Nashukuru kwa Kunielewa Mkuu na kuhusu aliyekuwa Msemaji wetu Haji Manara kumsema vibaya CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez alikuwa sahihi tena 100% kabisa sena tu akina Sisi Wabobezi na Waandamizi wa Propaganda akina GENTAMYCINE tuliamua tu Kupambana na Manara ili Kutuliza Hali na Kumuweka sawa CEO wetu Barbara Gonzalez ili ajikite zaidi katika Kuipigania Simba SC yetu.
Lakini cha Kushangaza analeta Dharau, Jeuri na Kiburi hata kwa Watu ambao wanamshauri ( tunamshauri ) halafu wala hatutaki Malipo yake yoyote kwani Umasikini wetu tumeshauzoea, ila tuna Mapenzi ya Kweli na ya Kujitoa Mhanga kwa Simba SC yetu.
Mkuu nina Nyeti Mbili ambazo nazihifadhi Kwanza kwa Maslahi mapana ya Simba SC yangu ( yetu ) kwani najua wana Simba SC wakizijua ( zikienda Public ) Moto mkubwa sana utawaka Klabuni.
Wajitahidi mno Kesho Simba SC ishinde.