dkt Philip Mpango
20.Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Paramagamba Kabudi
21 Ardhi-William Lukuvi
22.Ulinzi na JKT Elias John Kuandikwa
23.Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Capt Mstaafu George Mkuchika


MANAIBU WAZIRI:
1.Viwanda na Biashara-Kigahe Exaud Silaoneka
2.Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi-Dkt.Angelina Mabula
3.Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, Vijana na Ajira-Katambi Pascal Patrobas
4.Mambo ya ndani ya nchi-Hamis Hamza Hamis
5.Fedha na Mipango-Mwanaidi Ali Hamis
6.Elimu Sayansi na Teknolojia-Kipanga Juma Omary
7.Ofisi ya Rais TAMISEMI-Dkt Festo John Lugange
8.Nishati-Byabato Stephen Mjwahuka
9.Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala bora- Ndejembi Deogratias John
10.Mawasiliano na Telnolojia ya habari-Mhandisi Kundo Andrea Mathew
11.Mifugo na Uvuvi- Gekul Pauline Philipo
12.Madini-Ndulane Francis Kumba
13.Ujenzi -Mhandisi Msongwe Godfrey Kasekenya
14.Ofisi ya Waziri mkuu wenye Ulemavu-Ummy Hamis Nderiananga @⁨Ummy Ndeliananga⁩
15.Maji-Mhandisi Maryprisca Wilfred Mahundi
16..Habari, Umaduni,Sanaa na Michezo-Abdalah Ulega
17.TAMISEMI Silinde David Ernest
18.Kilimo-Husein M.Bashe
19.Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na watoto Dkt Godwin Molel ⁩
20.Katiba na Sheria Pinda Geofrey Mizengo
21.Muungano na Mazingira-Mwita Waitara
22.Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki-William Tate Ole Nasha
23.Maliasili na Utalii - Mary Francis Masanja


KANDA YA ZIWA -MAWAZIRI
Kutoka kanda ya ziwa wapo mawaziri 10 kati ya 23 Tanzania nzima, hapa HAKUNA UKANDA.

MANAIBU:-
wachache sana , ha ha ha

DINI:
Nchi yetu si ya udini na si vyema kuzungumzia maana kila mtu ana dini yake.
Kuna akina John lakini waislamu na Ramadhani lakini mkristo kama alivyokuwa jaji agustino ramadhani
Vipi kuna waziri kutoka unguja??
 
Mie Kyusa, kwa muda mrefu hatujawahi kukosa uwakilishi toka kanda ya myanda za juu, hasa Njombe, Songea, Iringa na Mbeya.
Kanda hii ya The Big Four, breadbasket ya Tanzania in umuhimu wake.

Lukuvi, silinde, ndumbaro hao wanatokea wapi?
 
Kulikua na wagombea wengi wasomi, kwani kulikua na ulazima wa kpitisha jina la babu tale kugombea ubunge?

Nadhani hii sheria ya kusema mbunge awe anajua kusoma na kuandika ifutiliwe mbali ili kuwe na usawa au ueiano wa viwango vya elimu baina ya wagombea, sasa imagine PhD holder analipwa mshahara sawa na la saba b, kisa wote ni wabunge, atlist wangesema sifa ya kugombea kiwango cha elimu kisiwe chini ya degree

Anyway, ngoja tuamini kwamba kanda ya ziwa ndio wana elimu kubwa na CV nzuri, na pia tuamini kwamba cv zao na elimu yao itaifikisha nchi sehemu nzuri by 2025[emoji41]
Una hoja, lkn pia una viroja.

Unaona sio haki Phd holder kulipwa mshahara sawa na std 7 bungeni,.. kwani hiyo Phd ni ya ubunge!?

Kama mtu anataka 'atazamwe zaidi' kwa sababu ya vyeti vyake si abaki tu kwenye taaluma yake!
 
Mle mle
 

Attachments

  • Screenshot_20200518_071225.jpg
    Screenshot_20200518_071225.jpg
    78.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom