Baraza la sanaa(BASATA) lasitisha usajili wa Msanii Dudubaya

Huo ni mwanzo tu nadhani mpaka j3 watampandisha kizimbani sasa hivi watakuwa wanatafuta kesi ya kumpa
Kwa jinsi niijuavyo Tanzania,mpaka sasa unaweza kuta tayari ana kesi zaidi hata ya 10 za kujibu,ndipo unajiuliza zimetokea wapi na kavunja sheria gani.
 
Primary court magistrate Act inamkataza mtu yeyote kutoa matusi hadharani hivyo apelekwe mahakani akajibu shtaka la kutoa matusi.
dfg.PNG
 
U
Kama wapo sahihi, ni busara, mara nyingi, kuwaheshimu watu wenye "power". Wana athari kwa kiasi kikubwa kwenye mustakabali wa maisha yako.
Umenena kama mtu mwenye hekima ya juu zaidi kushinda yote.
 
.
Nimeona tamko, na ningependa kufanya comment mstari baada ya msitari kama ifutavyo:

Mosi, BASATA wanasema:
View attachment 1034718

Aya hii ni taarifa, na haina lolote la kujadili kwani mamlaka hayo yako ndani ya uwezo wa kisheria wa BASATA.

Pili, BASATA wanasema:

View attachment 1034719

Hapa kuna kuna tatizo. Kukamatwa na Jeshi la Polisi ni kutuhumiwa. Kutuhumiwa sio kuhukumuiwa. Katiba ya nchi inasema kila mtu anayo haki ya kuhesabiwa mwenye haki mpaka mahakama inapomtia hatiani. Dudubaya hajatiwa hatiani na mahakama. Kwa hiyo, uamuzi wa BASATA unaweza, na unapaswa kufanyika, baada ya hukumu ya mahakama na sio kabla yake. Kwa hiyo, aya hii inamaanisha kuwa BASATA wamefanya maamuzi yanayokiuka Katiba ya nchi.

Tatu, BASATA wanasema:

View attachment 1034720
Aya hii inaendeleza kosa lililofanyika aya ya hapo juu. Kwamba Dudubaya ni "raia mwema" au kinyume chake ni suala la kuamuliwa na mahakama na sio vingnevyo. BASATA walipaswa kusbiri maamuzi ya mahakama ili wachukue hatua hii. Lakini wameitangulia mahakama. Wamekosea.

Na nne, BASATA wanasema,

View attachment 1034721

Aya hii imekaa kiswahili kweli kweli. Kwamba kuna Watanzania wengi "waliojitokeza kukemea kitendo cha Msanii Dudubaya" kwa sababu wanaona "hakifai," haimaanishi kwamba mahakama imetoa hukumu ya kisheria. Kisheria tunasema "plausibility does not imply validity." Kwa hiyo, BASATA wametumia sheria za mitaani kana kwamba ni sheria za kimahakama. Wamekosea.

Hivyo, naona kwamba, BASATA wanaendeleza utamaduni mpya wa baadhi ya vyombo vya serikali "kufanya kazi kwa mujibu wa matamko ya wakubwa" badala ya kuangalia sheria inasema nini. Utamaduni huu haukubaliki kwa Watanzania wanaojua na kuheshimu kanuni za utawala bora.

Kanuni moja ya utawala bora ni kanuni ya usawa mbele ya sheria.
Yaani, "the same law should apply to like persons in like circumstances."
BASATA wamezingatia kigezo hiki ? Hapana

Na bahati nzuri ni kwamba, Waziri wa Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe, ni Mwanasheria Nguli. Nimesoma PHD Thesis yake yote. Yuko safi kichwani. Pia ni mlokole mzuri. Wengi tuliona alivyousindikiza mwili wa hayati Samwel Sitta kwa mbwembwe tosha za machozi ya Kilokole. Tunataka imani yenye vibwagizo vya matendo.

Ama sivyo, tutahitimisha kwamba ulokole ule ulikuwa ni usanii, na usanii sio taji lenye heshima kwa mtu mwenye umri kama wa Dr. Harrison Mwakyemba.

Mama Amon.
Hizi nchi zetu bwanaaa,,watu ni maskini mpaka kifikra,, kuna muda unajiuliza hawa watu wa nauelewa kweli,, daah! Aibu nimeona Mimi,, sijui nchi zilizoendelea wanatuchukuliajee,,
 
hahahahahahaaa

wameahindwa kusema dudubaya katamka ambacho hakiruhusiwi

watu wanamsema marehemu Nyerere itakuwa Ruge?
 
Basata yatangaza kumfutia usajili msanii Tumaini Godfrey,
kutokana na kuagizwa na waziri mwakyembe kumchukulia hatua kali,
hii ni baada ya kumsema vibaya marehemu Ruge mtahaba,
kitendo ambacho kimewachukiza wengi.

Inshort,jamaa hatakama alikuwa anamchukia marehemu Sawa
lakini njia aliyochagua kuwasilisha machungu na dukuduku zake ni mbaya Sana,sio njem.

The Future is in Our Brain,Tongue's&Hand's.
Lakin bado hakuna la kumfanya afungiwe hapo,Basata wamefata order ya boss wao na si vinginevyo

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
.
Nimeona tamko, na ningependa kufanya comment mstari baada ya msitari kama ifutavyo:

Mosi, BASATA wanasema:
View attachment 1034718

Aya hii ni taarifa, na haina lolote la kujadili kwani mamlaka hayo yako ndani ya uwezo wa kisheria wa BASATA.

Pili, BASATA wanasema:

View attachment 1034719

Hapa kuna kuna tatizo. Kukamatwa na Jeshi la Polisi ni kutuhumiwa. Kutuhumiwa sio kuhukumuiwa. Katiba ya nchi inasema kila mtu anayo haki ya kuhesabiwa mwenye haki mpaka mahakama inapomtia hatiani. Dudubaya hajatiwa hatiani na mahakama. Kwa hiyo, uamuzi wa BASATA unaweza, na unapaswa kufanyika, baada ya hukumu ya mahakama na sio kabla yake. Kwa hiyo, aya hii inamaanisha kuwa BASATA wamefanya maamuzi yanayokiuka Katiba ya nchi.

Tatu, BASATA wanasema:

View attachment 1034720
Aya hii inaendeleza kosa lililofanyika aya ya hapo juu. Kwamba Dudubaya ni "raia mwema" au kinyume chake ni suala la kuamuliwa na mahakama na sio vingnevyo. BASATA walipaswa kusbiri maamuzi ya mahakama ili wachukue hatua hii. Lakini wameitangulia mahakama. Wamekosea.

Na nne, BASATA wanasema,

View attachment 1034721

Aya hii imekaa kiswahili kweli kweli. Kwamba kuna Watanzania wengi "waliojitokeza kukemea kitendo cha Msanii Dudubaya" kwa sababu wanaona "hakifai," haimaanishi kwamba mahakama imetoa hukumu ya kisheria. Kisheria tunasema "plausibility does not imply validity." Kwa hiyo, BASATA wametumia sheria za mitaani kana kwamba ni sheria za kimahakama. Wamekosea.

Hivyo, naona kwamba, BASATA wanaendeleza utamaduni mpya wa baadhi ya vyombo vya serikali "kufanya kazi kwa mujibu wa matamko ya wakubwa" badala ya kuangalia sheria inasema nini. Utamaduni huu haukubaliki kwa Watanzania wanaojua na kuheshimu kanuni za utawala bora.

Kanuni moja ya utawala bora ni kanuni ya usawa mbele ya sheria.
Yaani, "the same law should apply to like persons in like circumstances."
BASATA wamezingatia kigezo hiki ? Hapana

Na bahati nzuri ni kwamba, Waziri wa Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe, ni Mwanasheria Nguli. Nimesoma PHD Thesis yake yote. Yuko safi kichwani. Pia ni mlokole mzuri. Wengi tuliona alivyousindikiza mwili wa hayati Samwel Sitta kwa mbwembwe tosha za machozi ya Kilokole. Tunataka imani yenye vibwagizo vya matendo.

Ama sivyo, tutahitimisha kwamba ulokole ule ulikuwa ni usanii, na usanii sio taji lenye heshima kwa mtu mwenye umri kama wa Dr. Harrison Mwakyemba.

Mama Amon.
Duh Mama Amon....mbona ni kama flani....kwa nondo hizi mujarabu
 
Back
Top Bottom