Baraza la Mawaziri la serikali ya Tanzania limepokea taarifa ya awali ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022

Baraza la Mawaziri la serikali ya Tanzania limepokea taarifa ya awali ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022

Mgombea nadhani alikuwa Lowasa aliahidi kuunda wizara ya kushughulikia mkoa wa DSM pekee nadhani alijua kwa idadi ya watu kufikia milioni 5 mahali pengine ni nchi hiyo lazima iwe na uangalizi wa karibu kwa changamoto kibao ikiwemo hii ya maji, msongamano, masoko,uwekezaji.
Basi tu ishakuwa .
 
watu tuna mwezi hatujaona maji bombani afu kumbe nyie ni siku 6tu ........mie nasubir bill ya dawasco ya oct hawakawii kukubambikizia
 
Juzi hapo Dar kwenye uzinduzi wa visima amesema mnapata maji kwa 94% na mataga wakashangilia mnoo na Mrisho Mpoto akasainiwa cheki(sio chini ya million 10 alikua na bendi) akaimba mashairi ya kumpongeza rais kwa kutatua shida ya maji hapo Dar.
 
“Nitoe wito kwa mamlaka zote za maji kuhakikisha zinafanya masahihisho kwenye taarifa zenye mapungufu ili ziweze kutoa hali halisi ambayo mwisho wa siku itasaidia katika kupima utendaji na ufanisi wa huduma wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira” amefafanua Mhandisi Lumato' EWURA yazitaka mamlaka za maji nchini kutoa taarifa sahihi za huduma ya maji na usafi wa mazingira
5E3D7EC3-7EDB-4803-83FF-76BE158E2FEC.jpeg
 
Eneo ninalokaa tuna zaidi ya siku sita bila kuona tone la maji kwenye mabomba. Fikiria vyoo vya ndani bila maji hali inakuwaje. Kinachosikitisha zaidi ni viongozi wetu wako busy na siasa kama vile hili sio janga linalohitaji dharura. Kitakachofuata ni mlipuko wa magonjwa.

Nashauri baraza la mawaziri likae na lije na suruhisho, huo ndio uongozi badala ya kuzunguka mitaani na ma v8 yenu ndani ya viyoyozi mkisifiana.
Nilikuwa na mpango wa kuhamia Dar lakini naona Kama ni Bora nihamie Arumeru nikachimbie likisima lirefuuu
 
Baraza la Mawaziri nchini Tanzania, limeagiza wataalamu wa ndani kushirikiana na wataalamu kutoka nje ya nchi katika kufanya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022 na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 24 wakinusurika.

Hayo yamesemwa hii leo Novemba 14, 2022 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa mara baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, na kuongeza kuwa Baraza hilo limetoa maagizo ili kupata chanzo cha ajali na mapendekezo.
EA1B4A17-7DFB-430D-9E29-909B14C03FE6.jpeg

Amesema, “Baraza la Mawaziri limewaelekeza wataalamu wa ndani kushirikiana na wataalamu kutoka nje ya nchi katika kufanya uchunguzi wa ajali hii na pia kupata chanzo cha ajali pamoja na mapendekezo ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa mara baada ya ajali kutokea.”

Msigwa amesema Baraza hilo pia limeelekeza vitengo vinavyohusika na kukabiliana na majanga viimarishwe mambo mbalimbali ambayo yatatuwezesha kama nchi kuongeza uwezo zaidi ya uliopo katika kukabiliana na majanga yanapotokea.
6D1C90C5-A418-43C3-92B5-DD57CA7E5172.jpeg

Msigwa, amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na timu ya uchunguzi itakayofanya kazi na kutoa maelezo ndani ya siku 14, ikifuatiwa na ripoti ya awali itakayotolewa ndani ya siku 30 na kisha ripoti kamili ambayo inatolewa ndani ya miezi 12.

Ndege hiyo ilianguka katika Ziwa Victoria takribani mita 100 kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba, mkoani Kagera ikiwa na watu 43 waliokuwa wakitoka jijini Dar es Salaam, 39 wakiwa abiria, marubani wawili na wahudumu wawili ambapo shughuli za uokoaji kwa sehemu kubwa zilifanywa na wavuvi wakiongozwa na kijana Jackson Majaliwa na wenzake waliowezesha watu 24 kuokolewa.
A3AADD60-1917-4DEE-9EE6-21D3F7ECFFCF.png
 
ccm wanategemea mungu kuvusha yote ila ukweli wanategemea vyombo vya dora kukupoteza na ubakaji wa uhuru
 
Upuuzi mtupu! Ajali ya ndege kuzungumziwa baraza la mawaziri?? Kama hii ndio standard mbona vifo vitokanavyo na ajali barabarani havifiki baraza la mawaziri??

Hili jambo sasa linachukuliwa kama kiki! Watu wanapata airtime ya kusifiana!

Wazungumzie umeme, ajira, mfumuko wa bei! Hayo ndio mambo muhimu kwa taifa! Watumie muda kujadili na kufanyia kazi mambo yanayohusu taifa hili na linakoelekea! Sitaki kuonekana nina roho ngumu, lakini wajishighulishe na mambo muhimu yanayohusu walio wengi na kesho ya nchi hii!! Ni bora wangezungumzia janga la ebola ambalo liko nchi jirani!!
 
Baraza la Mawaziri la serikali ya Tanzania limepokea taarifa ya awali ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022, Bukoba mkoani Kagera na kugharimu maisha ya watu 19.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Novemba 14, 2022, jijini Dodoma na Msemaji Mkuu wa serikali kufuatia maelekezo ya Baraza la Mawaziri lililoketi hii leo na Rais Samia Ikulu ya Chamwino.

"Leo kikao cha Baraza la Mawaziri kikiongozwa na Rais Samia kimekutana hapa Dodoma, na Baraza la Mawaziri limepokea taarifa ya awali ya ajali ya Ndege ya Precision Air na hatua zilizochukuliwa baada ya ajali," amesema Msigwa

Aidha Msemaji ameongeza kuwa "Baraza la Mawaziti limewaelekeza wataalam wa ndani kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi katika kufanya uchunguzi na kupata chanzo cha ajali pamoja na kupata mapendekezo ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa mara baada ya ajali kutokea,".

Baraza la Mawaziri pia limeelekeza kwamba vitengo vyote vinavyohusika na kukabiliana na majanga nchini viimarishwe ili kuongeza uwezo zaidi wa kukabiliana na majanga yanapotokea.

Chanzo: EATV
Upuuzi mtupu
 
Upuuzi mtupu! Ajali ya ndege kuzungumziwa baraza la mawaziri?? Kama hii ndio standard mbona vifo vitokavanavyo na ajali barabarani havifiki baraza la mawaziri??

Hili jambo sasa linachukuliwa kama kiki! Watu wanapata airtime ya kusifiana!

Wazungumzie umeme, ajira, mfumuko wa bei! Hayo ndio mambo muhimu kwa taifa! Watumie muda kujadili na kufanyia kazi mambo yanayohusu taifa hili na linakoelekea! Sitaki kuonekana nina roho ngumu, lakini wajishighulishe na mambo muhimu yanayohusu walio wengi na kesho ya nchi hii!! Ni bora wangezungumzia janga la ebola ambalo liko nchi jirani!!
Viongozi vipofu ingawa wana macho. Inasikitisha sana.
 
Baraza la Mawaziri la serikali ya Tanzania limepokea taarifa ya awali ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022, Bukoba mkoani Kagera na kugharimu maisha ya watu 19.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Novemba 14, 2022, jijini Dodoma na Msemaji Mkuu wa serikali kufuatia maelekezo ya Baraza la Mawaziri lililoketi hii leo na Rais Samia Ikulu ya Chamwino.

"Leo kikao cha Baraza la Mawaziri kikiongozwa na Rais Samia kimekutana hapa Dodoma, na Baraza la Mawaziri limepokea taarifa ya awali ya ajali ya Ndege ya Precision Air na hatua zilizochukuliwa baada ya ajali," amesema Msigwa

Aidha Msemaji ameongeza kuwa "Baraza la Mawaziri limewaelekeza wataalam wa ndani kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi katika kufanya uchunguzi na kupata chanzo cha ajali pamoja na kupata mapendekezo ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa mara baada ya ajali kutokea,".

Baraza la Mawaziri pia limeelekeza kwamba vitengo vyote vinavyohusika na kukabiliana na majanga nchini viimarishwe ili kuongeza uwezo zaidi wa kukabiliana na majanga yanapotokea.

Chanzo: EATV
Kwa hiyo miaka yote hiyo vikosi havina vifaa vya kutosha kukabiliana na majanga?.
 
Walivyo kaa unaweza kufukiri wanapanga cha maana kumbe in utumbo tu.Ajali hata ikitokea tena zaidi wataokolewa na watu wa kawaida ambao hawana mafunzo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, ni aibu sana kwa watu wana kipaza sauti na vifaa lakini wanampa maelekezo mtu asiyekuwa na ufahamu wala vifaa. Kikosi husika hakikuwa na uwezo wa kutaka kuokoa maisha ya wengine wengi na kupoteza angalau mmoja wapo, waokozi hawa ni watu wasiojali kazi yao isipokuwa mishahara. Kama majaliwa angekufa pia, bila aibu wao ndio wangejiita waokozi.
 
Ni hili tu wameliona?
Umeme Maji mfumuko wa bei hawavioni?
Mkoloni arudi tu
 
Back
Top Bottom