Baraza la Mawaziri 2020 linamuhitaji Dr Slaa, karibu Kawe Dr wa ukweli

Halima Mdee hakuna wa kumtoa kawe,kawe ina watu wwnye uchumi wa kati wapenda mabadiliko ya nchi wenye upeo kielimu kiasi hivyo mwana ccm asijaribu kupoteza pesa zake bure kwa hongo ya wapiga kura
 
Labda chadema, CCM Kuna vijana wengi wenye maono na uthubutu, Slaa ameshakua Kikongwe! WEWE subiria kikosi cha 2020!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda viti maalum, hapo sawa maana hata uenyekiti bawacha aligombea na kivuli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingefaa sana Dr. Slaa kuwa Chief Secretary kwa awamu ya pili ya Mh. Rais Magufuli, si kwamba aliyepo haifai lakini ni kwa sababu anahitaji kupokewa kijiti.. Dr. Slaa anajua kufanya homework yake vizuri pasina kubakiza kitu, tathmini fupi ya jumla ni kwamba kuna tatizo kwenye utumishi wa Umma, mfano mdogo fomu za tume ya maadili hazijajazwa na watumishi wengi mpaka leo bado siku 2, lakini hata ile panga pangua ya kila Mara kwa nafasi mbali mbali ni Ushahidi kuwa vetting haifanywi vizuri ili Rais achague mtu sahihi.. Mara zote ninashangaa kila kwenye sherehe ya kiapo kwa wateuliwa, Chief Secretary ambaye ndiye msimamizi wa hao wanaoapishwa huwa kama hajisikii kuongea ili kukumbusha uadilifu, tija, nk Rais ndio huwa analazimika kuongea yale ambayo CS alipaswa aongee.. Inawezekana si muongeaji lakini nafasi aliyo nayo inamtaka awe anaongea tena sana hasa kwa zama hizi.. Ningependa sana asaidiwe kazi hii alipofanya panatosha, awamu ya pili tunahitaji Rais aweke msingi wa kuwa na watendaji mathubuti kwa ajili ya awamu inayofuata pia aweke mfumo bora wa kupata watendaji na kuwasimamia hata kupima utendaji wao, anayeweza kufanya jukumu hili ni Dr. Slaa!!!
 
Bwashee ni wapi hapa duniani sanduku la kura linatenda haki?!
 
..Natamani apewe Wizara ya mambo ya ndani ili awabamize wapinzani.
 

..wakuu wa mikoa na wilaya vijana wenye mihemko ya kichama ndiyo wanaosababisha migogoro na wabunge wa upinzani.

..eneo lenye wabunge wengi wa upinzani panahitajika wakuu wa mikoa na wilaya watu wazima wenye busara na waliokomaa kiuongozi.

.
 
Naunga mkono hoja
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili kubwa miaka 58 ya uhuru watu wanakunywa maji ya vidimbwi na fisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…