Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), naomba majibu ya maswali haya...

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
1. Jamii ya watanzania haipendi kujisomea.

2. Wanafunzi wa Tanzania hasa O level hawawezi kujisomea bila usimamizi wa mwalimu.

3. Familia nyingi Tanzania hazina uwezo wa kuwanunulia watoto vitabu ili wajisomee nyumbani.

4. Shule pia hazina vitabu kabisa vya kutosha.

5. Shule zilifungwa muda mrefu Sana mwaka Jana kwasababu ya Corona.

6. Mikusanyiko na tuition zote mitaani zilipigwa ban. Hii ilimaanisha wanafunzi waliokuwa likizo ndefu hawakujisomea pamoja.

7. Hii maana yake mwaka Jana wanafunzi walikaa darasani muda mfupi.

SWALI LANGU:
Huu ufaulu mkubwa hivi ambao unauzidi wa mwaka 2019 ni halali? Haujapikwa? Hamjapanua goli?

Je, mnataka kutuaminisha kwamba wanafunzi watoro shuleni ndio wanaopaswa kufaulu?

Yani mimi nikae darasani mwaka mzima nikimsikiliza mwalimu na kufanya mapraktiko kila siku nije nipitwe na mwanafunzi mtoro aliekaa nyumbani miezi minne?

NECTA naomba ufafanuzi wa maajabu haya katika elimu ya Tanzania.
 
Unajua kwenye mizania ya logic haiwezekani.
 
Kuna jamaa yangu yuko necta anasema kilichofanyika baraza sawa sawa NEC walichokifanya kwenye uchaguzi wa 2020,Mungu ndie anaejua tunakoelekea na hii elimu yetu.
 
Aisee imaumiza sana bora wachezee siasa Moto wake watauzima kwa risasi Sasa wakichezea elimu yetu doooh
 
Kila mtu na kichwa chake na sio kila mtu hajisomei mwenyewe.

Na shule hakuna kigumu cha kukufanya ukeshe ukisoma usiku kucha plus tuition ili ujibu mtihani mmoja mdogo wa maswali 50 labda kama unakariri.

Considering wengi hawajui hata kwanini wanasoma hivyo huishia kukariri mimi sijawahi kukanyaga tuition na wala sisomi usiku na hakuna anayenipita popote hivyo tuition ni sawa na kupoteza muda na wasiojua kwanini wanasoma maybe na wanaokariri.

So tuition sio sababu ya ufaulu kuongezeka au kupungua.

Na bila shaka mitihani imetungwa kutokana na kipindi hichohicho walichosoma muda mchache na si vinginevyo so it make sense ufaulu kuongezeka kama hivyo kungekuwa hakuna wanaopata zero.
 
1. Jamii ya watanzania haipendi kujisomea.

2. Wanafunzi wa Tanzania hasa O level hawawezi kujisomea bila usimamizi wa mwalimu.

3. Familia nyingi Tanzania hazina uwezo wa kuwanunulia watoto vitabu ili wajisomee nyumbani.

4. Shule pia hazina vitabu kabisa vya kutosha.

5. Shule zilifungwa muda mrefu Sana mwaka Jana kwasababu ya Corona.

6. Mikusanyiko na tuition zote mitaani zilipigwa ban. Hii ilimaanisha wanafunzi waliokuwa likizo ndefu hawakujisomea pamoja.

7. Hii maana yake mwaka Jana wanafunzi walikaa darasani muda mfupi.

SWALI LANGU:
Huu ufaulu mkubwa hivi ambao unauzidi wa mwaka 2019 ni halali? Haujapikwa? Hamjapanua goli?

Je, mnataka kutuaminisha kwamba wanafunzi watoro shuleni ndio wanaopaswa kufaulu?

Yani mimi nikae darasani mwaka mzima nikimsikiliza mwalimu na kufanya mapraktiko kila siku nije nipitwe na mwanafunzi mtoro aliekaa nyumbani miezi minne?

NECTA naomba ufafanuzi wa maajabu haya katika elimu ya Tanzania.
Sijawahi kuwa na imani na mtendaji mkuu wa NECTA tangu alipo re-standardize matokeo aliyokataa ku re-standardize Ndalichako enzi za Mkwere, halafu mwaka uliofuata akaja na uongo akasema BRN.
 
Sijawahi kua na imani na serikali ya mitano tena.
 
Nilivyoona tu NECTA wamekanusha yale matokeo ya Shule za Mtwara kushika top ten mkiani, nikakata tamaa na system nzima ya matokeo mwaka husika....
 
Back
Top Bottom