Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na wadau Dar wakutana katika kikao maalum cha udhibiti kelele

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Katika kikao hicho cha Mei 17, 2023 NEMC ilishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pmaoja na BASATA.

Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
2.jpg

1.jpg
 
Hawa jamaa ndiyo wanaandika majina ya wapiga kelele?
 
Hii NEMC inataka kujipatia sifa kwa vitu vidogo visivyo na maana wala athari kwa wananchi. Eti kelele, kelele zenyewe ni shangwe na furaha kwa wananchi ndio wanakomaa nazo, wanaacha ku deal na uharibifu wa mazingira, ukataji miti hovyo, uchafuzi wa mazingira ya viumbe hai, uchafuzi wa mazingira ya bahari, mito, maziwa na anga wanakimbilia kwenye kelele za shangwe huku wakiacha wale wahuni wa pikipiki na magari yanayotoa mingurumo ya kelele mbaya na moshi unaokera. Kelele za shangwe huwezi kuziwekea ukomo wa kusikika, hata kunong'oneza nako ni kelele inayoweza kukera mtu asiyependa kuisikiliza
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Katika kikao hicho cha Mei 17, 2023 NEMC ilishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pmaoja na BASATA.

Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
Hiyo ni nguvu ya soda tu sheria imetungwa tangu miaka mingi hilio pita wali kuwa wapi?

Mbona makanisa ya kirokole miziki kwenda mbele hawayaoni?

Makampuni ya cm miziki mikubwa hawayaoni?

Mbio za mwenge ukikesha mitaani miziki zinaa usiku kucha watu hawalali hawaoni?

Magereji kwenye mitaa ya watu na viwanda uchafu huo na moshi wa viuma hawaoni?

Mikutano ya wakuu wa mikoa wilaya wabunge miziki mikelele hawaoni?

Wao walicho kiona ni mabaa tu huo ni unafiki mzazi mwenye akili watoto wakikosa hanapiga wote bila kujali mtoto wa kuzaa au wa kambo wote bakora tu
 
Kelele zinapaswa kudhibitiwa maana zinachangia maradhi moyo, presha na matatizo ya afya ya akili. Bila udhibiti wagonjwa watakuwa wengi ktk hospitali zetu
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Katika kikao hicho cha Mei 17, 2023 NEMC ilishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pmaoja na BASATA.

Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
Picha hazina tija tunataka kujua way forward ya ustawi wetu tumechoka na kelele, ukikaa nyumbani kelele za miziki na matofari, ukienda kazini wauza cd na maspika kelele, ukisafiri kwenye mabasi kelele nchi inakuwa kama imetindikiwa
 
Wadau na wamiliki waelimishwe kununua na kutumia sound proof ili wazidi kuzuia kelele
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Katika kikao hicho cha Mei 17, 2023 NEMC ilishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pmaoja na BASATA.

Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
NEMC tekelezeni wajibu wenu makelele siku hizi yamezidi sana ikiwezekana mfanye doria wakati wa usiku kudhibiti wapiga kelele
 
Makelele ni kero kubwa ktk ukuwaji wa uchumi vizuri kama mmeanza kuona umuhimu wa kudhibiti hizo kelele
 
Walikua wapi siku zote umbwa hawa mpk nchi imeharibika na makelele
Wamefika wamefanyia kazi suala limekaa sawa niwakati wa kuwapongeza sio kuwatukana unajua siasa zinaharibu mifumo lakini ya sita imekuja kitofauti sana tuwapongeze sio kuwa tukana
 
Hii NEMC inataka kujipatia sifa kwa vitu vidogo visivyo na maana wala athari kwa wananchi. Eti kelele, kelele zenyewe ni shangwe na furaha kwa wananchi ndio wanakomaa nazo, wanaacha ku deal na uharibifu wa mazingira, ukataji miti hovyo, uchafuzi wa mazingira ya viumbe hai, uchafuzi wa mazingira ya bahari, mito, maziwa na anga wanakimbilia kwenye kelele za shangwe huku wakiacha wale wahuni wa pikipiki na magari yanayotoa mingurumo ya kelele mbaya na moshi unaokera. Kelele za shangwe huwezi kuziwekea ukomo wa kusikika, hata kunong'oneza nako ni kelele inayoweza kukera mtu asiyependa kuisikiliza
Wewe kwa maono yako ivo hivyo lakini suala la kelele za mitetemo zina asali zaidi ya unavyofikiria wewe wajawazito mimba zinatoka watu wanapata ukiziwi wewe unazungumzia shangwe fikiria pia athari zinazopatikana watu wanapata stress wanashindwa kulala wale wanaotaka kumpumzika inakosekana lakini wanadeal na vyote fuatilia mbona kuna viwanda wamefunga juu ya uchafuzi sema umeangalia upande unaokupa faida tu ukasahau upande wa hasara
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Katika kikao hicho cha Mei 17, 2023 NEMC ilishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pmaoja na BASATA.

Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
Hongera saana NEMC kwa hakika wanatimiza wajibu wao katika kiwango cha kuridhisha
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Katika kikao hicho cha Mei 17, 2023 NEMC ilishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pmaoja na BASATA.

Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
Kwa nlichokiona kwa NEMC wanafanya kazi zao kwa utulivu mkubwa na kwa kushirikisha wadau na hivi ndivyo inavyotakiwa ,na wamenifurahisha sana wanavyopambana na kelele kwa kweli kumekuwa na utulivu kidogo kuliko ilivyokuwa mwanzo
 
Hiyo ni nguvu ya soda tu sheria imetungwa tangu miaka mingi hilio pita wali kuwa wapi?

Mbona makanisa ya kirokole miziki kwenda mbele hawayaoni?

Makampuni ya cm miziki mikubwa hawayaoni?

Mbio za mwenge ukikesha mitaani miziki zinaa usiku kucha watu hawalali hawaoni?

Magereji kwenye mitaa ya watu na viwanda uchafu huo na moshi wa viuma hawaoni?

Mikutano ya wakuu wa mikoa wilaya wabunge miziki mikelele hawaoni?

Wao walicho kiona ni mabaa tu huo ni unafiki mzazi mwenye akili watoto wakikosa hanapiga wote bila kujali mtoto wa kuzaa au wa kambo wote bakora tu
Hapa umeenda mbali sana unajua hizi sheria pia zina viwango vya sauti mchana na usiku vinavyokubalika kisheria na suala masuala ya kiimani Mhe Waziri Mkuu aliagiza baraza la Amani likae wajadili hayo ,Hoja yako ipo mikutano sijui matamasha ipo sheria ukiwa kwenye maeneo ya magereji sauti yake ipoje nje ya maeneo ya makazi unatakiwa upige volume ngapi ukiwa eneo la makazi hivyo hivyo sasa fahamu kwanza haya ndo ulaumu lakini kiukweli NEMC imekuja kutibu kidonda cha muda mrefu na sasa mtaani kumepoa
 
Hiyo ni nguvu ya soda tu sheria imetungwa tangu miaka mingi hilio pita wali kuwa wapi?

Mbona makanisa ya kirokole miziki kwenda mbele hawayaoni?

Makampuni ya cm miziki mikubwa hawayaoni?

Mbio za mwenge ukikesha mitaani miziki zinaa usiku kucha watu hawalali hawaoni?

Magereji kwenye mitaa ya watu na viwanda uchafu huo na moshi wa viuma hawaoni?

Mikutano ya wakuu wa mikoa wilaya wabunge miziki mikelele hawaoni?

Wao walicho kiona ni mabaa tu huo ni unafiki mzazi mwenye akili watoto wakikosa hanapiga wote bila kujali mtoto wa kuzaa au wa kambo wote bakora tu
Sio kweli juzi Walikuwa na Kikao na Jumuiya ya Amani ambayo inajumuisha viongozi wa dini zote ,hivyo kwa upande wa taaisis za dini tayari wameshafikiwa na viongozi wa dini walipongeza NEMC na kuahidi kufanyia kazi lakini pia NEMC imekutana na taasisi nyengine ,kwenye hili la kelele naona NEMC wamejipanga na wameweza kutuliza kelele kwq sasa mtaani panakalika na kulalika muda wa usiku
 
Picha hazina tija tunataka kujua way forward ya ustawi wetu tumechoka na kelele, ukikaa nyumbani kelele za miziki na matofari, ukienda kazini wauza cd na maspika kelele, ukisafiri kwenye mabasi kelele nchi inakuwa kama imetindikiwa
Kwa kweli imekuwa kero kubwa lakini naona NEMC wapo serious na swala hili ,kwani kitaalamu pia imegundulika kelele zimekuwa na madhara makubwa kwa jamii ikipelekea ulemavu na hata vifo ,na juzi nimeona wamekutana na kamati ya amani ili kumaliza kelele zinazotokana na taasisi ya dini
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Katika kikao hicho cha Mei 17, 2023 NEMC ilishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pmaoja na BASATA.

Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
NEMC mnafanya kazi nzuri binafsi sisi tunaoishi kwenye mazingira haya ya kelele tumeona nguvu mambo yanakwenda shwari mmefanya jambo zuri kukutana mana iyo itatibu matatizo yenu kwa pamoja na kuwa kitu kimoja tunawapongeza sana msiishie watu hawa kaeni na wenye viwanda na watu wote wanaohusika na uchafuzi wa mazingira
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na wadau mbalimbali kujadili kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.

Katika kikao hicho cha Mei 17, 2023 NEMC ilishirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Brela, WMA, TBS, COSOTA, pmaoja na BASATA.

Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.
Kikao bila kuwepo walokole hakieleweki! Mmewaacha wajinga wale Wana kelele db 400
 
Back
Top Bottom