ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Naona watakuwa wanapekua vitabu vyao vya sheria ukurasa wa kwanza hadi mwisho....wanarudia rudia kuona anaangukia kwenye kosa lipi.....Hamna kesi.Labda watunge
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona watakuwa wanapekua vitabu vyao vya sheria ukurasa wa kwanza hadi mwisho....wanarudia rudia kuona anaangukia kwenye kosa lipi.....Hamna kesi.Labda watunge
Hahahahaaa ni shidaNisaidie kushangaa. Yaani kwa vile ni msanii basi akifanya kosa hata kama halihusiani na sanaa basi wao ni kufungia tu! Kama kuna jinai si polisi na mahakama zipo. Au mie ndo sielewi na akili zangu za usiku?😴
Duh.Hao jamaa ni very hopelessly
KudadadekBasata wasivyo na aibu wanaweza wakamsitishia na hilo pia. Wakasema wao ndiyo watoa leseni kwa watu wanaotaka kujiajiri kwenye kuchamba wenzao
Kuna mchangiaji kasema alishamvunja kiuno Mr. Nice hivi kweli? Dudu baya halafu wanasema ni bisexual.Tanzania bwana,sasa wanamfungia kafanya kosa gani?
Unaweza unaenda kuomba judicial review na jamaa akiende anatoka vizuri tuHivi kwa nini ukifungiwa na BASATA hamna kukata rufaa au hao Basata ni malaika maamuzi yao yapo sawa kila wakati hayatakiwi kupingwa.Sasa Dudu kisheria hana kosa ,ila kimaadili sawa sasa kwa nini unamfungia kavunja sheria gani ya BASATA.Ila aisee hii nchi yetu hii mihemko mingi sana.
Unaweza tuhumiwa na Polisi ila ukawa umefanya kosa kwenye mamlaka husika..mfano sianond alifungiwa na basata lakini hatushtakiwa na polisi.
Nimeona tamko, na ningependa kufanya comment mstari baada ya msitari kama ifutavyo:
Mosi, BASATA wanasema:
View attachment 1034718
Aya hii ni taarifa, na haina lolote la kujadili kwani mamlaka hayo yako ndani ya uwezo wa kisheria wa BASATA.
Pili, BASATA wanasema:
View attachment 1034719
Hapa kuna kuna tatizo. Kukamatwa na Jeshi la Polisi ni kutuhumiwa. Kutuhumiwa sio kuhukumuiwa. Katiba ya nchi inasema kila mtu anayo haki ya kuhesabiwa mwenye haki mpaka mahakama inapomtia hatiani. Dudubaya hajatiwa hatiani na mahakama. Kwa hiyo, uamuzi wa BASATA unaweza, na unapaswa kufanyika, baada ya hukumu ya mahakama na sio kabla yake. Kwa hiyo, aya hii inamaanisha kuwa BASATA wamefanya maamuzi yanayokiuka Katiba ya nchi.
Tatu, BASATA wanasema:
View attachment 1034720
Aya hii inaendeleza kosa lililofanyika aya ya hapo juu. Kwamba Dudubaya ni "raia mwema" au kinyume chake ni suala la kuamuliwa na mahakama na sio vingnevyo. BASATA walipaswa kusbiri maamuzi ya mahakama ili wachukue hatua hii. Lakini wameitangulia mahakama. Wamekosea.
Na nne, BASATA wanasema,
View attachment 1034721
Aya hii imekaa kiswahili kweli kweli. Kwamba kuna Watanzania wengi "waliojitokeza kukemea kitendo cha Msanii Dudubaya" kwa sababu wanaona "hakifai," haimaanishi kwamba mahakama imetoa hukumu ya kisheria. Kisheria tunasema "plausibility does not imply validity." Kwa hiyo, BASATA wametumia sheria za mitaani kana kwamba ni sheria za kimahakama. Wamekosea.
Hivyo, naona kwamba, BASATA wanaendeleza utamaduni mpya wa baadhi ya vyombo vya serikali "kufanya kazi kwa mujibu wa matamko ya wakubwa" badala ya kuangalia sheria inasema nini. Utamaduni huu haukubaliki kwa Watanzania wanaojua na kuheshimu kanuni za utawala bora.
Kanuni moja ya utawala bora ni kanuni ya usawa mbele ya sheria.
Yaani, "the same law should apply to like persons in like circumstances."
BASATA wamezingatia kigezo hiki ? Hapana
Na bahati nzuri ni kwamba, Waziri wa Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe, ni Mwanasheria Nguli. Nimesoma PHD Thesis yake yote. Yuko safi kichwani. Pia ni mlokole mzuri. Wengi tuliona alivyousindikiza mwili wa hayati Samwel Sitta kwa mbwembwe tosha za machozi ya Kilokole. Tunataka imani yenye vibwagizo vya matendo.
Ama sivyo, tutahitimisha kwamba ulokole ule ulikuwa ni usanii, na usanii sio taji lenye heshima kwa mtu mwenye umri kama wa Dr. Harrison Mwakyemba.
Mama Amon.
serikali ina viongozi wajinga sana hii! kwani ruge ndio nani hadi akidhihakiwa ipelekee ku end someone's career!? ujinga mtupu umewajaa viongozi wa nchi hii hasa yule jamaa wa BASATA anaitwa Mungereza nahisi hana ubongo hua anafikiri kwa kutumia bandama.
kwani kishatoka jela?Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kusitisha usajili wa Msanii Godfrey Tumaini (Dudubaya) kuanzia leo tarehe 28/02/2019.
Faida na hasara yake ni nini.
Alitukana tusi gani?Chukulia wewe baba yako kafa, harafu Kuna fala anatokea na kuanza kuitukana maiti ya baba yako, we ungemchukulia hatua gani, nahisi ungeenda kumfanya chochote ili ulidhike, sasa serikali kuona hivyo ndo ikaona umuhifadhi ili asidhurike
Sent using Jamii Forums mobile app