Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
=====
Watanzania wanne wameteuliwa kuwa wajumbe kwenye Kamati mbalimbali za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameteuliwa kuwa mjumbe kwenye Kamati mbili.
Kamati hizo ni ya Maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) pamoja na Kamati ya Fedha.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani ameteuliwa kwenye Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ni Mjumbe katika Kamati ya Mashindano ya Klabu.
Mjumbe katika Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya CAF kutoka Tanzania ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha.