Baraza la Sanaa limfungie Bambo kazi zake. Anaharibu sana Kiswahili kwa makusudi

Bambo anawakilisha kiswahili cha makabila yanayopatikana Mkoa wa Ruvuma.

Sasa kama mtu akiongea kiswahili kama Muha labda braza K afungiwe akiongea kama msukuma afungiwe kama mchaga afungiwe (Akina Kiwewe)

Basi makabila yetu yanashida Sana.
Siyo Ruvuma ni Songea wangoni ndiyo wanaongea hivyo
 
Kakae songea ndanindani huko kama Luhagala, Likuyufusi,Nakauga, halafu uje urudi hapa
 
View attachment 3019674
Dickson Samson Makwaya (Bambo)

Baraza la sanaa linashindwa vipi kumuita na kumuonya Bambo aache kuharibu lugha ya kiswahili kwa makusudi.

Huyu kijana nje ya kuharibu lugha yetu ya kiswahili sidhani kama ana kitu anachochekesha.

Ifike mahali sasa aonywe ikiwezekana afungiwe kabisa ,nakumbuka hata wimbo wa Sumalee (Hakunaga) ilibaki hati hati kufungiwa kwa kosa la kuharibu lugha .

Yeye kama msanii ni kioo cha jamii hivyo anatazamwa na wengi, sasa kama yeye anaanza kuharibu lugha inamaanisha wengi atawapoteza haswa kwa wale wageni wasiofahamu vyema lugha ya kiswahili na Wana nia ya kujifunza.
Chai
 
Shida ya Tanzania yetu tunaacha vitu vya msingi kuvipigania tunashughurika na mambo ya kawaida
Kelele za katiba,matibabu ,ufisadi ulipo sasa ni wa kutisha sana ila watu wapo kimya ,elimu nk
Watu wanakuja na mambo ya bambo
 
View attachment 3019674
Dickson Samson Makwaya (Bambo)

Baraza la sanaa linashindwa vipi kumuita na kumuonya Bambo aache kuharibu lugha ya kiswahili kwa makusudi.

Huyu kijana nje ya kuharibu lugha yetu ya kiswahili sidhani kama ana kitu anachochekesha.

Ifike mahali sasa aonywe ikiwezekana afungiwe kabisa ,nakumbuka hata wimbo wa Sumalee (Hakunaga) ilibaki hati hati kufungiwa kwa kosa la kuharibu lugha .

Yeye kama msanii ni kioo cha jamii hivyo anatazamwa na wengi, sasa kama yeye anaanza kuharibu lugha inamaanisha wengi atawapoteza haswa kwa wale wageni wasiofahamu vyema lugha ya kiswahili na Wana nia ya kujifunza.
Eti ww shogo

Mbono uno roho mbayo ivoo

Hutako wenzako tupate riziko?
 
Back
Top Bottom