Baraza la Wawakilishi Zanzibar latoa fedha zote zilizobakia kabla halijavunjwa kutengeneza Barakoa na kuwagawia wananchi

Baraza la Wawakilishi Zanzibar latoa fedha zote zilizobakia kabla halijavunjwa kutengeneza Barakoa na kuwagawia wananchi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Baraza la wawakilishi Zanzibar ambalo liko kwenye mkutano wao wa mwisho kabla halijavunjwa rasmi limeamua fedha zote zilizobaki kwenye akaunti zitumike kutengeneza Barakoa ambazo zitagawiwa bure kwa wananchi.

Fedha hizo atakabidhiwa makamu wa Rais balozi Seif ili azikabidhi kwa vikosi vya ulinzi watakaotengeneza barakoa hizo.

Naye balozi Seif amewashukuru wawakilishi hao kwa kutopuuzia madhara ya janga hili hatari la Corona.

Chanzo: ITV habari!
 
Huku kwetu waziri jina ameambiwa achunguze maabara
 
Yani mawaziri wa Magufuli ni weupe vichwani hawajiongezi hawajui hata wanaelekea wapi wapo wapo tu.
 
QUOTE="G Sam, post: 35245660, member: 137610"]
Yani mawaziri wa Magufuli ni weupe vichwani hawajiongezi hawajui hata wanaelekea wapi wapo wapo tu.
[/QUOTE]
Sawa. Mbowe ambaye amegomewa na wabunge wake sasa hivi analia tu ndio yuko vizuri. Na Mnyika yuko vizuri na muda so mrefu atamzidi umaarufu Katibu Mkuu aliyemtangulia, Mashinji! Ahahahahahahha!
 
Wazanzibari pamoja na kutawaliwa na Tanganyika bado wana kaustaarabu fulani hivi kenye utu ndani yake. Nahisi uislamu wao unawasaidia katika hilo, unawafanya waone soni kidogo.

The prophet say: The believer’s shade on the day of Resurrection will be his Charity
Ni jukumu letu kuwa na utu na kumuogopa Mungu
Sio kuwa waislam tu bali wote wanaofuata vitabu vinasemaje pia
Angalia wazungu wakipiga debe la mchango kwa kitu Fulani utaona dau linavyopanda haraka
Kutoa sio utajiri bali ni imani tu na malezi

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Wazanzibari pamoja na kutawaliwa na Tanganyika bado wana kaustaarabu fulani hivi kenye utu ndani yake. Nahisi uislamu wao unawasaidia katika hilo, unawafanya waone soni kidogo.
Na ndio maana Kipindi choote cha maraisi waislam tulikua na maisha Mazuri yenye kuheshimiana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom