A
Anonymous
Guest
Kwa zaidi ya miaka 14 sasa, changamoto zinazowakabili wauguzi na wakunga nchini hazijapatiwa ufumbuzi wa kudumu licha ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wanakada hao.
Kwa hali ilivyo sasa, tunaona ni wakati mwafaka kwa wauguzi na wakunga kuungana na kuiomba Serikali kuvunja na kuunda upya Baraza la Uuguzi na Ukunga, kutokana na sababu zifuatazo:
Kwa hali ilivyo sasa, tunaona ni wakati mwafaka kwa wauguzi na wakunga kuungana na kuiomba Serikali kuvunja na kuunda upya Baraza la Uuguzi na Ukunga, kutokana na sababu zifuatazo:
- Viongozi wa Baraza kukosa weledi na uwezo wa kutosha katika kushughulikia changamoto zinazowakabili wauguzi na wakunga.
- Kuendelea kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wanakada bila kupatiwa ufumbuzi wa kuridhisha.
- Usimamizi usioridhisha wa taaluma za uuguzi na ukunga nchini.
- Kushuka kwa ari na morali ya utendaji kazi miongoni mwa wauguzi na wakunga.
- Baadhi ya wauguzi na wakunga kuhamia kada nyingine, huku wengine wakiacha kazi kabisa, hali inayochangia kupungua kwa nguvu kazi katika sekta hiyo muhimu.