Baraza la sanaa(BASATA) lasitisha usajili wa Msanii Dudubaya

Sheria zote duniani zinalazimika kufuata na kuzingatia misingi ya 'Haki Asili za binadamu' (Principles of Natural Justice), moja ya misingi mikubwa ya sheria hizi ni haki ya kusikilizwa.

Haupaswi na hauwezi kutoa hukumu ya upande mmoja tu, ni lazima uusikilize na upande mwingine, ni lazima usikilize nini chanzo vile vile.

Basata wameendeleza kuhamua mambo kwa hisia tu pasipo kufuata sheria, kwakua wana uwezo wa kumfutia mtu leseni basi hawaangalii huo utaratibu wao wanajifutia tu, hii sio haki na hapa lazima lifanyike jambo kukomesha upuuzi huu.

Hakuna sheria inayotambua mambo ya hisia, mtu kuumiza hisia zako sio kosa kisheria, dudubaya kaumiza hisia za basata na hili sio kosa la kisheria.
 
Nisaidie kushangaa. Yaani kwa vile ni msanii basi akifanya kosa hata kama halihusiani na sanaa basi wao ni kufungia tu! Kama kuna jinai si polisi na mahakama zipo. Au mie ndo sielewi na akili zangu za usiku?😴
Hahahahaaa ni shida
 
Siku atakayo kufa mpinzani wa kisiasa, wa vyama vya upinzani atakejeriwa, kutukanwa na kuundiwa vikatuni na watakaofanya hivyo watasifiwa hata kupewa nishani.
Hii ndiyo nchi yangu iliyotekwa, na wanasiasa kila nyanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kusitisha usajili wa Msanii Godfrey Tumaini (Dudubaya) kuanzia leo tarehe 28/02/2019.

Faida na hasara yake ni nini.
 
Unaweza unaenda kuomba judicial review na jamaa akiende anatoka vizuri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza tuhumiwa na Polisi ila ukawa umefanya kosa kwenye mamlaka husika..mfano sianond alifungiwa na basata lakini hatushtakiwa na polisi
 
Ni upuuzi kulazimishwa kufikiri sawa nchi nzima. Rais alitweet kuhuzunishwa na kifo cha Ruge, Lakini dudubaya yeye hakuona huzuni,bali akaona ndio muda wa yeye kutoa nyongo yake dhidi ya Marehemu. Hilo likawaudhi Serikali ya CCM kwa sababu aliyefariki ni wa kwao.
Kila mtu anakichwa chake na kila mtu yuko huru kufikiria na kusema akili yake inachoona kinafaa kusemwa hata kama hakiwapendezi. Uhuru wa mawazo uko wapi? Hao BASATA wamefuata kanuni na sharia gani au ndio wametumwa na Mwakyembe wamfungie?! Mwakyembe katumwa na mkubwa, nchi hii ni yetu sote jamani achene ubaguzi wa kifikra.
 
serikali ina viongozi wajinga sana hii! kwani ruge ndio nani hadi akidhihakiwa ipelekee ku end someone's career!? ujinga mtupu umewajaa viongozi wa nchi hii hasa yule jamaa wa BASATA anaitwa Mungereza nahisi hana ubongo hua anafikiri kwa kutumia bandama.
 
Dudubaya kaja na stail mpya[emoji38]
Kaona akitukana au akitoa kashfa mitandaoni eti ndio anapata jina[emoji38]
Alijua na hii nayo atapata jina kam ileee,!!!ishu ya mashoga[emoji38]
Duh,!!!kapewa Ban ya Nguvu[emoji38]na hivi hana hata hela ya chips[emoji38]huyo ndio Buriani naaga masela[emoji1321]‍♂️
 
Chukulia wewe baba yako kafa, harafu Kuna fala anatokea na kuanza kuitukana maiti ya baba yako, we ungemchukulia hatua gani, nahisi ungeenda kumfanya chochote ili ulidhike, sasa serikali kuona hivyo ndo ikaona umuhifadhi ili asidhurike
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kusitisha usajili wa Msanii Godfrey Tumaini (Dudubaya) kuanzia leo tarehe 28/02/2019.

Faida na hasara yake ni nini.
kwani kishatoka jela?
 
Alitukana tusi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…