Katika mtandao wa
Facebook ipo
taarifa inayosambazwa kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) lina watangazia wazazi na walezi utaratibu wa marekebisho majina ya watoto walio sajiliwa kimakosa kwenye mifumo ya usajili wanafunzi kielektroniki yani PREM kwa shule za msingi na PREMS kwa shule za sekondari ambapo Mzazi au mlezi ana hitajika kuwa na Cheti cha kuzaliwa mtoto, Namba ya usajili mtoto PReM/PREMS Namba ya NIDA ya mzazi au mlezi na kwamba vielelezo hivyo vinahitajika kutumwa kwa njia ya WhatsApp: +255 621 741 590.
Aidha taarifa hiyo inabainisha gharama za marekebisho kuwa ni Tsh. 48,950/= na gharama za kufanya mabadiliko ni Tsh. 55,850/= mwisho wa zoezi hilo ukitajwa kuwa ni tarehe 24 Oktoba, 2025.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani haijatolewa na Baraza la mitihani Tanzania (
NECTA)
Aidha alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo Afisa Habari na Uhusiano wa NECTA, John Nchimbi amethibitisha kuwa haijatolewa na baraza hilo bali imetengenezwa na wapotoshaji.
Aidha
Septemba 30, 2025 NECTA ilikanusha taarifa ya Agosti 18, 2025 ambayo inafanana na taarifa hiyo ambayo inathibitika kuwa imeghushiwa na wapotoshaji wenye nia ovu kwani Baraza hilo halitumii mawasiliano binafsi kuwasilisha maombi hayo.
Baraza la Mitihani la Tanzania hushughulikia maombi ya marekebisho ya majina ya watahiniwa yaliyokosewa kuandikwa katika mitihani ya Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu ambapo maombi hayo hufanyika kwa njia ya mtandao huku malipo malipo yakifanyika kwa namba maalum (Control number) inayotolewa kupitia tovuti ya NECTA.